Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Unajua hizi idara zetu pia nafukiria kama zingekuwa zinajiweza kiuchumi zingekuwa independent pia kutekeleza majukumu Yao pasipo kuingiliwa na Hawa wanasiasa . Shida huku kwetu wanasiasa ndio wenye Hela
Wazungu walijua kabisa tulivyo kiufikiri. Wakati wanaondoka wakatuachia siasa mbovu,kiasi kwamba mwanasiasa akiwa madarakani anakuwa kama mungu mtu.

Wanasiasa wamefifisha sana maendeleo ya nchi za Africa kwa maamuzi yao ya kibinafsi.

Ona Gabon. Ona sisi na hiki chama na siasa za kimasikini kwa walio wengi. Ona M7 mpaka anauliza kwa nini mtoto wake asiwe rais.

Lakini hizi idara za ujasusi zingekuwa makini ndizo zenye jukumu la kumuandaa kiongozi mzuri. Kama wanavyofanya urusi. Japo siipendi musimamo ya Urusi na siasa zake za udikteta na ukandamizaji
 
Mimi nasema Oleg ni shujaa wetu mpaka sasa. Kwa lugha ya The bold hapo angekuambia bila mtu mmoja kuiokoa dunia. Mtu huyo ni Oleg kuna uwezekano mkubwa dunia tusingeikuta kama ilivyo sasa.
 
Hii story kuna kitu cha msingi sana imetufundisha nacho ni kwamba West walikuwa smart sana kwenye kuplan UJASUSI wao kuliko East au soviet. Na hichi kitu pekee ndio kilimuokoa huyu Oleg gordievskjy
Ndio walikuwa smart sana na aset zao. Ndio maana Uk pamoja na kumtumia Oleg,tayari walishamgeuza kama ni mtu wao kabisa kuliko alikozaliwa.

Na kwa ufundi wa ujasusi wao tayari walikuwa na backup ya kumchomoa kwa vyovyote vile ukipatwa na tatizo. Kumuokoa ikiwemo na kuhatarisha maisha yao kuja kukunyang'anya kijasusi,hata jera au hata mikononi mwa wetesi wako. Na ndio maana umesema mpaka sasa yuko huru anamalizia Uhuru wake kwa kazi kubwa aliyoifanyia dunia kwa ujumla. Na kuna uwezekano mpaka sasa analindwa ama anaishi sehemu ya siri sana.

Tofauti na Soviet ilikuwa wanakutumia kama takatata kwa manufaa ya muda huo huo. Ukidakwa wanakaa pembeni bila kujishughurisha na lolote,hasa ukizingatia wewe sio raia wao. Ndio maana Ames yuko jera mpaka sasa. Hapo anategemea huruma ya USA tena. Urusi tayari wameshamsahau pamoja na kuwapa zaidi ya 4000.

( Urusi ndio maana mpaka sasa wana ubinafsi wa kiafrica),hata siasa zao mpaka sasa ni za kikandamizaji kama Africa tu. Ndio maana mpaka sasa Africa ni halali wamkumbatie Putin ksbb Putin haangalii siasa za ndani ya nchi husika kuisapot. Hata kama hiyo nchi inakiuka kwa kiasi kikubwa haki za binadamu,yeye anaangalia maslahi yake tu bila aibu. Sawa na wachina kwa Africa,wanaangalia maslahi yao tu.
 
Hata Urusi kuna aliowapa makaz na anawalinda kinomanoma km Snowden na wengineo
 
Huyu mwamba Oleg japo watu wanamuona snich. Lakini mimi kwa jicho la 3 namuona shujaaa wa dunia. Usariti wake ulikuwa na maana sana. Kuna uwezekano mpaka sasa dunia isingekuwa hivi ilivyo. Huyu mwamba alisaidia sana kufanya visitokee vita vya nuclear
Akusikie cariha unamuita oleg shujaa 😀😀
 
Kusema kweli mimi huo ushujaa wa Oleg siuoni hapo,ila kwa kuwa ni west wamefanya inataka kuonekana kwamba imefanyika kwa maslahi mapana ya dunia ili kumuondolea sifa ya usaliti kisa wamenufaika naye. Katika story inaonyesha Russia walikuwa wanahisi USA/UK wanataka kufanya mashambulizi ya makombora na wao wakawa wametuma mashushu wao kuhakiki taarifa hizo na sio kwamba walikuwa na lengo la kushambulia bila kuwa na taarifa za uhakika za wapinzani.
Ukianza kuangalia hata taarifa alizokuwa anazitoa zilikuwa hazielekea kusaidia dunia bali kusaidia USA/UK kuufahamu udhaifu wa Rusia. Na kitendo cha kuendelea kukomalia kuwa naye ni kwa maslahi yao na wala sio usalama wa Oleg,ilimradi walijua jamaa anajua mengi kuhusu Russia na si vinginevyo.
 
Mzee membe marehem nae eti ni kachero...
 
Sijaona sababu za msingi za Oleg kuwa msaliti ... Ukizingatia amezaliwa katika familia ya kishushushu ambao ni mambo super mda wote ...
Msaliti tuu mwamba
 
Umefikiria mbali wamempamba Oleg kuliko uwezo pia waonekane wao intelligence ya ni hatari mara oo Oleg kasave Dunia na vita ya nyuklia mara kile tu kumpa sifa kuliko uhalisia.
Jasusi hatari ni yule aliyeokoa nchi ya Israel huyo ndio alikuwa hatari mno
 
[emoji28][emoji28] halo kumbe usaliti ni ushujaa, at least Oleg was smart kiasi maua yake apewe
Umeona-eeh?. Hatimae umemuelewa eeh?. Ukimfuatilia vizuri kwa umakini utagundua kuna muda dunia nzima ilimtegemea yeye kusave mambo fulani makubwa yasitokee bila kujua
 
Umeona-eeh?. Hatimae umemuelewa eeh?. Ukimfuatilia vizuri kwa umakini utagundua kuna muda dunia nzima ilimtegemea yeye kusave mambo fulani makubwa yasitokee bila kujua
Ila western Huwa Wana propaganda kuliko uhalisia ili waonekane Bora. Wako vizuri kwenye promo pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…