Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na kuliwa kicwa ni kitu Cha kawaida!Ulimwegu wa ujasusi ni full kuwindana,yaana unakuwa kama swala katikati ya kundi la simba.
PESA inafanya mapinduzi katika huu ulimwengu.
Halo ama kweli duniani hamna Siri na ni mwendo wa kuviziana tu Kwa kwenda mbele plus uyuda iskariote Kila sehemu09
Ni kwamba mwaka 1971 serikali ya uingereza wakati huo ikiwa chini ya pm Edward heath iliamua kutimua maafisa wa ki Soviet 105 waliosadikiwa kuwa ni makachero wa KGB . Hii operation ilijulikana kama Operation Foot. Kama tu shirika la ujasusi la Denmark la pET lilivyokuwa likifanya kupeleleza maafisa wa Soviet ,hivyo hivyo na uingereza walifanya . Uingereza ilikuwa inawafuatilia waandishi, wanadiplomasia,na wawakilishi wa urusi na kuweza kuwachambua wapi walikuwa na element za ujasusi na wapi hawana . Hivyo ikasadikika raia 105 wa urusi ni manjagu ,wakatimuliwa. Na mpaka uingereza wakaweza kugundua idadi kubwa hivyo ya majasusi,waliweza kumtumia jasusi wa urusi aliyekuwa mwakilishi wa ki Soviet nchini uingereza kwenye maswala ya viwanda vya nguo. Aliitwa Oleg lyalin(hana uhusiano na Oleg Gordievsky).Huyu alikuwa jasusi mbobevu na mtiifu wa KGB aliyekuwa anafanya kazi kwenye idara ndani ya kitengo Cha KGB kiitwacho thirteenth department . Hii ni idara special kwa ajili ya torture, assassination na kidnapping ndani ya KGB. Siri alizotoa ni mipango mikakati ya urusi kufanya mauaji ya watu maarufu uingereza. Vilevile aliwatonya kwamba urusi ilipanga kuleta mafuriko kwenye njia za reli ya chini ya ardhi huko uingereza hususan London . Hivyo M15 baada ya kupewa hizi infos wakaamua kuchukua jukumu la kutimulia mbali mrusi yoyote aliyekuwa na element za ujasusi nchini uingereza.
NB:M15 Ina deal na ujasusi wa ndani na M16 Ni ujasusi wa nje .. refer FBI VS CIA.
Hili tukio liliwavua sana nguo Urusi kiasi kwamba hata idara ya FCD ambayo bwana Oleg Gordievsky ilipata pigo kwa maana baadhi ya majasusi waliotimuliwa huko uingereza walikuwa chini ya hii idara.Hii ilikuwa pigo sana kwa urusi maana assets zao zimekuwa compromised. Na vilevile baadhi ya taarifa za Siri za kiintelijensia zilipotea na kuwapa hasara . Hapo baadhi ya vigogo wa idara mbalimbali ndani ya kitengo wakaanza kutumbuliwa . Kwa mfano idara ya FCD aliyopo Bwana Oleg kigogo wake alitumbuliwa na akawa replaced na Bwana Dimitri Yakushin.
Ukiwa na boss mpya Kuna kuwa na changamoto zake sana hususan mwenye misimamo mikali na damu haziendani . Ni wakati bwana Oleg alipotishiwa kufukuzwa kazi kwa hasira za mkuu wake kutokana na kutimuliwa kwa majasusi huko uingereza.
Kwa miaka mingi Sasa kaka yake Oleg,bwana Vasili alikuwa ni mpiga vyombo mzuri sana. Akiwa anafanya kazi za kijasusi. Kama illegal huko south-east Asia alipata homa ya ini na kushauriwa aachane na gambe na madaktari . Lakini mwamba aliendelea Hadi umauti ulipomkuta akiwa na miaka 39. Alipewa heshima ya kijeshi na KGB.zikapigwa automatic machine gun Kama salute huku geneza lake likiwa limefunikwa na bendera ya Soviet likishushwa taratibu kwenye crematorium. Oleg alitazama geneza la bro wake huku akiwaza ni jinsi gani alifichwa mambo mengi yeye na alitamani kuyajua. Oleg hakuwahi jua kaka yake alikuwa anafanya Nini nchini Czechoslovakia mpaka umauti unamkuta. Hakuwahi yaelewa maisha ya kaka na Wala hakuwahi kumuuliza. Kiuhalisia walikuwa karibu kipindi Cha uhai wake Kama mtu na nduguye lakini mioyoni walikuwa wametengwa na ulimwengu mpana wa Siri nyingi .
Mama mtu na dada mtu wakiwa wameinamisha nyuso zao wakiomboleza ,yeye mzee alikuwa akitoa salute za mwisho kwa mwanaye wa kwanza kama jembe lililotumikia KGB kwa uzalendo wa Hali ya juu akiwa na ile Sense of proud.
kwenye idara nyeti hizi za usalama umbea ni kitu Cha kawaida sana . Bwana Oleg alipaswa kurudi Tena nchini Denmark kikazi . Hizi taarifa walikuwa Nazo Hadi PET/M16 .
kama una mke lazima pawe na mfarakano.Ni kazi ngumu sana hii
Ni kweli yanikama una mke lazima pawe na mfarakano.