Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

09


Ni kwamba mwaka 1971 serikali ya uingereza wakati huo ikiwa chini ya pm Edward heath iliamua kutimua maafisa wa ki Soviet 105 waliosadikiwa kuwa ni makachero wa KGB . Hii operation ilijulikana kama Operation Foot. Kama tu shirika la ujasusi la Denmark la pET lilivyokuwa likifanya kupeleleza maafisa wa Soviet ,hivyo hivyo na uingereza walifanya . Uingereza ilikuwa inawafuatilia waandishi, wanadiplomasia,na wawakilishi wa urusi na kuweza kuwachambua wapi walikuwa na element za ujasusi na wapi hawana . Hivyo ikasadikika raia 105 wa urusi ni manjagu ,wakatimuliwa. Na mpaka uingereza wakaweza kugundua idadi kubwa hivyo ya majasusi,waliweza kumtumia jasusi wa urusi aliyekuwa mwakilishi wa ki Soviet nchini uingereza kwenye maswala ya viwanda vya nguo. Aliitwa Oleg lyalin(hana uhusiano na Oleg Gordievsky).Huyu alikuwa jasusi mbobevu na mtiifu wa KGB aliyekuwa anafanya kazi kwenye idara ndani ya kitengo Cha KGB kiitwacho thirteenth department . Hii ni idara special kwa ajili ya torture, assassination na kidnapping ndani ya KGB. Siri alizotoa ni mipango mikakati ya urusi kufanya mauaji ya watu maarufu uingereza. Vilevile aliwatonya kwamba urusi ilipanga kuleta mafuriko kwenye njia za reli ya chini ya ardhi huko uingereza hususan London . Hivyo M15 baada ya kupewa hizi infos wakaamua kuchukua jukumu la kutimulia mbali mrusi yoyote aliyekuwa na element za ujasusi nchini uingereza.

NB:M15 Ina deal na ujasusi wa ndani na M16 Ni ujasusi wa nje .. refer FBI VS CIA.

Hili tukio liliwavua sana nguo Urusi kiasi kwamba hata idara ya FCD ambayo bwana Oleg Gordievsky ilipata pigo kwa maana baadhi ya majasusi waliotimuliwa huko uingereza walikuwa chini ya hii idara.Hii ilikuwa pigo sana kwa urusi maana assets zao zimekuwa compromised. Na vilevile baadhi ya taarifa za Siri za kiintelijensia zilipotea na kuwapa hasara . Hapo baadhi ya vigogo wa idara mbalimbali ndani ya kitengo wakaanza kutumbuliwa . Kwa mfano idara ya FCD aliyopo Bwana Oleg kigogo wake alitumbuliwa na akawa replaced na Bwana Dimitri Yakushin.
Ukiwa na boss mpya Kuna kuwa na changamoto zake sana hususan mwenye misimamo mikali na damu haziendani . Ni wakati bwana Oleg alipotishiwa kufukuzwa kazi kwa hasira za mkuu wake kutokana na kutimuliwa kwa majasusi huko uingereza.

Kwa miaka mingi Sasa kaka yake Oleg,bwana Vasili alikuwa ni mpiga vyombo mzuri sana. Akiwa anafanya kazi za kijasusi. Kama illegal huko south-east Asia alipata homa ya ini na kushauriwa aachane na gambe na madaktari . Lakini mwamba aliendelea Hadi umauti ulipomkuta akiwa na miaka 39. Alipewa heshima ya kijeshi na KGB.zikapigwa automatic machine gun Kama salute huku geneza lake likiwa limefunikwa na bendera ya Soviet likishushwa taratibu kwenye crematorium. Oleg alitazama geneza la bro wake huku akiwaza ni jinsi gani alifichwa mambo mengi yeye na alitamani kuyajua. Oleg hakuwahi jua kaka yake alikuwa anafanya Nini nchini Czechoslovakia mpaka umauti unamkuta. Hakuwahi yaelewa maisha ya kaka na Wala hakuwahi kumuuliza. Kiuhalisia walikuwa karibu kipindi Cha uhai wake Kama mtu na nduguye lakini mioyoni walikuwa wametengwa na ulimwengu mpana wa Siri nyingi .
Mama mtu na dada mtu wakiwa wameinamisha nyuso zao wakiomboleza ,yeye mzee alikuwa akitoa salute za mwisho kwa mwanaye wa kwanza kama jembe lililotumikia KGB kwa uzalendo wa Hali ya juu akiwa na ile Sense of proud.

