Tarehe 17 Machi huku wakifanya sherehe za kumbukizi za kifo cha Magufuli, sisi wengine tutafanya sherehe za shukrani kwa uongozi wa Samia Suluhu

Tarehe 17 Machi huku wakifanya sherehe za kumbukizi za kifo cha Magufuli, sisi wengine tutafanya sherehe za shukrani kwa uongozi wa Samia Suluhu

Kama mlifukuzwa makazini kwa vyeti feki kaeni kwa utulivu.

Kama mlikuwa Majizi mkatumbuliwa kwa Wizi tulizeni akili.

Kama mlitumbuliwa kwa Uzembe jifunzeni kuchapa kazi.

Kama mlizoea kupiga madili na kuweka maslahi yenu mbele rudini mkaibe tena maaana shamba la bibi liko wazi sasa Tanesco Umeme mnaugawa kwa michongo, Treni ya Arusha hakuna kitu, SGR mmegoma kuipa kipaumbele, Bwawa la Nyerere ni danadana, mashuleni Michango imerudi, Mtaaani Uhalifu umerudi, Makazini Uzembe umejaaa maradufu, Mahospitalini Unakufa huku unajiona.

Inshort Mmepoteza dirra na Watanzania kuwaongoza kwa kucheka nao mtavuna mabua, wajanja wanamega Nchi Kisela wengine mnabaki kushabikia msivyovijua.
Umenisemea yoote niliyokuwa nayo Moyoni. mmteule
 
uongozi wa Rais Samia ulianza tarehe 19
 
Andiko langu Ili la leo litakuwa na mifano kuntu miwili tu Ili nisiwachoshe wasomaji wa maandiko yangu.

Mwaka 1994,Mimi nikiwa darasa kadhaaa pale shule ya msingi Mbuyuni, nilikuwa na utaratibu wa kwenda kusali ibada ya asubuhi pale kanisa la St Peter pale osterbay.

Ule ulikuwa ni utaratibu wangu Kila siku nilikuwa nikianza na ibada kabla ya kuingia Darasani,(utamaduni huu nipende kushauri ndugu mwana JF kama upo karbu na kanisa na wewe ni mkiristu au upo karbu na msikiti hasikwambie mtu utaratibu huu unasaidia sana kubright the future Yako.

Kuamini Ili hata Mwalimu Juliasi kambarage Nyerere nae tulikuwa tukisali nae Kila siku asubuh kabla ya kuingia Ikulu, Sasa tizama Raisi anaingia Ikulu anaanzia kanisani wewe mvumvi, mkulima, mwizi,tapel na mwalimu au sijui Mwandishi wa habari eti uhanzi na Mungu we unadamka unaingia jf baada ya hapo unakoga maji na kwenda kazini kana kwamba jf ndo imekupa zawadi ya uhai.(nisamehe kwa kukwambia ukweli).

Mwaka huo nilio utaja ilikuwa Ndiyo mara yangu ya kwanza kuona na Mh Raisi wa awamu ya kwanza,je nilimuonaje na Nini kilijili baada ya kumuona?

Ilikuwa hivi,nikiwa kanisani ndani nilikili nilikuwa sijawai kukutana na sura ya mwalimu Nyerere live, siku hiyo Niko kanisani nikiwa na shilingi ishirini mkononi, kwa ajili ya kutoa sadaka, nikam uona Mzee Nyerere akiwa anapita kwenye benchi nililirokuwa nimekalia anaenda mbele kwanza nilishutuka. Maana nilikuwa nimetokea Kijijini, sikuwai kumwona live, hatua ile ilinifanya nitoe shilingi ishirini na kuangalia je ninae mwona kwenye pesa ile ni yeye live?nikagundua ni kweli ni yeye,kimoyo moyo nikajipa tumaini moja yakuwa nangojea ikifika wakati wa kupokea sacrament, Ili niende nikamuone vizuri, na kweli paapu ukafika wakati wa kupokea sacrament kweli nilikuwa mtu wa pili baada ya kuwa Mwalimu amesmama kwenda kupokea,kosa likaja maana alipoenda kupokea kumbe kiutaratibu nilitakiwa nisubiri mpaka atakapo pokea arusi akae, ndo tunaruhusiwa waumini wengine kwenda kupokea.

