Taratibu za utumishi wa umma zinaruhusu mwalimu kufanya biashara darasani kwa wanafunzi anaowafundisha?

Habari za asubuhi wanajamvi,

Samahani naomba kujuzwa ikiwa kanuni na taratibu za utumishi wa umma zinaruhusu Kwa waalimu kufanya biashara darasani Kwa wanafunzi anaowafundisha?

Kwa ufupi ni kwamba kuna shule moja ipo mkoani Morogoro, wilaya ya Morogoro DC ambapo mwezi January niliwahamishia wanangu wakitokea Mkoani Rukwa tulikokua tukiishi.

Tangu wameanza shule hapo kumekua na mabadiliko kidogo ya kitabia kwa wanangu, wamekua na tabia ya kuomba sana pesa asubuhi wanapotoka kwenda shule kitu ambacho hawakua nacho mwanzo na usipowapa wanakosa amani kabisa.

Sasa katika kufuatilia nini chanzo cha mabadiliko hayo kitabia nikagundua kuwa Kuna mwalimu wa chekechekea anauza maandazi na vitu vingine humo darasani Tena anaweka juu ya meza pale ndo anapendelea kufundisha huku anauza tena kwa kupromote biashara yake.

Sasa hili limenifikirisha nimeona nililete hapa tulijadili Kwa pamoja 🙏🙏🙏
Andamana serikali iongeze maslahi kwa walimu.
Bila hivyo wataendelea kuuziwa tu.
 
Unaonyesha ni jinsi Gani ulivyomkulupukaji , wapi nimeandika kuwa ninakuzidi katika uwezo wa kufikiri?
Au nimeandika kuwa una uwezo mdogo wa kufikiri ? Usiongozwe na mihemko mkuu soma elewa kilichoandikwa kabla hujajibu
Bro usitafute jumba bovu kwangu, wewe wape watoto hela za maandazi asubuhi hivyo tu yaani. Hawa ni watoto wako kumbuka hawana mwingine wa kumtegemea

Yaani unataka kuchunguza sera ili ufanyeje? Ubadili utaratibu au? Hiyo shule hapo Morogoro ina wanafunzi 800+ na wazazi wenye watoto wamekuwa wanaishi vizuri tu na waalimu kwa kuwa support hizo mia mia za maandazi wewe umehamia toka Mpanda huko unajifanya unajua sana habari za sera, kwamba wewe una akili na maarifa sana kuwazidi wazazi wote wenye watoto hapo kwa miaka yote ya hiyo shule.

Acha ubahili na kujifanya mjuaji, NUNULIA WATOTO MAANDAZI FULLSTOP
 
....kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake...
Ila tukubali kwamba tukiendelea na tabia hizi za kuruhusu mambo ya uvunjaji wa kanuni,miongozo,taratibu,maadili na sheria za kazi,tutaendelea kuwa na taifa lenye wafanyakazi wasio na weledi mahala pa kazi kama ambavyo tumekuwa tukilalamika mara kwa mara juu ya wafanyakazi na wayatendayo mahala pa kazi.

Samaki mkunje angali mbichi.

Tukubali moja,ama turuhusu hizi tabia na tusilalamike, au tukataze na kutengeneza uwajibikaji mahala pa kazi na weledi na kufaidi matunda yake.

Tanzania bora ya kesho inaanza kujengwa leo na watoto wanaokuzwa kimaadili.
Kiukweli hata mambo yanafikirisha sana wale tunapaswa kukemea
....kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake...
Ila tukubali kwamba tukiendelea na tabia hizi za kuruhusu mambo ya uvunjaji wa kanuni,miongozo,taratibu,maadili na sheria za kazi,tutaendelea kuwa na taifa lenye wafanyakazi wasio na weledi mahala pa kazi kama ambavyo tumekuwa tukilalamika mara kwa mara juu ya wafanyakazi na wayatendayo mahala pa kazi.

Samaki mkunje angali mbichi.

Tukubali moja,ama turuhusu hizi tabia na tusilalamike, au tukataze na kutengeneza uwajibikaji mahala pa kazi na weledi na kufaidi matunda yake.

Tanzania bora ya kesho inaanza kujengwa leo na watoto wanaokuzwa kimaadili.
Shukrani mkuu , nafikiri Kuna mahali kama taifa tunapaswa tujitathmini
 
Bro usitafute jumba bovu kwangu, wewe wape watoto hela za maandazi asubuhi hivyo tu yaani. Hawa ni watoto wako kumbuka hawana mwingine wa kumtegemea

Yaani unataka kuchunguza sera ili ufanyeje? Ubadili utaratibu au? Hiyo shule hapo Morogoro ina wanafunzi 800+ na wazazi wenye watoto wamekuwa wanaishi vizuri tu na waalimu kwa kuwa support hizo mia mia za maandazi wewe umehamia toka Mpanda huko unajifanya unajua sana habari za sera, kwamba wewe una akili na maarifa sana kuwazidi wazazi wote wenye watoto hapo kwa miaka yote ya hiyo shule.