kwenye idara nyeti hizi za usalama umbea ni kitu Cha kawaida sana . Bwana Oleg alipaswa kurudi Tena nchini Denmark kikazi . Hizi taarifa walikuwa Nazo Hadi PET/M16 .
Halo ama kweli duniani hamna Siri na ni mwendo wa kuviziana tu Kwa kwenda mbele plus uyuda iskariote Kila sehemu
 
10



unapotumwa kama mwanadiplomasia mwakilishi wa nchi yako kwenye nchi nyingine, taarifa zako zinatumwa kwanza huko kwa ajili ya kukagua record zako, ikiwemo ku process visa n k. Taarifa zinazokaguliwa pia wanaangalia nchi ulizowahi kwenda,marital status n.k. Kwa kifupi wanakufanyia ukaguzi wa kutosha through papers ,Nchi husika ikiona hauna shida wanatoa go ahead na kuendelea na taratibu zingine kuruhusiwa kuingia.
Taarifa za bwana Oleg ikiwemo tuhuma za uwezekano wa kuwa jasusi la KGB zilikuwa zipo mezani. kumbuka file la Oleg waliokuwa nalo MI6 walililipa jina SUNBEAM likiwa linasimamiwa na afisa guscott waliona kwamba huenda Denmark haitaweza kumpokea kama mwakilishi huyo wa kidiplomasia kutoka urusi tena kutokana na record zake. Hivyo MI6 wakatuma kachero Hadi Denmark kuwashawishi PET wakubali ujio wake huko,ikiwa na maana kuruhusu visa itakayotumwa ubalozini ifanyiwe clearance zote na kumruhusu kuingia Denmark na taratibu zingine za kidiplomasia kwa maana M16/M15 yaliamini huenda kumtumia jasusi wa KGB kupata taarifa nyeti na mipango yote ya Kremlin kutawasaidia sana hususan wakati huo vita baridi kati ya Soviet bloc na west ulikuwa unatokota jikoni na muda wowote linaweza kuiva na kuwa vita rasmi ya dunia.
Hivyo MI6 wakamtuma kachero wao Hadi Copenhagen aliyeitwa Richard bromhead.