Mimi sikungojea na Wala sikujua utaratibu ule,nilinyanyuka na kwenda kupokea,nilipishana na Mwalimu wakati yeye anarudi Mimi naenda kupokea,nilipofika Halitare,padri Jovi alikuwa paroko pale,hakunipa mkate kwanza mpaka Mwalimu Nyerere akae, alitamka maneno haya" siku nyingine ukimuona huyo Rais msitaafu inabidi usubiri, mpaka akipokea yeye na arudi akae na wewe ndo usonge mbele kupokea nikasema sawa padri nimekuelewa,"

Nia yangu ya kudhibithisha kuwa Nyerere nilie msikiliza kupitia redio Tanzania,nimemwona live, Nyerere nilie muona kwenye pesa leo ndo namwona live nilifurahi sana na niseme live leo nilifurahi Nina imani hata humu jf Kuna vijana ambao hamkupata fursa ya kuonana Huyu Mzee live. Mmezaliwa akiwa ameisha kufa.

HOJA YANGU!

Utaratibu wa kumwenzi Nyerere imebakia siku moja tu siku ya kumbukizi na siku yenyewe kimsingi Kila uchwao inazidi kuchuja na viongozi mliopo madarakani mnajiskiaje?hivi kweli mambo aliyoyafanya Nyerere kwa miaka 25 niyakusemwa kupitia vyombo vya habari kwa siku moja tu?hotuba zake nzuri alizo zitoa Kwa Nini zisiwe zinatangazwa walau kwa mwezi mmoja au miwili kabla ya siku ya maazimisho? Ili walau watoto wetu wapate kuwasikiliza viongozi hawa na kuwaenzi kwa mazuri waliyoyatenda?hamtaki hawa Hayati wasikike mnaficha Nini?je kwani mnaona aibu watoto wetu wakisiliza hotuba hizo mtakumbuka maana baada ya vifo vyao uwa nyie mliopo madarakani uwa mnakengeuka?hivi nanyi mtafurai mkifa mliyoyatenda na kuyasema tusiayanzi mpotee mazima?

Mfano wa pili; siku kadhaaa zilizopita nikili kwa mara ya kwanza nikiona familia ya Mzee Hayati Moses Nauye wakiazimisha miaka 20 tangu alipo twaliwa, nikili Mimi nilikuwa sehemu ya ile sherehe, ndugu wasomaji ambao hamkuwepo mahala pale niwaombe muingie YUTUBU msikiliza madini. Yaliyotemwa na Mzee yusuph Makamba, Mzee wetu wa msoga, Jakaya Mrisho Kikwete, aise madini yaliyo temwa na Katibu mkuu wa ccm mstaafu, Yani ye Hayati alipewa sifa ambazo zilifanya mpaka mwanae Nape Moses Nauye amwage machozi, (ingawa kutoa machozi kwa nape yeye mara nyingi upenda Julia ila siku ila aliguswa sana na history dhidi ya baba yake, ninakili atakuwa aliumia Kwa Nini hatumwenzi mtu huyo,Makamba Sinior alifika mbali kwa kulalamika kudai kuwa aliumia sana kuona linajengwa soko kubwa kama JOBO(aliyepotea).pale Dodoma linapewa jina ilo badala ya hata kuitwa Moses Nauye,alienda mbali zaidi na kusema,yeye aliumi kuona anapewa jinaa barabara kabla ya Nauye.aliumia sana.

Hatuwaenzi hawa wazee walio tangulia je mbadhani nyie hamtokufa?

Ili limekuja, mpaka kwa Mzee Mkapa,Huyu lijendar kwa kutambua kuwa Kuna ukweli utaweza potoshwa dhidi ya Yale aliyoyasema,na kuyatenda,na kujutia,aliamua kuandika kitabu chake, tunamshukuru sana kwa kuandika kitabu chake,changamoto kwa Tanzania ukitaka kumyima mtu pesa mwambie asome kitabu,maana hata Ili andiko Kuna watu watasema ni refu na hawatalisoma,serikali zetu na watawala wetu wataweza kuruhusu kitabu Cha Mkapa kitumike kwenye mitaala yetu?lengo. Likiwa ni kuenzi aliyoyaamini kuliko kuwafundisha mambo ya ajabu?najua ntasutwa.

