Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
4,072
Reaction score
12,119
Kwa shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama directorate K. Hii idara ilikuwa na kazi maalumu ya kufanya bugging , kile kitendo Cha kupandikiza vinasa sauti na video camera kwa Siri kwenye ofisi za walengwa maalumu waliokusudiwa , kusikiliza mawasiliano Yao ya simu au pia wakati mwingine kwenye makazi Yao binafsi.

Ilichukua nusu dakika kufungu vitasa viwili vya mlango wa mbele wa chumba namba 220 kwenye ghorofa ya nane katika mtaa wa Leninsky prospekt. Hili lilikuwa ni jumba la ghorofa lililokuwa linakaliwa na maofisa wa KGB pamoja na familia zao.

Kwa Siri sana wanaume waawili waliokuwa wamevalia overall pamoja na gloves kwa haraka haraka wangedhaniwa kuwa ni mafundi tu wa kawaida kwa ajili ya kufanya matengenezo madogo madogo katika jumba hilo, lakini uhalisia haukuwa hivyo. Baada ya kufungua vitasa vya chumba hicho kwa ustadi na kuingia ndani wakaaanza kufanya kilichowaleta. Wanaume hao wawili wakaaanza kuweka camera pamoja na vinasa sauti kwa siri kwenye sehemu sehemu mbali mbali chumbani maeneo ambayo sio rahisi kushtukiwa. Vinasa sauti viliwekwa ukutani kwenye maiki za simu ya mezani ,pamoja na kwenye Kona za kitanda, jikoni, maliwatoni n.k.

Pia kamera ndogo za Siri ziliwekwa kwenye taa za kila Kona ya chumba hicho ,baada ya hapo wakavaa mask usoni na kuanza kunyunyiza vumbi lenye mionzi kwenye nguo na viatu vilivyokuwa kabatini katika Hali ambayo isingeweza kushtukiwa na mlengwa wao. Hili vumbi lingewasaidia ku-track movements za huyo mlengwa wao popote aendapo kwa kutumia kifaa kilichojulikana kama Geiger counte. Baada ya kumaliza kilichowaleta wakaurudishia mlango na kuufunga kama walivyoukuta na wakatokomea.

Masaa machache baadaye, afisa wa ngazi za juu wa KGB alishuka kwenye uwanja wa ndege wa Moscow na shirika la ndege la Aeroflot akitokea London. Kanali Oleg antonyevich Gordievsky alikuwa katika kilele cha mafaniko ya kazi Yake katika idara ya KGB. Mpaka kufika kuwa afisa wa ngazi za juu kwenye shirika Hilo alipitia vyeo mbalimbali, amefanya kazi kama balozi kwenye nchi za Scandinavia, Uingereza pamoja na hapo Moscow.

Akiwa na miaka 46 aliteuliwa kuwa mwakilishi wa KGB kwenye ubalozi wa USSR hapo London. Kwa kuwa alikuwa jasusi mbobevu alipanda vyeo kwa haraka ndani ya idara kiasi kwamba akawa na uwezo wa kujua Siri nyingi za kijasusi (Disclassfied material) pamoja na mtandao wa kijasusi kwenye mataifa mbalimbali ikiwemo mataifa ya magharibi.

Mwenye muonekano wa mwili wa mazoezi, akiwa hana hofu wala wasiwasi huku akitabasamu alikatiza katikati ya umati wa watu hapo uwanja wa ndege kwa ajili ya kutafuta teksi imuondoe hapo impeleke anapoishi.

Bwana Oleg afisa wa kijasusi mtiifu wa shirika la KGB aliyependwa na mabosi wake kama asset muhimu waliokuwa nayo kipindi hicho, pia alikuwa ni JASUSI MTIIFU WA UINGEREZA. Kwa kifupi alikuwa ni double agent.

Akiwa afisa wa KGB tayari alikuwa ni mwajiriwa rasmi wa shirika la kijasusi la uingereza la MI6 kwa miaka takribani 12 .na alipewa jina jina la uficho (codename) la NOCTON.

