Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

13


Wiki tatu baadaye bromhead na Oleg walikutana kwa Siri sana kwenye local bar iliyoko uchochoroni kwenye Giza Giza . Na mpaka wanafika eneo Hilo walihakikisha hakukuwa na dalili za kufuatiliwa (dry-cleaning) . Mazungumzo Yao yalikuwa ni kama business talk tu ya kawaida Lakini tangu mwanzo lugha baina ya Hawa jamaa wawili ilikuwa ni kipengele sana hususan kwenye kujadili Mambo seriously kidogo. Oleg kingereza kilikuwa hakipandi, alikuwa anajua kijerumani na ki danish na kirussia ,yeye mwenzake alikuwa anajua kingereza tu huku lugha nyingine ni za kuungaunga.
Bromhead alimwambia tu Oleg kwamba muda mfupi ujao ataondoka Copenhagen (alitarajiwa kupangiwa majukumu mengine) hivyo , jukumu la kukutana naye angemwachia ofisa mwenzake hapohapo Denmark ambaye pia ni muongeaji mzuri wa lugha ya kijerumani. Vilevile huyu bwana alipaswa kumwonyesha eneo ambalo ni SAFE HOUSE kwa ajili ya kukutana . Eneo ambalo sio rahisi kushtukiwa kuliko hiyo ya kukutana kwenye bar au hotelini . Na vilevile angepewa funguo za nyumba hiyo ikiwemo na usafiri wa siri. Kweli ndani ya week bwana Oleg alionyeshwa nyumba hiyo na bromhead iliyokuwa Mitaa ya Charlottenund.
Bromhead alimwelezea huyu bwana swala la yeye kuwapa infos za urusi lilijulikana na maafisa wachache sana wa PET , vilevile hata M16 ni maafisa wa ngazi wa juu wachache wanaofahamu uwepo wake kama agent SUNBEAM. Na hawajui jina lake halisi ni nani . Idara za ujasusi zina amini sana Siri haiuwi kwa mtu mmoja maana ni hatari na vilevile haipaswi watu wengi waijue. Hivyo Siri Ili iwe Siri kikundi kidogo sana Cha watu kinapaswa kufahamu. Ndivyo ilivyokuwa kwa file la bwana Oleg. Kwa sababu bromhead alimsisitizia lazima iwe Siri maana yawezekana Kuna agents walioko ndani ya PET au M16 wakasanukia mpango wakamrepoti huko Moscow ikawa ni kizaazaa.
Alijulikana kwa codename SUNBEAM tu na sio jina lake halisi. Alimwakikishia usalama wake kwa kiasi fulani.
Baada ya hapo bromhead aliagana na Oleg akimtakia kila la heri na kurudi makao makuu M16 huko London kwa maboss wake.
Baada ya kutua tu London boss wa bromhead alimuuliza maswala kadhaa kuhusu asset hiyo muhimu . Lengo ni kutaka kuhakikisha mipango Yao inaenda sawia kuhusiana na swala la bwana Oleg jasusi wa KGB kuwafanyia kazi mashirika ya kijasusi ya magharibi hususani M16.

Wanasema kwamba kuhamisha file la KAZI kwenye idara za ujasusi kutoka kwa agent mmoja kwenda kwa mwingine sio kazi nyepesi hata kidogo na inachukua mchakato sana . Kwa maana file la Oleg au SUNBEAM lilikuwa ni file zito kidogo na ilihitajika juhudi za ziada maana one mistake inge compromise kila kitu ikiwemo maisha ya Oleg yawe hatarini na kuwe na mgongano au Mgogoro wa kidiplomasia baina ya west na Urusi.
Hivyo January 1 1975 bromhead alirudi kwa siri sana huko Denmark akipitia Sweden akitumia utambulisho fake Hadi mwonekano wake. Lengo la safari hii ni kwamba alikuja kukutana na agent mwenzake wa M16 aliyeitwa Philip Hawkins kwa ajili ya kumkabidhi file la Oleg aweze ku deal naye. Baada ya hapo bromhead alikutana na Oleg kwenye safe house kwa ajili ya kutambulishana na Hawkins ,baada ya mazungumzo ya hapa na pale bromhead aliondoka. Ikawa kwamba Oleg na Hawkins wangeshirikiana.