The same mistake,kweli aliyoyafanya Mkapa yanafaaa kuoneshwa siku moja kupitia Chombo Cha habari TBC 1 vyombo vingine Huwa sio lazima kuazimisha siku za walio tutawala maana hawalazimishwi kamwe, Kwa Nini tusielekeze vyombo vyote siku hiyo view na agenda ya kuwaenzi viongozi wetu walio tangulia kwa kuweka hotuba zao?tunaogopa Nini kuwaelekeza hao?

Kesho ni kumbukizi, ya Lujendari najua ntashambuliwa sana kisa kumuita hivyo, ila mnyonge anyongwe haki yake mpeni,leo hii habari za kuamia Dodoma,ununuzi wa ndege,kurudishwa kwa nidhamu kazini,kutumbua majipu,kufukuza wafanya kazi hewa,kudhibit ajari za barabarani,ujenzi wa vituo vya afya,ujenzi wa SGR, ujenzi wa Bwawa la Nyerere, elimu Bure,ujenzi wa barabara,madaraja, kukamatwa wahujumu uchumi(ambao ndio mnanitukana), kumtia adabu kabendera,ujenzi wa uwanja wa ndege chato, ujenzi wa hospital ya Kanda ya ziwa, kutoongeza mishahara kwa watumishi wasio wajibika,kumteua mwanamke kuwa Makamu wa Rais na Sasa ni Rais,kuteua mijitu ambayo ni mijizi kama sabaya kwa kushauriwa vibaya na walio fanya vetting, kumteua makonda kwa kudanganywa na kikosi kazi Cha kufanya vetting,kuwakamata walio mtukana Raisi yaani Makamba Junior,and sinior na wengine,kuwakamata wale waliokuwa wakiimbwa kwenye music yaani waaaapi Papa msofe? Piga kelele kwa msofeeeeee wakeeeeee...... Na kuwasweka ndani

Yote haya yanafaaa kuoneshwa kwenye tv Kwa siku ndugu zangu?

Narudia Tena,mfano ujasiri wa Mama Raisi tulie nae Sasa hivi na mambo anayo yafanya lazima tukili ni mazuri wanapokufa viongozi hawa tuwaenzi kwa kufanya ifatavyo;

Viongozi walio hacha vitabu vyao hasa walivyoandika wao vienziwe kwa kupitia wizara ya elimu,mfano tujisahihishe Cha Nyrerere, pamoja na Cha mkapa.my life my p........

Nasema walivyoandika wenyewe, maana najua tukiruhusu hata walivyoandika wengine,wapo watakao andika kwa kujipendekeza na kutoposha ukweli.

Hotuba zao, ni vyema ziwe zinatangazwa kwenye vyombo vya habari, vyote na sio TBC1 nasema vyote,uwezi amini juzi niliweka chanel ya TBC1 mtoto wangu mchanga aliangua kilio kana kwamba nimemfinya kumbe yeye kazoea nyingine sio hiyo ndo mama yake akawa ananiambia hivyo, nilitamani nijue sababu ila najua wasomaji mnanielewa.

Naomba niishie hapo.
 
Mimi nipende tu kuwakumbusha hao wanaosema chama ni chao na nchi ni yao kuwa ujumbe huu ni muhimu wakausave kwenye simu zao.
 
Moja ya Sacrament muhimu kwa Imani yetu sisi wakatoliki ni sacrament ya Kitubio kabla ya kifo.

Ni sacrament ambayo mkatoliki uombewa Toba na mara nyinyi Sara ile uwa akiombewa mtu kupona ni tia maji tia maji hata yule mgonjwa anae fanyiwa au kuombewa Sara Huwa anajua live kuwa Sasa nasepa kwenda kwa muumba.

Hii ni sacrament ambayo kimsingi wakatoliki tulio wengi uwa tunapenda uongozwe na kiongozi wa kiroho aliyepakwa mafuta kwa maana ya PADRI.

