Tarehe 17 March 2021, Makamu wa Rais akitangaza kifo cha aliyekuwa rais Ndugu Hayati Magufuli ulikuwa wapi?

Tarehe 17 March 2021, Makamu wa Rais akitangaza kifo cha aliyekuwa rais Ndugu Hayati Magufuli ulikuwa wapi?

Nilikua Njoss.
Mda huo tumetoka prep...
Nakuta story story. Nikatoka kwenda jidah kuangalia kwa jamaa ambao walikua na simu..
Ndio nakuta Mama anatangaza rasmi
 
Niliamshwa toka usingizini na simu ya rafiki kuniambia niangalie TV.

Nilikuwa mmoja ya wanaomkandia na kumpinga sana lakini kibinadamu huwezi furahia mauti ya mwenzio ukijua wewe mwenyewe unaelekea huko huko. Naamini nilihuzunika.

Kwa sasa kwa baadhi ya mambo yanavyokwenda huwa najutia baadhi ya vitu nilivyokuwa navipinga na kumkandia.

Yote kwa yote sisi wote ni wa Mola na hakika kwake tutarejea. Kila nafsi itaonja mauti. Mungu amlaze mahala pema na atupe mwisho mwema sisi tuliobaki.
 
Nakumbuka watubwalifurahi hatariii..
Na kufurahi ni kwa sababu tulijua kutakua na kughailishwa kwa vipindi maana sio kwa pindi lile....
 
Aiseee hyo siku nililia sanaa nilikua nipo kwny nyumba ya kupanga wapangaji wote tulitoka nje tukaanza kulia daahh wamama full vilio hadi balaa aiseee[emoji119]
Mwingine alilia hadi akashikwa na period
 
Nakumbuka nilikuwa lodge moja tabata nachepuka. Nishamaliza round ya pili kutupia jicho TV namuona Hangaya anaongea na maandishi yakipita chini kuwa mwamba kavuta. Ilibidi niongeze sauti ili nisikie.

Baada ya hapo nikarudi zangu juu ya kifua cha Salma wangu kuendeleza libeneke. Nilikuja kusikitika vizuri asubuhi baada ya kumaliza uzinzi wangu.
 
Mi nilikua nimelala coz kigogo twitter alishatuhakikishia ilibaki kutangaza TU!!

Hata ilipotangazwa usiku nilikua nimelala nikashangaa napigiwa simu sikutoka nje kabisa coz nilihisi nchi haitokua salama kabisa!!

Nikawa mkimya na nikajitenga na baadhi ya maeneo hasa yenye mkusanyiko!!

Kifo Cha jpm wachache tulikijua karibu mwaka mmoja kabla lakini hatukujua ni lini itakua hasa Uzi was tumia akili wa "Rais ambae hajawahi kugombea ilitokea marekani itatokea na huku" nilianza kufuatilia comment na duru za maandishi ya code na kuanza kupata picha!!Kuna id Moja inaitwa nguseroh aiseh!!ilisema kabisa mwakani tuna Rais mwanamke nilimshangaa Sana!

Hata Sasa mambo sio.salama.sana kama tunavodhani !

Tuendelee kuwa wazalendo wakimya Sana!!

Mungu ibariki Tanzania!
 
Binafsi taarifa za msiba wa rais nilizipata nikiwa njiani, nimepanda basi la Majinja likilokuwa linàfanya safari za wizi za usiku, likitoka Dar kuelekea Mbeya. Safari yangu ilikuwa ikiishia Mafinga mkoani Iringa.

Nilikuwa nime tune Radio 1, ndipo wakakata matangazo na tukaunganishwa na TBC.

Makamu wa Rais alipotangaza tukio lile, basi likageuka kama la kusafirisha msiba, vilio vikatawala, hadi nafika Mafinga, mji wote una msiba.

Je mwenzangu msiba ulikukutia wapi? Hali ilikuwaje?
Ilikuwa ni form 6, tunakaza msuli kukitafuta chuo
Mm nimelala zangu bwenini, jamaa kutoka bweni jingine wakaidaka taarifa Kwa kutumia simu. Wadau hawakuamini, ikabidi waende staff (mle Kuna tv, inayotumiwa na walinzi wa shule)
Kesho yake, Head Master anakuja kutangaza..Kila mtu ana taarifa [emoji23][emoji23]
Kilichobaki ni kujazana dining hall kuangalia TBC tu
Shule ilikuwa kama km 100 kutoka chato, wadau siku ya mazishi walitimba
 
Mi nilikua nimelala coz kigogo twitter alishatuhakikishia ilibaki kutangaza TU!!

Hata ilipotangazwa usiku nilikua nimelala nikashangaa napigiwa simu sikutoka nje kabisa coz nilihisi nchi haitokua salama kabisa!!

Nikawa mkimya na nikajitenga na baadhi ya maeneo hasa yenye mkusanyiko!!

Kifo Cha jpm wachache tulikijua karibu mwaka mmoja kabla lakini hatukujua ni lini itakua hasa Uzi was tumia akili wa "Rais ambae hajawahi kugombea ilitokea marekani itatokea na huku" nilianza kufuatilia comment na duru za maandishi ya code na kuanza kupata picha!!Kuna id Moja inaitwa nguseroh aiseh!!ilisema kabisa mwakani tuna Rais mwanamke nilimshangaa Sana!

Hata Sasa mambo sio.salama.sana kama tunavodhani !

Tuendelee kuwa wazalendo wakimya Sana!!

Mungu ibariki Tanzania!
Wazee wa VPN na followers wa handle ya @Kigogo2016
 
Nimesahau ilikua radio ipi inatangaza hio taarifa yule mtangazaji akashindwa kuendelea kutangaza msiba akaanza kulia radio ipo hewani ikabidi wakatishe na kuweka nyimbo.

Lakini ipo wazi wengi walishafahamu jamaa alikua amekata moto mapema tu sema ile kutoamini na pia walisubiri uthibitisho.

RIP JPM.
 
Nilikuwa nimelala muda huo, ghafla napigiwa simu kupewa taarifa ya msiba wa Mwamba.

Nilishtuka sana Kwa habari hizo japo nilishasoma soma Kwa Kigogo14 Siku kadhaa nyuma kwamba Mzee alikuwa kwenye battle ya kupigania Uhai wake pamoja na hadithi za PM kusema Mwamba alikuwa Kazini anapiga kazi 🙌

All in all Kifo hakizoeleki

Tuendelee kumwombea Pumziko jema

Mbele yetu, nyuma yake
 
Back
Top Bottom