Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K


Hii sehemu ilikuwa fupi sana boss
Ongezea weekend ni ndefuuu
 
Na marafiki zangu ni wa Irish aisee wakija bongo wakienda supermarket wananunua bidhaa made in Irish Kwa kuzitafta na wanafurahia kabisa huku Tanzania sijui kwanini hatupendi kununua vitu made in Tanzania tunapenda vya nje
We mtanzania humjui kwa ulimbukeni?Mtz yeye kutumia vitu vya kutoka nje,kwake ni sawa na kuwaringishia wengine kuwa ana mkwanja mnene na elimu ya kutosha eti!.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni hovyo kweli yani hata story ya yoga alijifanyaga yake na kutoza watu ili kupata updates baada ya yoga ku stop updates na yeye aka stop, heri mleta mada ana share humu free Kwa wote kujifunza Sasa huyu mwizi anatoza wengine
Hivi yoga kapotelea wapi? Bi dada alinikamata vyema ghafla akapotea nami nikawa mvivu kufuatilia Habari za Mr. born town.
 
Na ile story ya dada Yoga mbona uliikopi na kuipeleka twitter?
 
Hivi yoga kapotelea wapi? Bi dada alinikamata vyema ghafla akapotea nami nikawa mvivu kufuatilia Habari za Mr. born town.
Nakwambia I think plan ilivokuwa inaendelea born town akagundua mchezo na kuudhibiti mapema ikiwemo new CEO kufatiliwa ma file yake ikiwemo machafu so imebidi new CEO awe mdogo ka piritoni,;ila kuja Kwa Paka nchini Kuna jambo
 