Ntaeleza kisa kimoja Cha bibi mmoja aliyekuwa muumini wa kweli kanisa katoliki, hapo ndara tumemzika mwaka jana akiwa na miaka 102,ilipofika wakati wa kufanyiwa au kuombewa Sara ya Toba alitumiwa katekista aje amfanyie Sara ya Toba, bibi akiwa mahututi aliweza kutikisa kichwa kwa inshara ya kutokupenda afanyiwe Sara na mtu yule.

Walilazimisha lakini bibi alionesha kutokuwa na Imani na katekista yule na tulifanya ibada tukamaliza tukasubili Kate roho ahaaaa wapi roho haikutoka tulikaa na bibi mpaka siku ya jumapili akiwa anapumua,siku ya jumapili jirani yetu mmoja akamfata padri wetu na kumwelezea Hali ya bibi padri kwa kuwa alikuwa jumapili alikibali kufika nyumbani kumwona mgonjwa yaani bibi.

Ndugu zangu ninayoyasema au kutandika wewe kapuku waweza nibiashia,huwezi amini alitemfata Padri alikuwa Mzee mwenye miaka zaidi ya 83, tulikuwa nae siku ya ibada ya Kitubio kwa bibi iliyoendeshwa na katekista kumbe aling'amua yakuwa bibi hakurudhishwa na Kitubio kire.

Padri afika kwa bibi!

Padri alipofika kwa bibi, bibi akiwa Bado Yu hoi kitandani aliitambua sauti ile ya padri kwa mbali tulimuona akijitingisha kwa mbali na alifungua macho,alipokutana Hana kwa Hana na padri jambo la kwanza na kwa zaidi ya miezi mitano ya kuumwa kwake,alifungua kinywa na kutamka neno 'TOBA" padri aliitambua na kutuuliza Huyu mgonjwa ametamka neno Toba kwani hamjamwongoza Sara ya Toba?tukijibu tayari,akauliza aliye iongoza tukasema ni katekista.

Hakuongea Tena aliongoza Sara ya kumwombea Toba ndugu zangu ninachokisema hamwezi amini baada ya Sara ya Kitubio,bibi alitokwa na jasho,jembamba, na kwa mbali alifunga macho, na kuiaga Dunia na Tabasamu la ajabu,hii ndo mara ya kwanza kumwona mwanadamu anakufa na Tabasamu kwa mbali la inshara yakuwa naenda mwana mwema mwendo nimeumaliza,odi baba muumba,na muumba anakupokea kwa faraja ujumbe tutende mema.

Nikiwa nafatilia kumbukizi ya kifo Cha Mwamba wa chato kupitia kituo Cha television ya Taifa, TBC1 nimesikia mtangazaji akisoma ujumbe wa mwisho wa Hayati John Pombe Magufuli kwa Taifa la Tanzania.nimeumia sana kabla ya kuweka hapa, naomba niombe kusema kitu kimoja,

Padri wa kanisa katoliki ni mwanadamu kama tulivyo sisi sote,Nina imani Baba askofu Kadinali Pengo na Baba Paroko uenda wakati Hayati anatoa ujumbe huu, wao walikuwa wanaangua "KILIO" kwani ujumbe ulikuwa ni mzito na Nina imani mapaka leo ukiwaingia maskioni mwao Huwa wanalia.
Nitanukuu sehemu ya ujumbe huu sio wote ila ntajitaid kuunukuu!

"Baba Askofu Pengo na Baba Askofu Paroko, nilitamani kuiona Tanzania mpya,Tanzania hisiyo na wara rushwa,natamani Tanzania ipate viongozi Wacha Mungu,nikipenda sana Tanzania ila Sina jinsi nifanyieni Sara ya TOBA wambieni Watanzania wapingane na viongozi wara rushwa" mwisho wakunukuu Kuna maneno mengi mazito nmeyaacha maana NAMI ni mwanadamu ila ni mazito mazito yalitamkaa na Hayati.
Swali Kwa Nini Pengo na Paroko hawakutaka sisi tuujue ujumbe huu?

