Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Nasimama na wewe
 
Buyoye alichomaind ni kwamba yeye kule telegram anawauzia afu huku mwana anatoa bure, kwahyo wasiwasi wake huenda watu wasiende kulipia kule ili waje kusoma huku bure ndo mana kama kapaniki vile mpaka anakuja na Id nyingi nyingi
 
Usijali ndugu, katika jumuiya ya watu wapo mchanganyiko mbali mbali, haswa kwenye mambo ya riziki fitina hazikosekani.

Hakuna popote ulipovunja sheria wala hakuna popote ulipogusa maslahi ya mtu , kwa hiyo usiwajali hao, wapuuze endelea kusimamia point yako.

Binafsi nakupa pongezi na shukurani.
 
Buyoye alichomaind ni kwamba yeye kule telegram anawauzia afu huku mwana anatoa bure, kwahyo wasiwasi wake huenda watu wasiende kulipia kule ili waje kusoma huku bure ndo mana kama kapaniki vile mpaka anakuja na Id nyingi nyingi
Mbona yeye huchukua humu story za watu na kwenda kuwalipisha wasio jua humu JF [emoji2][emoji2][emoji2] mbwa kala mbwa
 
25.


Ingawaje Margaret thatcher kwa wakati huo akiwa P.M wa uingereza alijua uwepo wa jasusi wa KGB ndani ya uingereza , anayefanya kazi na idara za kijasusi za uingereza. Kamwe maafisa usalama wa vitengo hivyo hawakuwahi mwambia identity yake halisi ni nani haswa. Hii tokea mwanzo ,M16 na washirika wake hawakutaka utambulisho halisi wa Oleg utambulike kwa sababu za usalama wake binafsi na pia kwa afya ya kidiplomasia baina ya nchi ya uingereza na Russia kwa wakati huo.Na thatcher ndie P.M pekee wa uingereza aliyekuwa anafuatilia swala la NOCTON kwa karibu swala lilikokuwa mikononi mwa taasisi za kiusalama . Inasemekana kwamba kupitia Oleg , uingereza na nchi za kimagharibi zilikuwa Zina uwezo wa kutambua think tank ya Kremlin walikuwa wanawaza Nini na mipango Yao yote waliopanga.
Kwa mfano Kipindi mashirika haya ya uingereza yakiwa katika process za kumsaka Koba aliyekuwa karibu ku expose identity ya Oleg ,nao KGB walikuwa wanataka kuhakikisha Margaret thatcher anapoteza uchaguzi wa mwaka 1983 akichuana na Michael foot. Russia Walimpa Margaret thatcher Jina la "IRON LADY " kama tusi kupitia magazeti ya propaganda ya urusi kama kumchafua kisiasa. Hivyo bahati nzuri thatcher alishinda uchaguzi kwa kura za kutosha Na inasemekana endapo Michael foot angeshinda uchaguzi ule Basi ni dhahiri Oleg angegundulika kama msaliti dhidi ya Soviet. Kumbuka huyu foot alikuwa ni pandikizi la KGB.
Baada ya uchaguzi kupita thatcher alijikita Sasa rasmi katika kitisho kilichokuwepo mbele yake . Vita baridi ilikuwa inakaribia kuwa ni vita halisi . Vita vya nyuklia baina ya west na east. Hii ni kutokana na panick ya Soviet kuanzisha operesheni ya RYAN. Ambapo kupitia operation hii Russia walikuwa wanatafuta sababu za kuingia vitani rasmi na nchi za west. Kumbuka huu mpango uliandaliwa na Yuri Andropov ambaye kwa wakati huo alikuwa rais wa Russia. Mshirika wa uingereza wakati huo marekani alikuwa anazidi kujizatiti kijeshi katika kukabiliana na vitisho vya nyuklia kutoka Soviet.

