Dah Seki jamani,alikuwa mchangamfu sana ,kumbe alikuja kuingia kwa wa bongo movie?RIP seki tulidiscuss sana metalic minerals,sitamsahau ucheshi wake,kama amekuwa bilionea na kuwekeza basi kijana nimemsifu kwa kweli.
Ama kweli dunia ni mapito Seky umeniuma sana naomba mwenyezi mungu akupumzishe kwa amani jamani kwa sasa niko nchini Ghana kiasi fulani sikupata mda wa kupitia baadhi ya habari kutokana na ubize wa kazi,nilipata hizi habari kwa shituko sana maana huyu ndugu alikua mcheshi sana tu yaani unavyomuona kwenye picha hiyo ndo ilikua tabasamu ya utambulisho wake.
Namkumbuka marehemu pale UDSM kitovu cha FOE akiwa ansoma Mining Engineering 2003-2007 kipindi hicho haijawa COET ucheshi , vituko na mengine mengi yalimfanya marehemu kua ng'aavu sana chuoni.
Nakumbuka mwaka 2006 tulipangiwa wote kwenda Field Buhemba Gold Mine wanafunzi wote wa mwaka wa tatu tukaishi nyumba moja tukiwa tunaangalia finaly za kombe la dunia tim aliyokua akishabikia ni Italy, ilipochukua ubingwa alifurahi sana.
Jamani naona watu wanachanganya mambo kidogo hapo,Seky tumemaliza nae UDSM mwaka 2007 akapata ajira huko Arusha Tanzanite basi tokea pale nikawa nasikia tu habari zake,mara kafunga bonge la harusi kua sehemu husika palilindima nk.
Habari ya kifo chake imenisikitisha sana nabaki na maswali kadhaa na chanzo cha kifo chake,
Mara alikua amekalia hivyo vi coffee table kimevunjika na kumkata
Alikua uchi ama kwenye taulo
Mtoto wake mdogo alikua kambeba mara kamuweka kwenye sofa
Alikua na ugomvi na kasukumwa kaangukia kimeza na vipande kumchoma kwenye shingo,mara tumboni,mara pajani ni wapi alipochomwa
Naona kama chanzo cha habari kinatatanisha ama kuna nini kimefichwa,