TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama(CCM) afariki dunia

TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama(CCM) afariki dunia

Ivi yale mazoezi ya kila mwisho wa mwezi nchi nzima yaliishia wapi!
 
hiyo ni km kuelekeza lawama kwa marehem juu ya maisha yake kwa kutokuwa muangalifu juu ya afya, haipendez, ilitosha tu kusema RIP
Kama kila mtu ataandika RIP itakuwa nini, hata kwenye misiba huwa kuna mawaidha ya kutuonya tuliobaki, kwahiyo Paschal yuko sahihi kabisa kutuonya tupunguze uzito.

Mungu amuweke Mahali panapomstahili.
 
RIP kiongozi, sina shaka kwa ule mwili nadhani kila aliyekuwa akikutana naye alitamani kumtahadharisha/kumwambia kitu.
 
Apumzike kwa amani mkuu Gama,Mbele yake nyuma yetu.
 
..duh...ni lile limwili....sipati picha mshindo wa kuanguka na uzito ule...haya maisha yana mwisho....maana hatujui lini israel atakuja kuchukua kilicho chake....sidhani kama wengi wanalijua hili huko ccm wenye mavitambi na roho mbaya zenye chuki mithili ya kutaka wenzao wa upinzani wafe....nafasi ya ubunge hiyo upinzani wachangamkie....RIP mbunge....
 
Ivi yale mazoezi ya kila mwisho wa mwezi nchi nzima yaliishia wapi!
Mazoezi ya mara moja kwa mwezi hayana faida yoyote kiafya zaidi ya kupoteza muda na fedha. Kiafya mazoezi yanatakiwa kufanyika kila siku, au angalau mara tatu kwa wiki.
 
..duh...ni lile limwili....sipati picha mshindo wa kuanguka na uzito ule......nafasi ya ubunge hiyo upinzani wachangamkie....RIP mbunge....
Leonidas Gama alikuwa Kiongozi wa mbio za mwenge , na alifungua kituo cha kwanza cha Polisi kidogo hapa Dodoma miaka ile ya Mrema.
Ni kijana aliyezaliwa Ikulu
ni mtu wa mazoezi
kila mtu kifo kitamkuta hata awe nani
RIP Gama
 
..duh...ni lile limwili....sipati picha mshindo wa kuanguka na uzito ule...haya maisha yana mwisho....maana hatujui lini israel atakuja kuchukua kilicho chake....sidhani kama wengi wanalijua hili huko ccm wenye mavitambi na roho mbaya zenye chuki mithili ya kutaka wenzao wa upinzani wafe....nafasi ya ubunge hiyo upinzani wachangamkie....RIP mbunge....
Roho za aina hii sijui mnazipata wapi!!?
 
..wao ccm wameonyesha wasivyojali madhila yawapatayo wenzao wa upinzani..rejea kina Lissu kupigwa risasi....nani alisimama bungeni kwa wabunge hawa kukemea tukio lile???au anapokufa mtu wa ccm ndio ahurumiwe????....huwa tunawaambia kila mara mnaposhabikia madhila ya wenzenu na nyie mjue kuna kufa....na njia ya kifo kwa wote ni hii ya natural death....hili ni angalizo.... Kwa viongozi wote...wa upinzani na wa ccm...na RAIA wote....kifo hakina unafiki.....hii ndio ilikuwa hoja yangu...upende usipende...

Roho za aina hii sijui mnazipata wapi!!?
 
RIP Gama ila alikuwa na mwili mkubwa mno kiasi kwamba magonjwa nyemelezi yalikuwa rahisi kumshambulia kama pressure, cardiac failure, diabete n.k
 
Back
Top Bottom