TANZIA: Mwandishi nguli wa Habari Marin Hassan Marin afariki dunia

TANZIA: Mwandishi nguli wa Habari Marin Hassan Marin afariki dunia

Apumzike Kwa Amani Mkongwe Marin, ingawa ni muda mrefu sijamsikiliza wala kumuona kutokana na huu utandawazi na utitiri wa media.

Nitakukumbuka kwa utangazaji wako mahiri wa kiswahili fasaha, ulioambatana na utamkaji wa maneno kimadaha.
 
TANZIA

Nguli wa habari nchini Tanzania, Marin Hassan Marin amefariki dunia leo Aprili 1, 2020 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam. Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Martha Swai.

Alikuwa anajua sana huyu mzee


Rip Marin
 
Ni miongoni mwa waandishi wachache Mahiri aliyekufa masikini .
Kazi ya uandishi wa habari ni noble professional kama ilivyo kazi ya aulimu, polisi, zimamoto, na kazi za kanisa, ni kazi ya wito na ni kazi ya kujitolea.

Sio haki kusema amekufa masikini, kwasababu umasikini na utajiri ni relative, sisi waandishi wa habari wa kitaifa, wote maisha yetu ni ya kawaida sana, sio masikini, sio matajiri it depends.

Kule kwenye Usukumani watu wanatembea kwa miguu, mtu mwenye baiskeli ndie tajiri na anagombewa na wanawake.

Tudumishe Uafrika wetu na Utanzania wetu kwa kuzungumza yale mazuri tuu ya Marehemu.
RIP Marine Hassan Marine
P
 
R.I.P mwamba wa habari.........wote njia yetu moja....ila namna ya kuelekea huko inatofautiana,,,,
 
Back
Top Bottom