Acha ubahili na kujifanya mjuaji, NUNULIA WATOTO MAANDAZI FULLSTOP
Umeshinda mkuu🙏🙏🙏
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Samahani naomba kujuzwa ikiwa kanuni na taratibu za utumishi wa umma zinaruhusu Kwa waalimu kufanya biashara darasani Kwa wanafunzi anaowafundisha?

Kwa ufupi ni kwamba kuna shule moja ipo mkoani Morogoro, wilaya ya Morogoro DC ambapo mwezi January niliwahamishia wanangu wakitokea Mkoani Rukwa tulikokua tukiishi.

Tangu wameanza shule hapo kumekua na mabadiliko kidogo ya kitabia kwa wanangu, wamekua na tabia ya kuomba sana pesa asubuhi wanapotoka kwenda shule kitu ambacho hawakua nacho mwanzo na usipowapa wanakosa amani kabisa.

Sasa katika kufuatilia nini chanzo cha mabadiliko hayo kitabia nikagundua kuwa Kuna mwalimu wa chekechekea anauza maandazi na vitu vingine humo darasani Tena anaweka juu ya meza pale ndo anapendelea kufundisha huku anauza tena kwa kupromote biashara yake.

Sasa hili limenifikirisha nimeona nililete hapa tulijadili Kwa pamoja 🙏🙏🙏
Hakuna taratibu wala kanuni hapo,mwalimu anatafuta namna ya kujikim,taratibu na kanuni zitafatwa mwalim akiwezeshwa,we mpe mtoto pesa tena mwalimu ana mpango wa kuweka na juice kabisa.
 
Wafungue wanao akili usilalamike.
Hii nchi mambo ni ngumu sana hata ule utaratibu wa dereva kusimamisha basis njiani kisha anapanda muuza korosho biskuti soda mahindi etc ni wa hovyo ila ndo hivyo tena tunaishi kijamaa.
Kesho wape karanga, ubuyu na visheti wanao wakauze shuleni wapate pesa, au wawe wachuuzi wa bidahaa za mwalimu ili wapate sehemu ya kama malipo na upendeleo na info mbalimbali kutoka kwa ticha husler.
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Samahani naomba kujuzwa ikiwa kanuni na taratibu za utumishi wa umma zinaruhusu Kwa waalimu kufanya biashara darasani Kwa wanafunzi anaowafundisha?

Kwa ufupi ni kwamba kuna shule moja ipo mkoani Morogoro, wilaya ya Morogoro DC ambapo mwezi January niliwahamishia wanangu wakitokea Mkoani Rukwa tulikokua tukiishi.

Tangu wameanza shule hapo kumekua na mabadiliko kidogo ya kitabia kwa wanangu, wamekua na tabia ya kuomba sana pesa asubuhi wanapotoka kwenda shule kitu ambacho hawakua nacho mwanzo na usipowapa wanakosa amani kabisa.

Sasa katika kufuatilia nini chanzo cha mabadiliko hayo kitabia nikagundua kuwa Kuna mwalimu wa chekechekea anauza maandazi na vitu vingine humo darasani Tena anaweka juu ya meza pale ndo anapendelea kufundisha huku anauza tena kwa kupromote biashara yake.

Sasa hili limenifikirisha nimeona nililete hapa tulijadili Kwa pamoja 🙏🙏🙏
Mwalimu hatakiwi kufanya biashara darasani na hata eneo zima la shule.

Hao ndiyo walimu na shule za Kusomesha ujinga.
 
Bro usitafute jumba bovu kwangu, wewe wape watoto hela za maandazi asubuhi hivyo tu yaani. Hawa ni watoto wako kumbuka hawana mwingine wa kumtegemea

Yaani unataka kuchunguza sera ili ufanyeje? Ubadili utaratibu au? Hiyo shule hapo Morogoro ina wanafunzi 800+ na wazazi wenye watoto wamekuwa wanaishi vizuri tu na waalimu kwa kuwa support hizo mia mia za maandazi wewe umehamia toka Mpanda huko unajifanya unajua sana habari za sera, kwamba wewe una akili na maarifa sana kuwazidi wazazi wote wenye watoto hapo kwa miaka yote ya hiyo shule.

Acha ubahili na kujifanya mjuaji, NUNULIA WATOTO MAANDAZI FULLSTOP
😀😀😀😀😀

Bro pole pole,ujue huyu anaweza kufunga safari na kurudi Mpanda kwa hasira.
 
Acheni roho mbaya mwalimu ana familia.

Wape watoto wako Hela wasome wakiwa wameshiba.

Unalalamikia mwalimu kwa shibe ya mwanao. Unresponsible father.

Kwanza sidhani hata mia Tano inazidi kununua vi Maandazi na na maji.

Akili za kimasikini
 
Maisha ni pesa najua na nilazima pesa itumike Ili maisha yaende but my point ni kutaka kuelewa miongozo inasemaje kuhusu Hilo
Muongozo gani unataka,miongozo inaanzia kuvunjwa kwa viongozi wa juu kabisa wa serikali sembuse huku kwa walimu.Hapa bongo hakuna cha muongozo wala nini kinachazingatiwa sasa hv ni kujinusuru kadri unavyoweza..
 
Back
Top Bottom