Katika bandiko Ili haya huu naomba uwe ujumbe!

Kwanza umuhimu wa Sala ya Toba kwa wanadamu.

Umuhimu wa viongozi wapakwa mafuta means Mapdiri wetu(ipo siku nitaeleza Kwa Nini Hayati bibi alimkataa katekista,na hakukata roho siku aliyofanyiwa Sara ya Toba) wanadamu tuishi maisha mema Ili hata tukisema tunamtumikia Mungu jamii ijue kkweli sisi ni. Wasafi

Mafuguli na rushwa je nchi ikoje Sasa?
 
Kwa Jina La Baba Na La Mwana Na La Roho Mtakatifu Amina.

Ee Bwana Ikupendeze upokee Sala na Sadaka za Mwanao John Magufuli. Umjalie Raha Ya Milele na Mwanga wa Kristo Umuangazie. Apumzike Kwa Amani

Roho za waamini Marehemu wapate rehema Kwa Mungu wapumzike Kwa Amani. Amina

Kwa Jina La Baba Na La Mwana Na La Roho Mtakatifu Amina
 
Ujumbe mzito sana!

Tanzania kuwapata viongozi wasiokula rushwa ni vigumu sana hata kule upinzani!

Ila viongozi wanaokumbatia rushwa wamejazana mno hasa upinzani!
Kiongozi bora na pekee ambaye atakumbukwa na visazi vyote ni yule atakayethubutu kuwapatia watanzania KATIBA MPYA - yaani mkataba kati ya watawala na watawaliwa.
 
Upako wa wagonjwa na sacrament ya kitubio ni siri kati ya padri na mgonjwa,ndo maana ata wakati wa kuungama wengine wote hamatakiwi mkae karibu msikie ,umechanganya vitu vitatu tofauti,katekista hawezi na haruhusiwi kutoa sacrament ya kitubio,labda sala ya mwisho tu
 
Subiri spirit yake i incarnate ukweli tutaujua….ila km hayo maneno alisema yeye…ni mtu tu mwenye calcified brain hataelewa alimaanisha nini na nini alichokisema kikawafanya watumishi wa Mungu walie machozi…
 
Continue to rest in peace Mr John Magufuli.

Ila we mtoa mada nae kwa nini usiyatamke hayo maneno yote aliyoyatamka kabla hajafa?
 
Tz asiye penda rushwa ni yule tu ambaye hayupo kwenye nafasi ya kupata rushwa Iyo ila na yeye akipata nafasi hawezi ikataaa

Umaskini ni mbaya sana
 
Huo ni uongo hukuna Sala ila ni kusuuza uso wake2, tumuoombee tu alale mahal pema ppni
 
Upako wa wagonjwa na sacrament ya kitubio ni siri kati ya padri na mgonjwa,ndo maana ata wakati wa kuungama wengine wote hamatakiwi mkae karibu msikie ,umechanganya vitu vitatu tofauti,katekista hawezi na haruhusiwi kutoa sacrament ya kitubio,labda sala ya mwisho tu
Kuna watu wana ongea wakati hata hiyo sacrament ya kitubio hajui inafanyikaje.

Umechambua vizuri sana Joe razinger
 
Kwa Jina La Baba Na La Mwana Na La Roho Mtakatifu Amina.

Ee Bwana Ikupendeze upokee Sala na Sadaka za Mwanao John Magufuli. Umjalie Raha Ya Milele na Mwanga wa Kristo Umuangazie. Apumzike Kwa Amani

Roho za waamini Marehemu wapate rehema Kwa Mungu wapumzike Kwa Amani. Amina

Kwa Jina La Baba Na La Mwana Na La Roho Mtakatifu Amina
Safiiii sana.
 

Kuna watu wana ongea wakati hata hiyo sacrament ya kitubio hajui inafanyikaje.

Umechambua vizuri sana Joe razinger
Ndio maana inakua ngumu kwake kuelewa bibi yake alichokua anataka ni kupata sacrament ya mwisho ,ambayo katekista hawezi kuitoa,ana kwambia katekista alimpa kitubio bibi yao kitubio wakiwa na wao pembeni,serious?
 
Back
Top Bottom