Na kuonyesha urusi ilikuwa imepaniki , tarehe 1 mwezi September mwaka 1981 ndege ya kijeshi ya umoja wa Soviet iliidungua ndege ya abiria aina Boeing 747 ya shirika la ndege la Korea iliyokuwa ikiruka kwenye anga ya Soviet. Ndege hii iliua abiria 269 pamoja na wahudumu wake . Hili tukio lilizusha tafrani baina ya nchi za magharibi na Urusi. Mara ya kwanza Urusi walikataa kutokuhusika na tukio hili ila baadaye walikubali. Walidai kwamba ndege hiyo ilikuwa ni ya kijasusi iliyokiuka taratibu na sheria kuruka kwenye anga yao na pia ilikuwa ni kama ishara ya uchokozi kutoka marekani . Kutokana na tukio hili bunge la congress likapitisha hoja ya kuongezwa bajeti ya matumizi ya kijeshi kwa lengo la kujilinda. Na Urusi wakaona Sasa hapa vita inaenda kuzuka kweli . Balozi mbalimbali zilizokuwa nchi za ulaya magharibi zikapewa order ya kulinda raia wao huko pamoja na Mali zao dhidi ya shambulio lolote. Pia ubalozi wa urusi uliopo London ulipewa order ya kuzima maandamano ya raia yoyote yaliyotarajiwa kufanyika nchini humo kupinga kitendo Cha urusi kutungua ndege ya abiria na kuua watu wasiokuwa na hatia. Hizi taarifa zilipenyezwa Hadi kwa M16 na bwana Oleg.
Wanahistoria waliamini na kutabiri endapo kutazuka vita halisi basi uwezekano wa kutumia silaha za sumu na nyuklia ulikuwa ni mkubwa kwa Sababu kipindi hicho kila upande ulijikita katika kutengeneza silaha nzito nzito za maangamizi. Na ingekuwa ni nafasi kwao kuona ni silaha za upande upi zilikuwa na damage impact dhidi ya mwingine.ilihitajika nguvu ya ziada kuzuia kutokea kwa vita. Lakini wao uingereza kupitia taarifa za Siri nyingi alizokuwa anatoa Oleg , waliamini vita halisi isingeweza kutokea . Ilikuja kubainika baadaye Russia walianza kutengeneza karakana za kutengeneza ndege za kivita huko ujerumani. Na vilevile ilisemwa kulikuwa na nyambizi zilizokuwa zimebeba makombora za ki Soviet zilizokuwa zimefichwa chini ya bahari ya Baltic zisije kugundulika. Taarifa hizi Oleg alichelewa kuzipata lakini CIA walizipata wa kwanza na kureport kwenye magazeti mbalimbali operation hizi za kijeshi za Urusi. Margaret thatcher akapendekeza taarifa za kijasusi alizokuwa anatoa bwana Oleg nao marekani wamegewe.
Kiuhalisia nchi za magharibi hazikuwa na mpango wa kupigana na umoja wa Soviet kijeshi . Tatizo lilikuwa la kwao Soviet kupitia operesheni Ryan wakiamini kwamba west walikuwa na Nia ya kuanzisha vita dhidi yao. Hivyo Margaret akaona ni vyema taarifa za kijasusi kutoka kwenye think tank ya Kremlin nao CIA wapewe Ili kuona uwezekano wa kuepusha vita . Kwenye personal diary ya Reagan aliandika hivi nanukuu." I feel the Soviet are.... So paranoid about being attacked that....we ought to tell them no one here has any intention of doing anything like that".
Diary ya Reagan iliendelea kusema nanukuu" Three years had taught me something surprising about the Russians: many people at the top of Soviet hierarchy were genuinely afraid of America and Americans..... I began to realize that many Soviet officials feared us not only as adversaries but as potential aggressors who might hurl nuclear weapons at them in a first strike" mwisho wa nukuu.
Haya yalikuwa ni maoni ya Reagan baada ya kuwa analetewa report zilizotokana na taarifa za Oleg (NOCTON) alizokuwa anatoa kupitia M16.
Kidogo kidogo CIA walitamani kujua source ya hizi valuable infos. Lakini M16 waliendelea kuficha identity yake. Makamu D.G. wa CIA wakati huo bwana Robert Gates alipokuwa anapitia taarifa alizokuwa anazitoa Oleg Kwa M16 ,alihitimisha na kusema kwamba CIA wamemisi kitu na walitamani huyo source awe wa kwao. Kwa kifupi CIA walitamani NOCTON angekuwa wa kwao. Taarifa za Oleg za KGB zilipotua kwa CIA walibadilisha baadhi ya mbinu katika ujasusi . Lakini Oleg hakuwa Salama sana na kutokugundulika



Hatimaye maelfu ya watu walikusanyika red square huko Moscow mwaka tarehe 14 Feb 1984,kuomboleza kifo Cha Yuri Andropov. Miongoni mwa viongozi wa kimataifa waliohudhuria alikuwa ni Margaret thatcher.
M16 kupitia Oleg alishauriwa ahudhurie kama ishara ya kuonyesha kwamba nchi za magharibi hazina kinyongo na Soviet na pia ilikuwa ni kama sababu ya kupunguza tension ya vita baridi kwa wakati huo.
 

Baadhi ya Wananchi kwenye nchi mbalimbali duniani wakiwa wanaandamana kutokana na kutunguliwa kwa ndege ya shirika la ndege la Korea KAL007.




Margaret thatcher akiwa na viongozi mbalimbali wa dunia wakiwa wamehudhuria ibada ya mazishi ya Yuri Andropov kiongozi wa Russia aliyeaga dunia . Mwaka 1983
 
Ana roho ya uwivu tu,uwivu usio na maana kila mtu ashinde mechi zake yeye kama anauza story aendelee watu ni wengi sana asiwe na wasiwasi
Kwa kweli huyu kijana sijui baba kwani tukisoma humu JF yeye anakosa oksigeni. [emoji2][emoji2] Ana mtisha Hadi mleta mada ati
 
Russia ni watu wa vitendo,nami napenda utayari wao na kutofanya mzaa wowote juu ya kitisho cha usalama wa nchi yao.
Japo waliitwa waoga kwa wao kuwa tayari kupiga wakati wowote,mimi nawaita ni watu shapu na wanao tumia mbinu sahihi ya kupiga ngumi moja kwa moja badala ya kupangua pale adui anapo kutishia kurusha yake.Na mbinu hii ndiyo uitwa mbinu za timing.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Safi sana.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Wanasema mwoga anakuwa na defensive mechanisms nyingi sana[emoji28][emoji28] sijui kama ni kweli
 
Yeye kapata Bure why awatoze wengine na hatoi credit Kwa mwandishi na JF au anataka asifiwe ni mjanja[emoji2][emoji2]
Kinachonikwaza ni vile anavyokua mbabe sasa wakati wote wameitoa mahali wakaleta humu
 
Watu wanalipishwa pesa telegram kusoma hizi lazima roho ziwaume!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…