Andiko langu Ili la leo litakuwa na mifano kuntu miwili tu Ili nisiwachoshe wasomaji wa maandiko yangu.
Mwaka 1994,Mimi nikiwa darasa kadhaaa pale shule ya msingi Mbuyuni, nilikuwa na utaratibu wa kwenda kusali ibada ya asubuhi pale kanisa la St Peter pale osterbay.
Ule ulikuwa ni utaratibu wangu Kila siku nilikuwa nikianza na ibada kabla ya kuingia Darasani,(utamaduni huu nipende kushauri ndugu mwana JF kama upo karbu na kanisa na wewe ni mkiristu au upo karbu na msikiti hasikwambie mtu utaratibu huu unasaidia sana kubright the future Yako.
Kuamini Ili hata Mwalimu Juliasi kambarage Nyerere nae tulikuwa tukisali nae Kila siku asubuh kabla ya kuingia Ikulu, Sasa tizama Raisi anaingia Ikulu anaanzia kanisani wewe mvumvi, mkulima, mwizi,tapel na mwalimu au sijui Mwandishi wa habari eti uhanzi na Mungu we unadamka unaingia jf baada ya hapo unakoga maji na kwenda kazini kana kwamba jf ndo imekupa zawadi ya uhai.(nisamehe kwa kukwambia ukweli).
Mwaka huo nilio utaja ilikuwa Ndiyo mara yangu ya kwanza kuona na Mh Raisi wa awamu ya kwanza,je nilimuonaje na Nini kilijili baada ya kumuona?
Ilikuwa hivi,nikiwa kanisani ndani nilikili nilikuwa sijawai kukutana na sura ya mwalimu Nyerere live, siku hiyo Niko kanisani nikiwa na shilingi ishirini mkononi, kwa ajili ya kutoa sadaka, nikam uona Mzee Nyerere akiwa anapita kwenye benchi nililirokuwa nimekalia anaenda mbele kwanza nilishutuka. Maana nilikuwa nimetokea Kijijini, sikuwai kumwona live, hatua ile ilinifanya nitoe shilingi ishirini na kuangalia je ninae mwona kwenye pesa ile ni yeye live?nikagundua ni kweli ni yeye,kimoyo moyo nikajipa tumaini moja yakuwa nangojea ikifika wakati wa kupokea sacrament, Ili niende nikamuone vizuri, na kweli paapu ukafika wakati wa kupokea sacrament kweli nilikuwa mtu wa pili baada ya kuwa Mwalimu amesmama kwenda kupokea,kosa likaja maana alipoenda kupokea kumbe kiutaratibu nilitakiwa nisubiri mpaka atakapo pokea arusi akae, ndo tunaruhusiwa waumini wengine kwenda kupokea.
Mimi sikungojea na Wala sikujua utaratibu ule,nilinyanyuka na kwenda kupokea,nilipishana na Mwalimu wakati yeye anarudi Mimi naenda kupokea,nilipofika Halitare,padri Jovi alikuwa paroko pale,hakunipa mkate kwanza mpaka Mwalimu Nyerere akae, alitamka maneno haya" siku nyingine ukimuona huyo Rais msitaafu inabidi usubiri, mpaka akipokea yeye na arudi akae na wewe ndo usonge mbele kupokea nikasema sawa padri nimekuelewa,"
Nia yangu ya kudhibithisha kuwa Nyerere nilie msikiliza kupitia redio Tanzania,nimemwona live, Nyerere nilie muona kwenye pesa leo ndo namwona live nilifurahi sana na niseme live leo nilifurahi Nina imani hata humu jf Kuna vijana ambao hamkupata fursa ya kuonana Huyu Mzee live. Mmezaliwa akiwa ameisha kufa.
HOJA YANGU!
Utaratibu wa kumwenzi Nyerere imebakia siku moja tu siku ya kumbukizi na siku yenyewe kimsingi Kila uchwao inazidi kuchuja na viongozi mliopo madarakani mnajiskiaje?hivi kweli mambo aliyoyafanya Nyerere kwa miaka 25 niyakusemwa kupitia vyombo vya habari kwa siku moja tu?hotuba zake nzuri alizo zitoa Kwa Nini zisiwe zinatangazwa walau kwa mwezi mmoja au miwili kabla ya siku ya maazimisho? Ili walau watoto wetu wapate kuwasikiliza viongozi hawa na kuwaenzi kwa mazuri waliyoyatenda?hamtaki hawa Hayati wasikike mnaficha Nini?je kwani mnaona aibu watoto wetu wakisiliza hotuba hizo mtakumbuka maana baada ya vifo vyao uwa nyie mliopo madarakani uwa mnakengeuka?hivi nanyi mtafurai mkifa mliyoyatenda na kuyasema tusiayanzi mpotee mazima?
