Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Hivi ukinunua silaha nje ya nchi unaweza kuisajiri/kuja nayo Tanzania?
 
Tengeneza Manati haina mlolongo ...joke..

Ngoj waje wataalamu mi Mwenyew Nipate elimu
 
Kumiliki silaha yoyote mkuu kisheria ni utumwa sana kwa nchi kama tz yaani process na maisha yako na condition za kucomply na maisha ya ukaguzi hautotofautiana na mtu mwenye kesi ya jinai the way utakuwa unaripoti mara kwa mara polisi.
Nakushauri uachane nayo mkuu boresha ulinzi unaotumia sasa basi.
 
Mchakato huanza kwa kuinunua kutoka Duka la Silaha na kwa hapa Dsm yapo Mawili tu Moja pale Pembeni mwa Diamond Jubilee na Lingine Pembeni mwa TRA ya karibu na Station!

Ukinunua unapewa risiti bila ya Silaha husika na unapewa Muda wa Miezi Sita kufuatilia vibali

Mchakato wa Vibali unaanzia Serikali ya Mtaa Mpaka kwa Mkuu wa Wilaya ambako Kamati ya Ulinzi na Usalama itaketi na kukujadili na ukishathibitishwa ndio itaenda kwa Jeshi la Polisi na ukishathibitishwa unapewa Document ya Umiliki ambayo ndio utaitumia kuonesha Kwny Duka la Silaha ili upewe Silaha yako.

Zipo aina mbalimbali za Silaha kutegemea Kiwango ha Pesa yako na uhodari na uzoefu wako wa kujenga Shabaha kwa kuwa kuna zingine Zina hitaji uzoefu

Ushauri wangu kwako Kama huna strong reasons usihangaike kuimiliki kwa kuwa baada ya Muda Mfupi hugeuka kuwa Mzigo na inaweza hata ikapelekea kukupeleka Gerezani!

Mie Nina cha kwangu cha Miaka Mingi kiasi lakin kwa Mazingira yangu naanza kuhisi Mzigo na hasa kadri umri unavyoyoyoma maana Siku hizi Silaha yenyewe ndio bidhaa inayotafutwa na Wahalifu wakupore wakati zamani wakagundua una Silaha ya Moto ndio wanakulalia Mbali ( Mchakato wa Maombi huanzia Serikali ya Mtaani kwako ambapo Wajumbe wengi ni Watu wa Vijiweni hivyo ukianza tu Mchakato Mtaa Mzima unajua)

Ukinunua na ukakosa Vibali Basi wanakurudishia Fedha yako kwa kukata kiasi kidogo sana cha charge ya usumbufu!

Zile Nzuri bei yake inaanzia 2Million-4.5 Million kutegemea aina. Wataalam ( Mie ni User sio Mtaalam) wanasema kwa Mazingira yetu za Turkey na Italy ni more njema zaid
 
Mkuu Si kila kitu tunaweza share hapa,kutokana na unyeti wake naomba ufike kwa mtu mwenye cheo cha msajili wa silaha pale polisi makao makuu ghorofa ya 5 utapata majibu yote.

poa mkuu
 


Ubarikiwe mkuu
 

Ikiwa sijui kuitumia,nafundishwa?
 
Ikiwa sijui kuitumia,nafundishwa?

Kama Siyo Polisi au Mwajeshi ni lazima utafute mtu wa kukufundisha kutumia ambaye ni mtaalamu wa mambo ya Silaha.

Hapa ni vema umuombe Mwanajeshi na Muelewane utamlipa Sh ngapi?
 
Usihangaike kote huko njoo nikupeleke mpaka mwa congo mpaka AK47 zinapatikana unabadilishana na wale jamaa magunia matatu ya mahindi wanakupa mashine angalizo ukikamatwa na vijana wa Magufuli utaisoma namba kwa kiyunani
 
Ni mara chache sana wenye kumiliki silaha zimewasaidia, sana sana zimewaongezea matatizo, na wengi wamezitumia kujiua na kuuwa wapendwa wao, na wengi zaidi wameporwa, wengi pia wanapenda kutishia tishia tu watu na kupiga hewani hovyo. Aliyeitumia silaha yake kwa ufasaha ni yule bibi wa bagamoyo tu.
 
Alifanyaje mkuu?
 
Kwanza jitathimini mwenyewe unajazba? Kama jibu ni ndio nakushauri usijaribu kununua itakua rahisi kuchukua maamuzi magumu.
 
Ila kumbuka kuwa makini nayo Siku wife ukimzingua.asije akakutwanga nayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…