Na baadaye ikaja semekana alikuwa ndiye JASUSI wa thamani sana enzi zile za vita baridi. Taarifa za Siri alizokuwa anazivujisha kutoka KGB na mipango ya Siri ya USSR zilibadilisha kabisa mkondo wa vita baridi kwa wakati ule. Bwana Oleg aliweza kutoboa Siri ikiwemo mikakati ya nyuklia za USSR. Mtandao wa majasusi uliokuwa kwenye nchi za magharibi,pamoja na sera za nje za urusi kwa wakati huo kwa wakubwa wa MI6.

Taarifa alizokuwa anazivujisha bwana Oleg ziliwafanya MI6 na CIA ku-share kwa pamoja baadhi ya taarifa, lakini ajabu ni kwamba DG na top officials wa MI6 hawakutaka kutoa identity ya Oleg kwa Margaret thatcher Wala Ronald Reagan waliemwajiri ndani ya Kremlin kwa maaana ya USSR kwa kuwapa sensitive Disclassfied informations. Na kulikuwa na sababu maalumu ya kufanya hivyo.
Pia mkewe bwana oleg hakuwahi kujua mumewe ni spy wa uingereza.

Lakini imekuwaje amekuja ghafla Moscow kwa kuitwa na wakubwa zake? . yaani ni kwa mfano balozi polepole kateuliwa balozi Tz Cuba, lakini ghafla hajamaliza hata miezi mitatu anaitwa nyumbani ghafla ,lazima hata kama ni wewe utajiuliza tu.

Lakini wanasema JASUSI ni jasusi tu . bwana Oleg aliweza kunusa hatari iliyokuwa mbele Yake ,akiwa anakatiza katikati ya watu hapo uwanja wa ndege baada ya kutua ndani ya nafsi yake alihisi upweke uliochanganyika na mashaka . Baada ya kukaguliwa nyaraka zake na hati ya kusafiria na wale maafisa wa passport uwanjani hapo alikabidhiwa akaagwa akaondoka.

Kikawaida kwa wakati huo afisa yoyote hususani mwakilishi akitokea nje ya nchi lazima kunakuwa na courtesy ya maafisa wenzake kuja kumpokea mwenzao airport lakini haikuwa hivyo. Akiwa anaangaza huku na kule asione dalili yoyote ya mapokezi alinotice jambo lisilo la kawaida, kulikuwa na wanaume na wanawake wamesimama hapa na pale uwanjani hapo pasipo jambo la muhimu waliokuwa walikilifanya zaidi ya kushangaa huku na huko.

Lakini bwana huyu akiwa ndani ya teksi alijiambia ikiwa KGB wanajua ukweli kumhusu yeye muda huo angekuwa tayari amewekwa chini ya ulinzi muda huo punde alipokanyaga ardhi ya Russia,aburuzwe Hadi kwenye cell za KGB ahojiwe,ateswe mwisho wa siku auliwe kwa kupigwa risasi ya kichwani .

Mpaka anaingia kwenye teksi Hadi kufika yalipo makazi yake mtaa wa Leninsky prospekt hakuwa anafuatiliwa kwa namna yoyote ile.alikwea lift Hadi ghorofa ya nane kwenye jumba Hilo kitasa Cha kwanza Cha mlango wake kilifunguka na Cha pili vilevile lakini kitasa Cha tatu Cha mlango kilikuwa locked bwana Oleg hakuwahi tumia kitasa Cha tatu kwa kuwa hakuwa na funguo zake, lakini ajabu ni kwamba alikuta kitasa kimefungwa na hapo hapo akahisi Kuna watu waliingia na kutoka wakajisahau wakafunga Hadi kitasa Cha tatu. Alikuwa sahihi . Alikuwa anatiliwa wasiwasi. The spy was being spied upon by his fellow spies.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…