Naomba msaada kujua mwongozo au kanuni rasmi zinazohusu uanzishaji wa makanisa katika maeneo ya makazi hapa Tanzania.
Mimi ni Mkristo na ninaamini kwa dhati katika uhuru wa kuabudu. Hata hivyo, kuna nyakati ambapo ibada na maombi kutoka baadhi ya makanisa yanapita kiwango na kuwa KARAHA, hasa kwa majirani wanaoishi karibu.
Kwa sasa, kuna kanisa jipya la walokole lililofunguliwa karibu kabisa na makazi yangu (eneo la Mbezi Beach – Goig). Kelele zinazotoka kanisani hapo ni nyingi sana, kiasi cha kuvuruga utulivu wa mazingira mchana na usiku. Cha kushangaza, sijawahi kuona taarifa yoyote kwa jamii ya mtaa wala mchakato wa kupata ridhaa ya majirani kabla ya kufunguliwa kwake.