Kama taarifa hii ni kweli, basi tumwombee Mungu aiweke roho yake pema peponi.
Kulingana na vyombo vya habari Uganda, wiki mbili au tatu zilizopita jamaa huyu akiwa Kampala katika maisha yake ya kawaida aligundua kuwa kuna mtu aliuza nyumba zake kadhaa kinyemelea bila yeye mwenyewe kujua. Hiyo ilimsitua sana kwa vile alishabadilisha umiliki wa nyumba zote zile pamoja na biashara zake zote na jina la Zari halikuwapo tena ila yeye peke yake; nadhani akidhania kuwa ni Zari kamchezea hivyo, akaamua kutangaza kuuza ile nyumba ya ghorofa moja aliyokuwa amemjengea mama yake Zari ambayo inasemekakana nayo ilikuwa katika jina lake Ivan peke yake. Mauti yamemkuta kabla nyumba hiyo haijanunuliwa. Nadhani mgawanyo wa mali zake utaleta mzozo sana katika familia yake kama hakuacha makaratasi mazuri kisheria; basi Zari atashinda na atachukua kila kitu pamoja na vituko vyote alivyomfanyia katika maisha.