Tujadili,[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

Swali ni kuwa kwanini mtu huamua hufanya ujasusi, inakuwaje mtu anahatarisha usalama wa hata familia yake, au anaamua kuacha kazi yenye kipato kizuri na kuwa jasusi ,Na Je Nini kinafanya mtu kuamua kufanyia ujasusi idara nyingine na kuisaliti idara iliyomwajiri..?
Wanasema ujasusi Huwa unakuja na shepu ya kila aina . Mwingine anaweza kuingia kwenye ujasusi kwa kusukumwa na itikadi,siasa na pia uzalendo. Wengine huingia huko kwa ajili ya kulipiza kisasi, wengine kulaghaiwa kingono ,kitapeli ,ujinga na pia sifa na majigambo ya kutaka kuonekana (kujipendekeza) . Pesa ikiwa kama kichocheo tu.
Bwana Pavel sudoplatov ambaye alikuwa ni KGB spy master enzi za Stalin aliwahi kusema kwenye kuajiri Hadi mtu kujiunga kuwa jasusi ni kwamba: nanukuu " search for people who are hurt by fate or nature-the ugly, those suffering from an inferiority complex,craving power and influence but defeated by unfavourable circumstances... .......In cooperation with us, all these find a peculiar compensation. The sense of belonging to an influential and powerful organization will give them a feeling of superiority over the handsome and prosperous People around them".
Hapa kwa tafsiri ya harakaharaka na isiyo rasmi ni kwamba mtu kujiunga na kuwa jasusi mzuri ni kuwatafuta wale ambao wako broken hawana mvuto ,wanaosumbuliwa na kutokujiamini ila wanataka kulazimisha kukubalika na wenye njaa na madaraka .wakiwekwa kitengoni watafanya vizuri na pia watafanya kazi kwa kujiamini kuliko wale wenye mvuto au wenye elimu kubwa kuwaliko wao hivyo watajihisi wenye nguvu wakiwa kitengoni [emoji39][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28].
Kwa mujibu wa KGB wanasema kwamba Kuna kanuni ya Hadi mtu kuwa jasusi MICE.

M-money
I-ideology
C-coersion
E-ego
1. Kwamba pesa inamfanya mtu awe tayari kujiunga na idara au kuuza Siri za nchi yake kwa vipande kadhaa vya shekeli. Money talks even there's great moment of silence.
2. Ideology au itikadi (capitalism vs communism) . Hata hapa kwetu huenda walioko huko kitengoni TISS ni matunda ya itikadi za ujamaa za Nyerere [emoji2][emoji2].
3.coercion.Hii ni labda mtu analazimishwa kufanya ujasusi kwa kulazimishwa pasipo ridhaa Yake. Mfano kushikiliwa mateka kwa familia yake ,mke na watoto au watoto tu. Haya hutokea . Au labda kutishiwa kuuawa endapo asipofanya kazi za kitengo.
4.Ego- nafikiri hii ni sababu ya kisaikolojia zaidi , kiburi ,kujifanya much know wa kila kitu ,kutaka kuonekana wewe ndio wewe ,yaani wewe ndio kusema ,ni sababu mojawapo watu kujiunga humo . Na hapa ndio pale wale hata kama kweli kaajiriwa kitengoni aonekane au ajulikane na kila mtu Ili aogopwe."UNAJUA MIMI NI NANI?" wako kwenye hiki kipengele [emoji38][emoji38][emoji38].
Na wanasema wapweke huwa ni rahisi kuwa majasusi wazuri na vilevile wengi wa majasusi ni wapweke wa kutupwa.. Kuna ukweli kiasi fulani.

