Tusker Bariiiidi
JF-Expert Member
- Jul 3, 2007
- 5,554
- 2,160
Habari nilizozipata usiku huu ni kuwa Mama Mengi is no more. Mama Mercy Mengi amefariki dunia usiku wa November 1,2018 katika hospitali ya Mediclinic Morningside Afrika Kusini akipatiwa matibabu.
Marehemu Mercy Mengi alikuwa nchini Afrika Kusini kwa zaidi ya wiki mbili akipatiwa matibabu, lakini mpaka sasa bado haijawekwa wazi ugonjwa uliosababisha kifo chake.
Mrs Mercy Mengi ninmama yake Regina, Marehemu Mutie na Abdiel (Mke wa kwanza wa Reggy Mengi)
Mwili utasafirishwa kuletwa nchini
RIP Mama.
=====
Mfanya biashara maarufu Tanzania Reginald Mengi amefiwa na aliyekuwa Mke wake wa kwanza, Mercy Mengi usiku wa kumkia November 1,2018 katika hospitali ya Mediclinic Morningside iliyopo Afrika Kusini akiwa anapatiwa matibabu.
Inaelezwa kuwa Marehemu Mercy Mengi alikuwa nchini Afrika Kusini kwa zaidi ya wiki mbili akipatiwa matibabu.
VILIO na simanzi jana vilitawala maeneo karibu yote ya Mji wa Moshi na baadaye katika makaburi ya familia ya Mangi Shangali, wakati mwili wa aliyekuwa mmoja wa waanzilishi wa Kampuni za IPP, Mercy Anna Mengi, ulipowasili kwa ajili ya kuhitimisha safari yake ya mwisho duniani.
MWENYEKITI MTENDAJI WA MAKAMPUNI YA IPP, DK. REGINALD MENGI NA WATOTO WAKE, REGINA NA ABDIEL WAKIWEKA SHADA LA MAUA KWENYE KABURI LA ALIYEKUWA MWANZILISHI MWENZA WA MAKAMPUNI YA IPP, MAREHEMU MAMA MERCY ANNA MENGI, WAKATI WA MAZISHI YAKE YALIYOFANYIKA KATIKA ENEO LA WARINDOO MMASENI, MACHAME, MKOANI KILIMANJARO JANA. PICHA: SELEMANI MPOCHI
Shughuli zilisimama kwa muda katika maeneo hayo kati ya saa 4:00 asubuhi na saa 7:30 mchana wakati msafara mkubwa wa mamia ya waombolezaji ulipokuwa ukienda Machame Wari, wilaya ya Hai ambako mwili wa mwasisi huyo ulizikwa.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Fredrick Shoo, ndiye aliyeongoza ibada ya mazishi hayo iliyofanyika Kanisa Kuu la Usharika wa Moshi Mjini.
Dk. Shoo alipokuwa anaeleza namna alivyomjua Mama Mercy Anna Mengi, alisema alikuwa mwanamke jasiri katika maisha yake duniani.
Mamia ya waombolezaji waliokuwapo katika maeneo ambayo msafara huo ulipita, waliacha kwa muda shughuli zao na kujongea pembeni mwa barabara kushuhudia umati wa watu waliokuwa katika magari, pikipiki na wengine wakitembea kwa miguu wakielekea makaburini.
Waombolezaji walianza kuwasili saa 3:00 asubuhi katika Usharika wa Moshi Mjini, kusubiri mwili wa Mercy Anna Mengi kuondolewa nyumbani kwake Shanty Town na kupelekwa kanisani kwa ajili ya ibada ya mazishi.
Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Moshi Mjini, Timoth Meena, akisaidiana na Mchungaji Deogratius Msanya wa Usharika wa KCMC, ndio walioongoza Liturgia katika ibada maalum ya kumwombea marehemu.
UJUMBE WA DK. SHOO
Askofu Dk. Shoo aliwaongoza waombolezaji akiwamo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kutoa heshima za mwisho kwa kuuaga mwili huo.
Baada ya shughuli za kuaga kumalizika na baadaye kufanyika ibada ya mazishi hayo, Dk. Shoo alisema: “Mama Mercy, mimi namfananisha na Debora, huyu mwanamke aliyetajwa katika Biblia kwa sababu ya jinsi nilivyomfahamu kutokana na maana ya jina lile la Debora.
"Debora maana yake ni nyuki, na nyuki huwa anatupa mambo mawili, huwa anatupa asali ambayo ni tamu lakini vilevile nyuki ni mkali. Debora anakumbukwa kwa heshima na taifa la Israel mpaka leo.
“Nimekuwa nikijiuliza hivi sisi kwa mama ambaye ametuachia mfano wa mambo mengi ya maendeleo, tunawezaje kuweka kitu cha kumkumbuka kama Waisrael walivyofanya kuweka kumbukumbu ya Debora kwa vizazi vijavyo.
"Na kwa kweli katika kutafakari likatokea wazo kwamba tunahitaji kuwaenzi kina mama wanaofanya mambo makubwa katika jamii yetu.