Siku hazigandi taratibu zilifuatwa hatimaye visa ya bwana Oleg Gordievsky ikawa approved kwa msaada wa MI6 Kwani PET walikuwa wanakaza ila walilegeza wakaamua kuruhusu Oleg arudi Denmark.Haya yote bwana bromhead aliambiwa awe attention Hadi huyu bwana ana report kituo chake Cha kazi kwa kufuatilia kila hatua .
Oleg na mkewe Yelena walifika Tena Copenhagen oktoba 11,1972. kwa mujibu wa boss wake Oleg ,Dimitri Yakushin, majukumu yake ndani ya Denmark sio Tena ku run na kusimamia operation za illegals la hasha. majukumu yake mapya ya Oleg yalikuwa ni ujasusi wa kisiasa. Hii ni ujasusi wa kuwatumia wanasiasa wawakilishi na upinzani , viongozi wa vyama vya wafanyakazi,wafanyabiashara wakubwa pamoja na waandishi wa nchi hiyo ya Denmark kupata infos za kiintelijensia kwa ajili ya Soviet . Ugumu ukaja kwamba kiasili nchi ya Denmark ni raia wachache sana ambao walikuwa interested na Soviet ,hivyo bwana Oleg huenda angetumia njia ya ziada kupata infos za kutosha.Money( the Grease that oils the wheels of so much espionage). Na njia nyingine za ushawishi ikiwemo kujipendekeza kwa baadhi ya wanasiasa au propaganda za kutengeneza fake news.
kila jaribio la kuwatumia baadhi ya wa danish ambao ni public figures kupata access ya infos ziligonga mwamba . Lakini bwana Oleg aliweza kumpata kiongozi wa chama Denmark's socialists people's party bwana Gert Petersen ambaye alikuwa mbunge wa bunge la ulaya kwa wakati huo. Alifanikiwa kujenga naye mazoea ya Siri sana na huyu bwana alipewa codename ZEUS . Na kweli huyu bwana mbele ya pesa hukumweleza kitu(alikuwa ni chapombe mzuri ) alitema Siri za kutosha hususan sera za nje ya nchi ya Denmark na mipango mikakati yote.
Baadaye Tena Copenhagen ikapata balozi mpya kutoka urusi aliyeitwa Alfred mogilevchik na akamchagua Bwana Oleg kama naibu wake.
Hii teuzi ikawa inamaanisha kwamba bwana Oleg anapanda ngazi taratibu ndani ya KGB . Na kadri alivyopanda ngazi ndivyo alivyokuwa anapata access ya taarifa nyingi za Siri za Soviet . Haya yote M16 na PET wanaangalia kupitia radar zao.
Ndani ya Denmark ilitarajiwa Kuna hafla ingefanyika siku za karibuni na miongoni mwa wageni waalikwa wangekuwemo maafisa wa balozi mbalimbali, wawakilishi, wafanyabiashara wakubwa n.k. Hivyo bwana bromhead jasusi wa M16 alikuwa na picha za Siri za Bwana Oleg hususan zilizopatikana wakati Wana process passport yake.Hafla ilifanyika kwenye ukumbi wa rådhus hapo Jiji la copenhagen. Na kweli kama ilivyotarajiwa bwana Oleg alihudhuria Hivyo bwana bromhead aliweza kumuona . wakakutana sehemu ya Diplomatic lunch club hapo ukumbini. Hapo bwana Oleg hakuweza ku notice huyu Bwana bromhead ni jasusi anayempeleleza yeye. Aliona ni mgeni mwalikwa kama waalikwa wengine [emoji28] . Waliongea Convos za hapa na pale kama tu wanadiplomasia wawili waliokutana kwenye party. Taarifa za bromhead kukutana na Oleg kwenye party alizituma nyumbani uingereza. swala na kipengele kikawa ni mawasiliano. Bromhead hakuwa anajua ki Russia ,lugha ya ki danish alikuwa anaongea kile cha kuunga . Ila bwana Oleg alikuwa anaongea kijerumani na ki danish kwa ufasaha ila kingereza cha you know, yeah, yes ok . Kwa kifupi kile Cha kuombea maji[emoji28][emoji28]. Kikwazo Cha kwanza ilikuwa ni lugha.
Kwenye hii dunia ya ujasusi ,kumwajiri jasusi wa nchi nyingine Ili akupe infos za nchi yake ni mchakato mgumu sana na inahitaji mambo ya ziada kufanyika.endapo pesa kama nyenzo kubwa kufeli.[emoji88]. kwa mfano TISS watake kumwajiri jasusi wa Rwanda aweze kutoa infos za Rwanda ni mchakato kidogo mzito . Endapo huyo jasusi pesa sio kipaumbele chake .Ndivyo hili swala lilikuwa linamwangaisha bwana bromhead jasusi la M16. Maana waliona kumshawishi bwana Oleg Gordievsky ni kazi ngumu ambayo ingeweza kuleta mgongano wa kidiplomasia na kashfa kubwa sana endapo mpango huu kabambe unge leak.
M16 Wakaamua kusuka Mpango mwingine ili waweze kumshawishi Oleg.
Iliandaliwa party nyingine ndogo ya kidiplomasia Ili waweze kualikwa maafisa kadhaa wa ubalozi na delegates ambao wako affiliated na urusi ikitarajiwa Oleg Gordievsky na jopo lake wangehudhuria.
 
Watu8 half American Chizi Maarifa Numbisa Clepatina Elton Tonny Carleen moneytalk Shunie mama D stevemollel To yeye Unique Flower kimsboy IBRA wa PILI Litro Big Phil Lavan Island mtu chake
 
IMG_20230427_102925_670.jpg

Oleg akiwa na best yake ambaye ni mfanyakazi mwenzake Mikhail lyubimov hapo ubalozi wa Copenhagen kwenye fukwe za bahari ya Baltic
 
Back
Top Bottom