TANZIA
Nguli wa habari nchini Tanzania, Marin Hassan Marin amefariki dunia leo Aprili 1, 2020 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam. Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Martha Swai.
Utangulizi
Marehemu Marin Hassan Marin alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania hadi umauti ulipomfika tarehe 01/04/2020. Marehemu amefariki ghafla nyumbani kwake hapa Dar es Salaam leo tarehe 01/04/2020.
Elimu
Marehemu alizaliwa tarehe 15/07/1972. Alihitimu elimu ya stashahada ya Uandishi wa Habari mwaka 2004.
Ajira
Marehemu aliajiriwa na iliyokuwa Taasisi ya Utangazaji Tanzania tarehe 01/05/2005 kama Mwandishi wa habari Daraja la II. Marehemu alipanda madaraja mbalimbali hadi kufikia katika cheo cha Mwandishi wa Habari Mwandamizi cheo alichokuwa nacho mpaka umauti ulipomfika.
Wengi wetu ndani na nje ya TBC tutamkumbuka marehemu Marin Hassan Marin kwa mema yake ikiwemo uchapa kazi wake, kujitolea na ushirikiano na wenzake. Amelitumikia Shirika la Utangazaji Tanzania kwa uaminifu na uadilifu mkubwa kwa kipindi chote miaka kumi na tano (15).
Marehemu ameacha Mke na Watoto.