Mimi ni Mtumishi wa Umma, ninahofu na usalama wa Taarifa zangu binafsi na za Utumishi kutumiwa na watu wasio sahihi.
Jumamne ya tarehe 3/12/2024 mtu mmoja mwenye namba 0768***684 ambaye baadaye nilibaini ni tapeli alijitambulisha kwamba ni Afisa Utumishi Mkoa wa Mwanza, alikuwa akiwapigia Watumishi wa Umma hasa toka Wilaya ya Ilemela kwa lengo la kuwatapeli.
Hoja yake kubwa ilikuwa ni kwamba Taarifa za Watumishi anaowapigia simu zimekosewa katika mfumo wa ESS, hivyo inabidi waongee nae vizuri ili awarekebishie sababu kuna watu zaidi ya 34 washafukuzwa kazi kutokana na makosa hayo ya taarifa za kiutumishi.
Hofu yangu juu ya Usalama wa Taarifa za Utumishi ni kwamba hawa matapeli walikuwa na Taarifa Binafsi za Mtumishi kuanzia shule aliyosoma, Index Number ya Cheti cha Kidato cha Nne, namba ya simu, mwaka alioanza kazi na eneo analoishi Mtumishi.
Taarifa hizi Mtumishi anajaza kwa mwajiri wake, swali ni kwamba hawa matapeli wanawezaje kupata access ya taarifa hizi nyeti za watumishi? Wanazitolea wapi?
Mfano kuna Mtumishi mwenzangu mwingine anadai yeye alipigiwa na namba hiyo ya tapeli, akamwambia kuna makosa katika taarifa zake na ni ukweli kabisa taarifa zake hazijakaa sawa katika mfumo, sasa hawa matapeli walijuaje jambo hilo?
Kitando cha tapeli huyo kutumia Taarifa Binafsi kutaka kuwatapeli Watumishi inaleta hofu juu ya usalama wa Taarifa Binafsi na faragha za Watumishi. Inakuwaje tapeli anakuwa na taarifa sahihi za Mtumishi na hata mapungufu ya taarifa za mtumishi anazijuaje?
Hawa watu wanatoa wapi hizi taarifa au kuna mtu aliekabidhiwa dhima ya kulinda hizi taarifa amekua anazivujisha kwa watu kwa faida yake binafsi?
Pia kumekuwa na tabia ya Watumishi kutumiwa meseji za mikopo kutoka taasisi mbalimbali za mikopo. Je, hizi namba za simu za Watumishi haya makampuni ya mikopo wanazitolea wapi?
Wito wangu nikuwa kama mdau Serikali inatakiwa ichukue hatua katika kulinda taarifa binafsi na faragha za watumishi wake.
Taarifa hizi zikiangukia mikononi mwa watu wasio waaminifu madahara yake ni makubwa sana.
Tukio la jumanne inawezekana kuna baadhi ya Watumishi ambao hawakujipa muda wa kutafakari watakua wamtapeliwa pesa zao maana uyo tapeli alikuwa anaongea na sauti ya mamlaka na kusema inabidi utoe chochote ili taarifa zako ziwekwe sawa la sivo unafukuzwa kazi.
Pia soma:
~ Mamlaka zishughulikie changamoto za Mfumo wa ESS kwa Watumishi
~ Serikali iangalie hii changamoto ya Mfumo wa ESS, kuhusiana na Uhamisho