“Likanijia wazo Kampasi ile ya Machame ambayo itakuwa Makao Makuu ya Chuo Kikuu chetu (Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Askofu Stephano Moshi (SMMUCo), mimi nimesema kwa heshima ya mama huyu (Mercy) tuta-'dedicate' (pendekeza), moja ya mabweni ya wanawake yaitwe jina la Mercy Anna Mengi.”
Dk. Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT, alisisitiza katika ibada hiyo kwamba anamwomba Mungu awawezeshe familia pamoja na kaka yake kiumri ambaye ni Dk. Regnald Mengi, watoto Regina na Abdiel, waombe jambo hilo lifanikiwe.
“Ninachowaomba mwandae 'portray' (picha nzuri) ya mama Mercy Anna, tutakayoiweka katika ukuta, mlangoni mwa bweni hilo. Kaka yangu Dk. Mengi, kwenu watoto Regina na Abdiel, ndugu wa nyumba ya Mangi Shangali, tunamsihi Mungu awape faraja, awaongoze, awajalie tumaini na amani moyoni mwenu,," alisema Askofu Shoo.
Awali, akiwa katika ibada hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira, alisema wananchi wa mkoa huo watamkumbuka marehemu kwa mengi.
Alisema ukiacha yaliyotajwa na familia na yaliyotajwa kwenye historia, yapo yanayoleta pengo moja kwa moja katika ujenzi wa taifa letu kwa kuwa alikuwa mtu mwenye nguvu, mwenye afya na ari kubwa sana ya kufanya kazi na kutumikia watu.
“Tunaposimama na kuona chombo hiki chenye mwili wake (jeneza), tujue familia inashuhudia kwamba mama kweli alikuwa mama wa familia, alikuwa mama anayemtegemea Mungu, alikuwa mama wa kanisa na tulikuwa tunamfuatilia hivyo tangu umauti ulipompata, alipoletwa Dar es Salaam, Usharika wa Azania Front wametuonyesha na tumeona upendo wake wakati wa uhai na hata baada ya uhai wake,”alisema kiongozi huyo.
Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la KKKT, Dk. Alex Malasusa akitoa salamu zake, alisema licha ya kutambua maisha ya mama huyo kwa muda mrefu ambayo amekuwa akiishi kwa kumtegemea Mungu katika dayosisi anayoiongoza, alizaliwa na kukulia Dayosisi ya Kaskazini.
Abdiel Mengi, mtoto wa marehemu, wakati anatoa shukrani kwa waombolezaji walioshiriki katika kanisa hilo, alimwelezea mama yake kuwa alimtanguliza Mungu katika maisha yake.
"Mama alimtegemea Mungu katika shida na raha, mama alibarikiwa sana kwa kipaji cha kutunza na kuunganisha familia yetu yote, mama ametuacha watoto wawili wa kuzaa Regina na mimi mwenyewe, kaka yetu (Rodney) ameshatangulia mbele za haki," alisema na kuongeza:
"Mama ameacha watoto wa kulea wengi ambao pia watakuwa ni mashuhuda wa mapenzi ya mama anayemtegemea Mungu, msingi aliotujengea mama yetu ni unyenyekevu na uchapakazi kiimani.
"Daima tutamkumbuka mama kwa hekima na misimamo yake, busara na ushauri wake, utulivu na ujasiri wake, utumishi na ukarimu wake na zaidi ya yote tutamkumbuka mama yetu kwa upendo wake wa dhati, upendo usiotetereka, upendo usiobagua familia wala wenye shida, wala wenye raha. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake la Bwana lihimidiwe."
VIONGOZI, WANASIASA
Mazishi ya marehemu Mercy Anna Mengi yaliwakutanisha pamoja viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa akiwamo Makamu wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu mstaafu, John Samwel Malecela, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, wabunge, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi.
Mercy Anna Mengi alizaliwa Aprili 13, 1948 katika Kijiji cha Wari, Machame mkoani Kilimanjaro kwa wazazi wake, Mangi Mwitori Heri Abdiel Shangali na Anna-Amen Masomi Shangali.
Alipata elimu ya awali katika Shule ya Msingi Native Authority, Nkwalebwe na baadaye alijiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana Machame ambako aliendelea na masomo ya Middle School na sekondari.
Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, mwaka 1966 alijiunga na Chuo cha Kianda Secretarial, Kenya.
Alipohitimu chuoni hapo, aliajiriwa na East Africa Community katika shirika lake la East African Airways, Nairobi, Kenya na baadaye alihamia Tanzania akiwa anafanya kazi katika shirika hilo.
www.jamiiforums.com

TANZIA - Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Abraham Mengi afariki dunia akiwa Dubai, UAE
Taarifa rasmi zinaonyesha kuwa Mzee Reginald Abraham Mengi(77yrs) amefariki dunia. Mengi amefikwa na umauti akiwa huko Dubai (UAE) alikokuwa kwa matibabu. Mzee Mengi alizaliwa mwaka 1942 mkoani Kilimanjaro. Update: ITV wamethibitisha HISTORIA YA MENGI KWA UFUPI Dr. Mengi alizaliwa mwaka...