Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 20,137
- 26,189
Msanii Sam wa ukweli hatunaye tena duniani, amefariki usiku huu hospitali ya Palestina iliyopo Sinza
Mwili wa Sam umepelekwa hospitali ya Mwananyamala kuhifadhiwa.
Sam, alitamba na vibao vyake kama, ‘Lonely’, ‘Usiniache’, ‘Sina Raha’, ‘Hata Kwetu Wapo’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva.
Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
=======
Msanii wa Bongo Fleva, Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni 7, 2018 baada ya kuugua na mwili wake kupelekwa katika hospital ya Mwananyamala.
Taarifa hiyo imethibitishwa na msambazaji wa nyimbo zake na Meneja wa ‘Team Mtaa kwa Mtaa’, Amri the Business ambaye aneeleza kwa masikitiko makubwa kuwa Sam amefariki dunia na kumtakia kupumzika kwa amani.
“Siamini kilichotokea muda huu ila sina jinsi, kwani woote safari ni moja, pumzika kwa amani Sam wa Ukweli, hakika nilikupenda kama ndugu yangu wakuzaliwa tumbo moja, #rip” amesema Amri the Business.
Pia, aliyekuwa mtayarishaji wa nyimbo za Sam wa Ukweli, Steve amesema Sam alikuwa akiumwa na walipomuuliza alisema ni UKIMWI wa kulogwa.
Baadhi ya Video zake