Baadhi ya Wanasaikolojia wanasema kwamba mpaka jasusi wa nchi Moja kuisaliti nchi yake kuamua kuifanyia kazi nchi nyingine inawezekana ni mgongano kati ya inner world and outer world Kwa maana ya Mgogoro wa nafsi. Hili yawezekana kwa bwana Oleg. Kiitikadi alikuwa ni mcommunist Lakini baada ya kutoka nje ya Russia na kwenda kufanya kazi na kuonja ladha ya umagharibi kiitikadi alikuwa compromised . Mfumo aliokuwa akiutumikia ulikuwa wa kinyonyaji na katili kuliko mfumo alioenda kuukuta kwenye dunia nyingine. Je hii ilikuwa ni Sababu ya Oleg kuamua ku switch kuwa jasusi wa KGB na kuwafanyia kazi west?.
na pia dunia ya nje iliyoamua Oleg kuwa double agent labda ni mpasuko wa kiitikadi kati ya West na east pale aliposhuhudia ujenzi wa ukuta wa Berlin.
Na pia the inner world au tuseme Mgogoro wa nafsi , kutaka kulipiza kisasi kutokana na madhila ambayo familia yake ilipitia hususan mama yake alivyoteswa na mfumo wa kikomunisti zamani zile za Stalin . Hakukuwa na majibu ya uhakika kwenye hili.
 
10



unapotumwa kama mwanadiplomasia mwakilishi wa nchi yako kwenye nchi nyingine, taarifa zako zinatumwa kwanza huko kwa ajili ya kukagua record zako, ikiwemo ku process visa n k. Taarifa zinazokaguliwa pia wanaangalia nchi ulizowahi kwenda,marital status n.k. Kwa kifupi wanakufanyia ukaguzi wa kutosha through papers ,Nchi husika ikiona hauna shida wanatoa go ahead na kuendelea na taratibu zingine kuruhusiwa kuingia.
Taarifa za bwana Oleg ikiwemo tuhuma za uwezekano wa kuwa jasusi la KGB zilikuwa zipo mezani. kumbuka file la Oleg waliokuwa nalo MI6 walililipa jina SUNBEAM likiwa linasimamiwa na afisa guscott waliona kwamba huenda Denmark haitaweza kumpokea kama mwakilishi huyo wa kidiplomasia kutoka urusi tena kutokana na record zake. Hivyo MI6 wakatuma kachero Hadi Denmark kuwashawishi PET wakubali ujio wake huko,ikiwa na maana kuruhusu visa itakayotumwa ubalozini ifanyiwe clearance zote na kumruhusu kuingia Denmark na taratibu zingine za kidiplomasia kwa maana M16/M15 yaliamini huenda kumtumia jasusi wa KGB kupata taarifa nyeti na mipango yote ya Kremlin kutawasaidia sana hususan wakati huo vita baridi kati ya Soviet bloc na west ulikuwa unatokota jikoni na muda wowote linaweza kuiva na kuwa vita rasmi ya dunia.
Hivyo MI6 wakamtuma kachero wao Hadi Copenhagen aliyeitwa Richard bromhead.

