TANZIA: Mwanahabari mkongwe, Bi Sarah Dumba afariki dunia ghafla akiwa Njombe

nimeipenda sana hii....wateule wengi wa rais wanapewa nafasi ngumu za uongozi wakiwa wamechoka, mfano mwanajeshi kastaafu miaka 65 anapewa ukuu wa mkoa wakati kajichokea, hawezi kwenda na kasi iliyopo.. akisikia tu Majariwa anakuja..BP juu
 
Asant Mungu kwa kuvuna ulicho panda.MPUMZISHE MAHALI pema, Mama cheichcei.
 
Yatupasa kumshukuru Mungu kwa kila jambo,Pumzika mama,pumzika,dada,pumzika rafiki,pumzika shangazi,pumzika kiongozi..Mwenyezi Mungu anayo makusudi kuruhusu kifo chako wakati huu na namna mauti yalivyokupata..Yatupasa kuyaenzi mema na mazuri yako tukikuombea rehema kwa mapungufu.Poleni wafiwa wote
 

Nadhani unayo matatizo wa uelewa wa lugha muafaka unayoweza kutumia katika kujenga hoja na kwa wakati muafaka. Unajua maana ya neno 'kujitakia'? Ndugu yangu, sina hakika na umri wako wala nafasi yako katika jamii hii, wala elimu (ingawa elimu haina maana sana kwani wako wengi ambao hawana elimu lakini wana busara kubwa) yako. Pia kwa hakika sifahamu hata itikadi yako. Sitaki kuendelea kutoa maoni yangu kwa suala hili lakini niseme tu kuwa ukisema hadharani dhidi ya mwenzio (hata ambaye hamuelewani) aliyekufa kuwa kifo chake kimekuwa cha 'kujitakia' huwezi ukaeleweka kwa waungwana katika jamii. Katika baadhi ya jamii ukisema hivyo ni lazima utaitwa mchawi.

Kuhusu suala la kustaafu kwani wewe hujawahi kuona watu wamestaafu lakini bado wanapewa majukumu mazito ndani ya jamii? Na huu ni utaratibu wa dunia nzima. Huwezi ukasema wastaafu wote ni marufuku kufanya kazi. Hiyo haipo duniani. Ukienda ulaya, Asia, Russia, Marekani ya Kusini, uarabuni na kadhalika na bila shaka Afrika wastaafu kadhaa bado kazini wapo na wanadunda kwa majukumu muhimu na nyeti ya kitaifa.
 
Sauti ya Mama Sarah Dumba imeondoka. Sauti iliyojaa ukakamavu, tumekua enzi zile za RTD tukiisikia sauti yake. RIP Mama. Sauti ya Julius Nyaisanga imeondoka, sauti ya Dominic Chilambo iliondoka siku nyingi zilziopita, sauti nzito ya David Wakati na yenyewe haipo tena. Maisha ni mafupi sana, ni kama vile wiki iliyopita wakati miamba hii ilipokuwa ikitamba radioni.
 
kweli ndio alikuwa na miaka 60 kamili
 
mama kaacha historia ya kipekee, dereva wake aliyekuwa anamwendesha mpaka mauti yalipomkuta ndio mkwe wake kwa binti yake wa kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…