Mfano wa pili; siku kadhaaa zilizopita nikili kwa mara ya kwanza nikiona familia ya Mzee Hayati Moses Nauye wakiazimisha miaka 20 tangu alipo twaliwa, nikili Mimi nilikuwa sehemu ya ile sherehe, ndugu wasomaji ambao hamkuwepo mahala pale niwaombe muingie YUTUBU msikiliza madini. Yaliyotemwa na Mzee yusuph Makamba, Mzee wetu wa msoga, Jakaya Mrisho Kikwete, aise madini yaliyo temwa na Katibu mkuu wa ccm mstaafu, Yani ye Hayati alipewa sifa ambazo zilifanya mpaka mwanae Nape Moses Nauye amwage machozi, (ingawa kutoa machozi kwa nape yeye mara nyingi upenda Julia ila siku ila aliguswa sana na history dhidi ya baba yake, ninakili atakuwa aliumia Kwa Nini hatumwenzi mtu huyo,Makamba Sinior alifika mbali kwa kulalamika kudai kuwa aliumia sana kuona linajengwa soko kubwa kama JOBO(aliyepotea).pale Dodoma linapewa jina ilo badala ya hata kuitwa Moses Nauye,alienda mbali zaidi na kusema,yeye aliumi kuona anapewa jinaa barabara kabla ya Nauye.aliumia sana.
Hatuwaenzi hawa wazee walio tangulia je mbadhani nyie hamtokufa?
Ili limekuja, mpaka kwa Mzee Mkapa,Huyu lijendar kwa kutambua kuwa Kuna ukweli utaweza potoshwa dhidi ya Yale aliyoyasema,na kuyatenda,na kujutia,aliamua kuandika kitabu chake, tunamshukuru sana kwa kuandika kitabu chake,changamoto kwa Tanzania ukitaka kumyima mtu pesa mwambie asome kitabu,maana hata Ili andiko Kuna watu watasema ni refu na hawatalisoma,serikali zetu na watawala wetu wataweza kuruhusu kitabu Cha Mkapa kitumike kwenye mitaala yetu?lengo. Likiwa ni kuenzi aliyoyaamini kuliko kuwafundisha mambo ya ajabu?najua ntasutwa.
The same mistake,kweli aliyoyafanya Mkapa yanafaaa kuoneshwa siku moja kupitia Chombo Cha habari TBC 1 vyombo vingine Huwa sio lazima kuazimisha siku za walio tutawala maana hawalazimishwi kamwe, Kwa Nini tusielekeze vyombo vyote siku hiyo view na agenda ya kuwaenzi viongozi wetu walio tangulia kwa kuweka hotuba zao?tunaogopa Nini kuwaelekeza hao?
Kesho ni kumbukizi, ya Lujendari najua ntashambuliwa sana kisa kumuita hivyo, ila mnyonge anyongwe haki yake mpeni,leo hii habari za kuamia Dodoma,ununuzi wa ndege,kurudishwa kwa nidhamu kazini,kutumbua majipu,kufukuza wafanya kazi hewa,kudhibit ajari za barabarani,ujenzi wa vituo vya afya,ujenzi wa SGR, ujenzi wa Bwawa la Nyerere, elimu Bure,ujenzi wa barabara,madaraja, kukamatwa wahujumu uchumi(ambao ndio mnanitukana), kumtia adabu kabendera,ujenzi wa uwanja wa ndege chato, ujenzi wa hospital ya Kanda ya ziwa, kutoongeza mishahara kwa watumishi wasio wajibika,kumteua mwanamke kuwa Makamu wa Rais na Sasa ni Rais,kuteua mijitu ambayo ni mijizi kama sabaya kwa kushauriwa vibaya na walio fanya vetting, kumteua makonda kwa kudanganywa na kikosi kazi Cha kufanya vetting,kuwakamata walio mtukana Raisi yaani Makamba Junior,and sinior na wengine,kuwakamata wale waliokuwa wakiimbwa kwenye music yaani waaaapi Papa msofe? Piga kelele kwa msofeeeeee wakeeeeee...... Na kuwasweka ndani
Yote haya yanafaaa kuoneshwa kwenye tv Kwa siku ndugu zangu?
Narudia Tena,mfano ujasiri wa Mama Raisi tulie nae Sasa hivi na mambo anayo yafanya lazima tukili ni mazuri wanapokufa viongozi hawa tuwaenzi kwa kufanya ifatavyo;
Viongozi walio hacha vitabu vyao hasa walivyoandika wao vienziwe kwa kupitia wizara ya elimu,mfano tujisahihishe Cha Nyrerere, pamoja na Cha mkapa.my life my p........
Nasema walivyoandika wenyewe, maana najua tukiruhusu hata walivyoandika wengine,wapo watakao andika kwa kujipendekeza na kutoposha ukweli.
Hotuba zao, ni vyema ziwe zinatangazwa kwenye vyombo vya habari, vyote na sio TBC1 nasema vyote,uwezi amini juzi niliweka chanel ya TBC1 mtoto wangu mchanga aliangua kilio kana kwamba nimemfinya kumbe yeye kazoea nyingine sio hiyo ndo mama yake akawa ananiambia hivyo, nilitamani nijue sababu ila najua wasomaji mnanielewa.
Naomba niishie hapo.