TANZIA TANZIA: Getrude Rwakatare, Mbunge na Mchungaji wa Kanisa la TAG (Mlima wa Moto - Mikocheni B) nchini Tanzania, afariki dunia

TANZIA TANZIA: Getrude Rwakatare, Mbunge na Mchungaji wa Kanisa la TAG (Mlima wa Moto - Mikocheni B) nchini Tanzania, afariki dunia

Pole kwa familia yake, Mungu alitoa na Mungu ametwaa jina lake libarikiwe
Tutakukumbuka kwa mengi mama yetu Lwakatre
 
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) na Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto (Mikocheni B Assemblies of God ) Mchungaji Dk. Getrude Lwakatare amefariki dunia Alfajiri ya leo. Mtoto wa amarehemu amethibitisha kifo.


Mtoto wa Marehemu Mama Rwakatare, Mutta Rwakatare amethibitisha kwa kusema

"Ni bahati mbaya imetokea asubuhi ya leo saa 11 kasoro, alikuwa na matatizo ya moyo, jana tulimkimbiza Hospitali lakini bahati mbaya imetokea, tupo katika hatua ya kuangalia namna gani tutafanya ili tuweze kumpumzisha mama yetu" amesema Muta.

2013, Mama Rwakatare alifiwa na Mumewe, Mzee Kennedy Rwakatare. Zaidi soma TANZIA: Mch. Getrude Rwakatare amefiwa na mumewe

2012, Mama Rwakatare aliichongea JF Bungeni. Zaidi soma Mama Lwakatare aichongea JamiiForums

Tutakukumbuka kwa mchango wako kwenye nyanja za elimu na jamii kwa ujumla.

Umepigana vita na mwendo umeumaliza

Upumzike kwa amani!!
R.I.P mama.
 
Nakupa tahadhari nyingine. Usikusanyike kwenye huu msiba maana waumini nyie mkishajazwa yule Roho huwa mnaamini miili yenu imegeuka malaika. Chukua tahadhari!
Sawa Mimi si muumini wake na sijawai kufika Dar. In short huyo ni mtu mkubwa tutaona mwili utakavyo agwa, ...kama wakimzika kimyakimya basi kongole kwa maelezo yako.
 
Hakuna hata muumini mmoja wa mlima wa moto amsemee sifa nzuri bishop lwakatare..pamoja na kumponda mama amefanya mengi mazuri na kuacha alama kubwa

Aliweza kuongoza kanisa, biashara na siasa kwa viwango vya juu kabisa tena kwa wakati mmoja..pia yeye ni mwanzilishi wa kwanza mtanzania wa shule za international schools hapa bongo..alikuwa mwanamke mwenye uthubutu na kiu ya mafanikio ..naamini pengo lake halizibika

Tulikupenda ila Mungu nakupenda zaidi..

Go safe mama lakwatare
 
Back
Top Bottom