TANZIA: Mwanahabari mkongwe, Bi Sarah Dumba afariki dunia ghafla akiwa Njombe

TANZIA: Mwanahabari mkongwe, Bi Sarah Dumba afariki dunia ghafla akiwa Njombe

Jamani kuna umuhimu wa kuheshimu umri wa kustaafu na kukubali kupumzika, vifo vingine vya kujitakia hivi, tangu nimemsika redioni sijaanza shule leo na mimi nafanya kazi nae yumo tu? Hizi presha zingine nazo ni mwili kuchoka kutokana na umri kushindwa kutimiza wajibu, ajabu kwetu wastaafu ndio wana ajiriwa upya! R.I.P .
nimeipenda sana hii....wateule wengi wa rais wanapewa nafasi ngumu za uongozi wakiwa wamechoka, mfano mwanajeshi kastaafu miaka 65 anapewa ukuu wa mkoa wakati kajichokea, hawezi kwenda na kasi iliyopo.. akisikia tu Majariwa anakuja..BP juu
 
Asant Mungu kwa kuvuna ulicho panda.MPUMZISHE MAHALI pema, Mama cheichcei.
 
Yatupasa kumshukuru Mungu kwa kila jambo,Pumzika mama,pumzika,dada,pumzika rafiki,pumzika shangazi,pumzika kiongozi..Mwenyezi Mungu anayo makusudi kuruhusu kifo chako wakati huu na namna mauti yalivyokupata..Yatupasa kuyaenzi mema na mazuri yako tukikuombea rehema kwa mapungufu.Poleni wafiwa wote
 
Hukumsikia mkuu wa mkoa akisema sababu ni kazi nyingi, na harakati za kuandaa wiki ya maji zimechangia kuongeza wingi wa majukumu kwake? Mpaka presha imepanda lazima mwili umechoka kwa umri wake kuna kiasi cha majukumu, unaelewa sababu ya kustaafu? Au unafikiri ni kupisha tu mtu mwingine kwenye nafasi yako? Wewe ndio um ewaza kitoto.

Nadhani unayo matatizo wa uelewa wa lugha muafaka unayoweza kutumia katika kujenga hoja na kwa wakati muafaka. Unajua maana ya neno 'kujitakia'? Ndugu yangu, sina hakika na umri wako wala nafasi yako katika jamii hii, wala elimu (ingawa elimu haina maana sana kwani wako wengi ambao hawana elimu lakini wana busara kubwa) yako. Pia kwa hakika sifahamu hata itikadi yako. Sitaki kuendelea kutoa maoni yangu kwa suala hili lakini niseme tu kuwa ukisema hadharani dhidi ya mwenzio (hata ambaye hamuelewani) aliyekufa kuwa kifo chake kimekuwa cha 'kujitakia' huwezi ukaeleweka kwa waungwana katika jamii. Katika baadhi ya jamii ukisema hivyo ni lazima utaitwa mchawi.

Kuhusu suala la kustaafu kwani wewe hujawahi kuona watu wamestaafu lakini bado wanapewa majukumu mazito ndani ya jamii? Na huu ni utaratibu wa dunia nzima. Huwezi ukasema wastaafu wote ni marufuku kufanya kazi. Hiyo haipo duniani. Ukienda ulaya, Asia, Russia, Marekani ya Kusini, uarabuni na kadhalika na bila shaka Afrika wastaafu kadhaa bado kazini wapo na wanadunda kwa majukumu muhimu na nyeti ya kitaifa.
 
Sauti ya Mama Sarah Dumba imeondoka. Sauti iliyojaa ukakamavu, tumekua enzi zile za RTD tukiisikia sauti yake. RIP Mama. Sauti ya Julius Nyaisanga imeondoka, sauti ya Dominic Chilambo iliondoka siku nyingi zilziopita, sauti nzito ya David Wakati na yenyewe haipo tena. Maisha ni mafupi sana, ni kama vile wiki iliyopita wakati miamba hii ilipokuwa ikitamba radioni.
 
Jamani kuna umuhimu wa kuheshimu umri wa kustaafu na kukubali kupumzika, vifo vingine vya kujitakia hivi, tangu nimemsika redioni sijaanza shule leo na mimi nafanya kazi nae yumo tu? Hizi presha zingine nazo ni mwili kuchoka kutokana na umri kushindwa kutimiza wajibu, ajabu kwetu wastaafu ndio wana ajiriwa upya! R.I.P .
kweli ndio alikuwa na miaka 60 kamili
 
mama kaacha historia ya kipekee, dereva wake aliyekuwa anamwendesha mpaka mauti yalipomkuta ndio mkwe wake kwa binti yake wa kwanza.
 
Back
Top Bottom