Siku hazigandi taratibu zilifuatwa hatimaye visa ya bwana Oleg Gordievsky ikawa approved kwa msaada wa MI6 Kwani PET walikuwa wanakaza ila walilegeza wakaamua kuruhusu Oleg arudi Denmark.Haya yote bwana bromhead aliambiwa awe attention Hadi huyu bwana ana report kituo chake Cha kazi kwa kufuatilia kila hatua .
Oleg na mkewe Yelena walifika Tena Copenhagen oktoba 11,1972. kwa mujibu wa boss wake Oleg ,Dimitri Yakushin, majukumu yake ndani ya Denmark sio Tena ku run na kusimamia operation za illegals la hasha. majukumu yake mapya ya Oleg yalikuwa ni ujasusi wa kisiasa. Hii ni ujasusi wa kuwatumia wanasiasa wawakilishi na upinzani , viongozi wa vyama vya wafanyakazi,wafanyabiashara wakubwa pamoja na waandishi wa nchi hiyo ya Denmark kupata infos za kiintelijensia kwa ajili ya Soviet . Ugumu ukaja kwamba kiasili nchi ya Denmark ni raia wachache sana ambao walikuwa interested na Soviet ,hivyo bwana Oleg huenda angetumia njia ya ziada kupata infos za kutosha.Money( the Grease that oils the wheels of so much espionage). Na njia nyingine za ushawishi ikiwemo kujipendekeza kwa baadhi ya wanasiasa au propaganda za kutengeneza fake news.
kila jaribio la kuwatumia baadhi ya wa danish ambao ni public figures kupata access ya infos ziligonga mwamba . Lakini bwana Oleg aliweza kumpata kiongozi wa chama Denmark's socialists people's party bwana Gert Petersen ambaye alikuwa mbunge wa bunge la ulaya kwa wakati huo. Alifanikiwa kujenga naye mazoea ya Siri sana na huyu bwana alipewa codename ZEUS . Na kweli huyu bwana mbele ya pesa hukumweleza kitu(alikuwa ni chapombe mzuri ) alitema Siri za kutosha hususan sera za nje ya nchi ya Denmark na mipango mikakati yote.
Baadaye Tena Copenhagen ikapata balozi mpya kutoka urusi aliyeitwa Alfred mogilevchik na akamchagua Bwana Oleg kama naibu wake.
Hii teuzi ikawa inamaanisha kwamba bwana Oleg anapanda ngazi taratibu ndani ya KGB . Na kadri alivyopanda ngazi ndivyo alivyokuwa anapata access ya taarifa nyingi za Siri za Soviet . Haya yote M16 na PET wanaangalia kupitia radar zao.
Ndani ya Denmark ilitarajiwa Kuna hafla ingefanyika siku za karibuni na miongoni mwa wageni waalikwa wangekuwemo maafisa wa balozi mbalimbali, wawakilishi, wafanyabiashara wakubwa n.k. Hivyo bwana bromhead jasusi wa M16 alikuwa na picha za Siri za Bwana Oleg hususan zilizopatikana wakati Wana process passport yake.Hafla ilifanyika kwenye ukumbi wa rådhus hapo Jiji la copenhagen. Na kweli kama ilivyotarajiwa bwana Oleg alihudhuria Hivyo bwana bromhead aliweza kumuona . wakakutana sehemu ya Diplomatic lunch club hapo ukumbini. Hapo bwana Oleg hakuweza ku notice huyu Bwana bromhead ni jasusi anayempeleleza yeye. Aliona ni mgeni mwalikwa kama waalikwa wengine [emoji28] . Waliongea Convos za hapa na pale kama tu wanadiplomasia wawili waliokutana kwenye party. Taarifa za bromhead kukutana na Oleg kwenye party alizituma nyumbani uingereza. swala na kipengele kikawa ni mawasiliano. Bromhead hakuwa anajua ki Russia ,lugha ya ki danish alikuwa anaongea kile cha kuunga . Ila bwana Oleg alikuwa anaongea kijerumani na ki danish kwa ufasaha ila kingereza cha you know, yeah, yes ok . Kwa kifupi kile Cha kuombea maji[emoji28][emoji28]. Kikwazo Cha kwanza ilikuwa ni lugha.
Kwenye hii dunia ya ujasusi ,kumwajiri jasusi wa nchi nyingine Ili akupe infos za nchi yake ni mchakato mgumu sana na inahitaji mambo ya ziada kufanyika.endapo pesa kama nyenzo kubwa kufeli.[emoji88]. kwa mfano TISS watake kumwajiri jasusi wa Rwanda aweze kutoa infos za Rwanda ni mchakato kidogo mzito . Endapo huyo jasusi pesa sio kipaumbele chake .Ndivyo hili swala lilikuwa linamwangaisha bwana bromhead jasusi la M16. Maana waliona kumshawishi bwana Oleg Gordievsky ni kazi ngumu ambayo ingeweza kuleta mgongano wa kidiplomasia na kashfa kubwa sana endapo mpango huu kabambe unge leak.
M16 Wakaamua kusuka Mpango mwingine ili waweze kumshawishi Oleg.
Iliandaliwa party nyingine ndogo ya kidiplomasia Ili waweze kualikwa maafisa kadhaa wa ubalozi na delegates ambao wako affiliated na urusi ikitarajiwa Oleg Gordievsky na jopo lake wangehudhuria.

Am just curious hivi Inawezekana mtu kuteuliwa ubalozi kwenda kuwakilisha nchi nyingine akiwa hajaoa?does marital status matter?
 
Back
Top Bottom