TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama(CCM) afariki dunia

TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama(CCM) afariki dunia

Tunatembea na kifo,kwa hiyo ni sekunde yoyote unakufa
Ni kweli lakini hakuna kifo kisicho na sababu, kuugua, ajali,hata kifo cha ghafla sio ghafla kwani wengi huwa na magonjwa ya Moyo.
 
View attachment 636895

TAARIFA YA AWALI:


Wadau nimepata taarifa muda huu zinasema mbunge wa Songea mjini Mh. Leonidas Gama hatunaye tena....

UPDATE:

JamiiForums imepata uthibitisho wa taarifa za kifo cha Mhe. Gama ambacho kinadaiwa kutokea muda wa Saa 6 kuelekea Saa 7 usiku wa kuamkia leo.

Amefariki akiwa mbunge wa Songea Mjini na amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hii Songea katika Hospitali ya Peramiho.

Gama amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. Vilevile amewahi kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro.

Inadaiwa marehemu Gama alianguka nyumbani kwake saa saba usiku juzi huko Likuyu; akapooza upande wa kushoto akawa hajitambui kabisa na akapelekwa Hospitali ya Peramiho ambako aliwekewa mashine za kumsaidia kupumua.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi.

========

Updates
Chama cha Mapinduzi chatuma salama za rambirambi kwa familia

View attachment 637060

View attachment 637146
View attachment 637147
apumzike kwa amani
 
Back
Top Bottom