21


Baada ya kufika safe walianza kutambulishana rasmi sasa kila mmoja akawa familiar na mwenzake .
Guscott alimwambia Oleg eneo hili ndio ingekuwa ni kama safe house na wangekutana hapa mara kwa mara kwa kila walipopata wasaha wa kukutana na Oleg angetoa umbea wake kwa M16 pasipo kugundulika au kufuatiliwa .
Maafisa wa M16 kipindi oleg akiwa kwao walikuwa wameandaa mpango mkakati wa kumtorosha bwana Oleg na familia yake nchini urusi endapo angekuja kuhisiwa na KGB anaifanyia uingereza kazi kwa Siri Na walitarajia hili lingetokea. Huo mpango ulipewa jina la operation PIMLICO. hivyo wakawa wanampa kama briefings za mpango huo uliokuwa kwenye makaratasi.
Ni kwamba hapo kabla M16 hawakuwahi kuwa na access ya kumtumia jasusi wa KGB ndani ya uingereza anayefanya kazi under official diplomatic cover. Hivyo Sasa kwakuwa Oleg alikuwa ndani ya uingereza waliamua kumbadilisha jina la uficho la SUNBEAM na kupewa jina la NOCTON . Asili ya jina hili ni Kijiji kilichoko huko Lincolnshire uingereza. Kulikuwa na sababu ya kumbadilisha jina la uficho.
Wanadai kwamba Japo M16 na M15 ni mashirika pacha lakini kila mmoja alikuwa anafanya kazi kivyake na kwa namna anavyojua yeye .. kwa mfano shirika la M15 lilikuwa Lina deal sana na domestic surveillance ndani ya uingereza, pia lilikuwa na wajibu katika kuwafuatilia nyendo za maafisa wa ki Soviet hapo London. Hivyo M16 wa wakaona M15 wangeweza ku compromise mpango wa kumtumia Oleg kuwapa taarifa . Wakaamua kuwashirikisha baadhi ya maafisa wachache sana wa ngazi za juu wa M15 ikiwemo D.G. Lengo la kuwashirikisha Hawa M15 ni kulinda asset Yao inayowapa info asije akagundulika na maafisa wengine wa kitengo na mpango uka leak. Huu mpango wa mashirikiano baina ya haya mashirika pacha kishughulika na hili swala la Oleg au NOCTON waliupa jina la uficho la LAMPAD.
Baada ya hayo yote baada ya kupeana briefings za hapa na pale baina ya Oleg na maafisa hao wa M16 wakaagana na kuondoka. Ni kwamba Oleg alipaswa kuwa katika safe house hiyo na kuwapa infos makachero hao wa uingereza kila ilipopatikana nafasi
Oleg pia alianza kuwapa infos za baadhi ya maafisa wa M16 Waliokuwa wanawafanyia kazi Soviet. Kwa mfano hapo nyuma ndani ya M15 kulikuwa Kuna afisa mstaafu aliyeitwa Roger Hollis ilisemekana alikuwa ni mole ndani ya shirika Hilo na alikuwa anavujisha taarifa nyeti kwa KGB, lakini kwa mujibu wa taarifa za Siri alizokuwa Nazo Oleg ni kwamba mchawi hakuwa huyo Hollis Bali alikuwa ni afisa mwingine mstaafu wa M16 aliyeitwa John cairncross aliyekuwa ni mole wa Soviet mwaka 1964.
Pia Oleg Kutokana na kufukunyua ma file ya KGB ,aligundua kwamba kulikuwa Kuna agent aliyeitwa ELLI ambaye M16 hawakuwahi mjua hapo kabla ,aliyepandikzwa na Soviet mwaka 1946 na alikuwa anaitwa Leo Long na alikuwa amepandikizwa kwenye chuo Cha Cambridge akitoa Siri kwa Soviet wakati wa vita ya pili ya dunia. Pia Oleg aliendelea kutema Siri ,kwamba hata aliyekuwa mtaalamu na injinia wa mabomu ya nyuklia aliyekuwa anaifanyia kazi
Idara ya kijeshi ya Britain's wartime atomic bomb research aliyeitwa Bruno pontecorvo alikuwa anauza taarifa za Siri za kijeshi kwa urusi wakati huo. Pia Oleg aliwapa infos za wanasiasa hususan wa chama Cha labour party walioko madarakani waliokuwa kwenye payroll ya KGB .Hizi infos zilitua mezani kwa M16 na zikakaliwa kikao na maafisa wa ngazi za juu waliokuwa wanajua hili swala la NOCTON. Taarifa hizi Ziliwashtua na vilevile kuwashangaza.
Katika taarifa hizi zote , M16 waliamua kuipa uzito taarifa kuhusu Michael foot kiongozi wa upinzani wa chama Cha labour ambaye alitarajiwa kuchuana na margaret thatcher kwenye uchaguzi wa 1984. M16 waliona endapo Michael Foot angeshinda uchaguzi uliotarajiwa na hizi taarifa kuwekwa public , ingeleta Mgogoro mkubwa wa kikatiba kwa taifa la uingereza na ingekuwa kashfa kubwa ya kisiasa. Hili swala wakapewa M15 Kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi walizoona ingemfaa. D.G wa M15 akalifikisha hili swala la tuhuma za foot mezani kwa katibu mkuu wa bunge (chief secretary) sir Robert Armstrong . Huyu alikuwa ni mshauri mkuu wa P.M wa uingereza na vilevile alikuwa na jukumu la maswala mazima katika kusimamia kamati za usalama na intelejensia kwa taifa la uingereza. Amewahi kuhudumu hapo nyuma kama principal private secretary kwa mawaziri wakuu kama Harold Wilson na Edward heath. Alipofikishiwa hizi taarifa aliamua kuziminyia chini kwa kuona hizi tuhuma zipo kisiasa zaidi. Akaona asilifikishe kwa Margaret thatcher. Huyu bwana Armstrong alikuwa ni miongoni mwa washauri walioaminika na margaret thatcher. Armstrong aliona ngoja kwanza asimwambie kuhusu hizi tuhuma za mpinzani wake wa kisiasa Michael foot. Ripoti zinadai endapo Armstrong angemwambia Margaret thatcher , thatcher angetumia hizo tuhuma kumkaanga Michael Foot kwenye kampeni. Kifupi Armstrong hakuwahi mwambia yoyote tuhuma za Michael Foot hata kwenye chama Cha conservative, labour au hata marafiki wa uingereza kama marekani. Swala likabaki kwa M16 , endapo Michael foot akishinda uchaguzi mkuu ingeleta mtafaruku kidogo ,na ingebidi Hadi malkia wa uingereza apewe taarifa . Lakini kama bahati Michael foot a.k.a agent BOOT hakushinda uchaguzi huo.

Mwaka 1982 joto la Vita baridi lilikuwa limepanda sana kwa pande zote east na west .. Kremlin waliamini kwamba nchi za magharibi hususani uingereza wangeanzisha vita halisi.
 

Huyu ni sir. Robert Armstrong.aliyekuwa cabinet secretary na mshauri wa karibu wa Margaret thatcher.



Leila akiwa na wanawe wawili maria na Ana nje ya mkahawa mmoja mtaa wa Trafalgar square huko London.


Jengo la ubalozi wa Soviet hapo London mtaa wa 13 Kensington palace gardens.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…