Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Je, ukimiliki silaha unaruhusiwa kusafiri nayo nje ya mkoa???

Je, mmiliki akihama atapaswa kuwajulisha kule alikohamia kwamba anamiliki silaha????

Naomba kujua masharti baada ya kupewa kibali cha kumiliki silaha.

Ahsanteni wadau
 
Wangeuza kama simu heshima ingekuwepo.
Nchi zote ambazo wanauza silaha kama simu kuna adabu na watawala pia wana adabu mfano tu zambia kwa afrika. Serikali ikileta timbwili mtaani kila mtu ana mguu wa kuku hadi sub machine gun smg.
 
Sifa ya kwanza upimwe akili,2 una Mali isiyo pungua m50 3:ushapata mashambulio mangapi ya kuvamiwa4: je nimlevi kupita kiasi,5: hauna tamaa ya Mali zingine tofauti na ulizo nazo maana usiitumie kujipatia Mali zingine 6: usiwe na wifu wa kimapenzi,nk
 
Tanganyika Arms kule mjini Dar utapata majibu yote. Mashine nzuri ya "kiume" ipo around TZS. 4.5M. Kawaida ukilipia unaiacha pale na kupewa forms za kupeleka serikali za mitaa na kwingineko. Unaw4za kuimiliki ndani ya miezi mitatu au zaidi ya mwaka
 
Katika mambo ya maana ambayo umejitahidi kuuliza humu jf basi hili linaongoza , kujilinda ni haki ya kikatiba , sijui wabongo ni masikini au hawajui tu , kwa maelezo zaidi nipigie simu .
 
Andika barua kwa mkuu wa wilaya yako ukimweleza kusudio/ombi la kutaka kumiliki Silaha ya Moto, kwenye barua hiyo umCC Mwenyekiti Seikali ya mtaa wako na afisa mtendaji wa kata yako, Utaratibu Utajadiliwa na kamati ya ulinzi ya mtaa,Kata na ya wilaya, ukikidhi vigezo unapewa kibali cha kwenda kununua silaha *angalizo* Usianze kwenda kununua kabla ya kibali wanaweza kupokea pesa na wakakupa risiti badala ya silaha na maelekezo kashughulikie KIBALI
 
Hamna namna nyepesi! Namna ni kufuata utaratibu unaanza kujadiliwa kwenye vikao vya serikali za mtaa then unaenda kwa OCD, akipitisha inapelekwa kamati ya ulinzi na usalama wilaya na process nyingine then unapewa kama itakuwa umekidhi.
 
unataka ujiyoe muhanga? kama sababu ndio hiyo sema nikuoneshe wapi utaipata chap
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…