Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Unajua hizi idara zetu pia nafukiria kama zingekuwa zinajiweza kiuchumi zingekuwa independent pia kutekeleza majukumu Yao pasipo kuingiliwa na Hawa wanasiasa . Shida huku kwetu wanasiasa ndio wenye Hela
Wazungu walijua kabisa tulivyo kiufikiri. Wakati wanaondoka wakatuachia siasa mbovu,kiasi kwamba mwanasiasa akiwa madarakani anakuwa kama mungu mtu.

Wanasiasa wamefifisha sana maendeleo ya nchi za Africa kwa maamuzi yao ya kibinafsi.

Ona Gabon. Ona sisi na hiki chama na siasa za kimasikini kwa walio wengi. Ona M7 mpaka anauliza kwa nini mtoto wake asiwe rais.

Lakini hizi idara za ujasusi zingekuwa makini ndizo zenye jukumu la kumuandaa kiongozi mzuri. Kama wanavyofanya urusi. Japo siipendi musimamo ya Urusi na siasa zake za udikteta na ukandamizaji
 
Wewe n mwanamke lazima utamtetea Ames.
Ames ni Kama Samson aliyechangamka kuuza Siri za nchi kisa mwanamke.

Oleg alikuwa anachukizwa na madhira ya ujamaa katika nchi yake.
Lakini pia,alikuwa anataka kulipa kisasa kwa madhira waliyopata wazazi wake hususani mama yake.

Mwisho kabisa, ujasusi wa Oleg ulikuwa na manufaa kwa dunia ,maana uliiokoa dunia katika Vita Kali ya ki nuclear.

Sasa tuje kwa Ames yeye hakuwa na impact yoyote ile.
Mimi nasema Oleg ni shujaa wetu mpaka sasa. Kwa lugha ya The bold hapo angekuambia bila mtu mmoja kuiokoa dunia. Mtu huyo ni Oleg kuna uwezekano mkubwa dunia tusingeikuta kama ilivyo sasa.
 
Hii story kuna kitu cha msingi sana imetufundisha nacho ni kwamba West walikuwa smart sana kwenye kuplan UJASUSI wao kuliko East au soviet. Na hichi kitu pekee ndio kilimuokoa huyu Oleg gordievskjy
Ndio walikuwa smart sana na aset zao. Ndio maana Uk pamoja na kumtumia Oleg,tayari walishamgeuza kama ni mtu wao kabisa kuliko alikozaliwa.

Na kwa ufundi wa ujasusi wao tayari walikuwa na backup ya kumchomoa kwa vyovyote vile ukipatwa na tatizo. Kumuokoa ikiwemo na kuhatarisha maisha yao kuja kukunyang'anya kijasusi,hata jera au hata mikononi mwa wetesi wako. Na ndio maana umesema mpaka sasa yuko huru anamalizia Uhuru wake kwa kazi kubwa aliyoifanyia dunia kwa ujumla. Na kuna uwezekano mpaka sasa analindwa ama anaishi sehemu ya siri sana.

Tofauti na Soviet ilikuwa wanakutumia kama takatata kwa manufaa ya muda huo huo. Ukidakwa wanakaa pembeni bila kujishughurisha na lolote,hasa ukizingatia wewe sio raia wao. Ndio maana Ames yuko jera mpaka sasa. Hapo anategemea huruma ya USA tena. Urusi tayari wameshamsahau pamoja na kuwapa zaidi ya 4000.

( Urusi ndio maana mpaka sasa wana ubinafsi wa kiafrica),hata siasa zao mpaka sasa ni za kikandamizaji kama Africa tu. Ndio maana mpaka sasa Africa ni halali wamkumbatie Putin ksbb Putin haangalii siasa za ndani ya nchi husika kuisapot. Hata kama hiyo nchi inakiuka kwa kiasi kikubwa haki za binadamu,yeye anaangalia maslahi yake tu bila aibu. Sawa na wachina kwa Africa,wanaangalia maslahi yao tu.
 
Ndio walikuwa smart sana na aset zao. Ndio maana Uk pamoja na kumtumia Oleg,tayari walishamgeuza kama ni mtu wao kabisa kuliko alikozaliwa.

Na kwa ufundi wa ujasusi wao tayari walikuwa na backup ya kumchomoa kwa vyovyote vile ukipatwa na tatizo. Kumuokoa ikiwemo na kuhatarisha maisha yao kuja kukunyang'anya kijasusi,hata jera au hata mikononi mwa wetesi wako. Na ndio maana umesema mpaka sasa yuko huru anamalizia Uhuru wake kwa kazi kubwa aliyoifanyia dunia kwa ujumla. Na kuna uwezekano mpaka sasa analindwa ama anaishi sehemu ya siri sana.

Tofauti na Soviet ilikuwa wanakutumia kama takatata kwa manufaa ya muda huo huo. Ukidakwa wanakaa pembeni bila kujishughurisha na lolote,hasa ukizingatia wewe sio raia wao. Ndio maana Ames yuko jera mpaka sasa. Hapo anategemea huruma ya USA tena. Urusi tayari wameshamsahau pamoja na kuwapa zaidi ya 4000.

( Urusi ndio maana mpaka sasa wana ubinafsi wa kiafrica),hata siasa zao mpaka sasa ni za kikandamizaji kama Africa tu. Ndio maana mpaka sasa Africa ni halali wamkumbatie Putin ksbb Putin haangalii siasa za ndani ya nchi husika kuisapot. Hata kama hiyo nchi inakiuka kwa kiasi kikubwa haki za binadamu,yeye anaangalia maslahi yake tu bila aibu. Sawa na wachina kwa Africa,wanaangalia maslahi yao tu.
Hata Urusi kuna aliowapa makaz na anawalinda kinomanoma km Snowden na wengineo
 
Huyu mwamba Oleg japo watu wanamuona snich. Lakini mimi kwa jicho la 3 namuona shujaaa wa dunia. Usariti wake ulikuwa na maana sana. Kuna uwezekano mpaka sasa dunia isingekuwa hivi ilivyo. Huyu mwamba alisaidia sana kufanya visitokee vita vya nuclear
Akusikie cariha unamuita oleg shujaa 😀😀
 
Kusema kweli mimi huo ushujaa wa Oleg siuoni hapo,ila kwa kuwa ni west wamefanya inataka kuonekana kwamba imefanyika kwa maslahi mapana ya dunia ili kumuondolea sifa ya usaliti kisa wamenufaika naye. Katika story inaonyesha Russia walikuwa wanahisi USA/UK wanataka kufanya mashambulizi ya makombora na wao wakawa wametuma mashushu wao kuhakiki taarifa hizo na sio kwamba walikuwa na lengo la kushambulia bila kuwa na taarifa za uhakika za wapinzani.
Ukianza kuangalia hata taarifa alizokuwa anazitoa zilikuwa hazielekea kusaidia dunia bali kusaidia USA/UK kuufahamu udhaifu wa Rusia. Na kitendo cha kuendelea kukomalia kuwa naye ni kwa maslahi yao na wala sio usalama wa Oleg,ilimradi walijua jamaa anajua mengi kuhusu Russia na si vinginevyo.
 
Kesi ya Sergei skripal

Tangu zamani za mwanafalsafa sun tzu , Ili uweze kushinda vita dhidi ya mpinzani wako ,ilipaswa kupata taarifa za Siri kumhusu huyo mpinzani. Taarifa hizi muda mwingine zinaweza kukupa insight kuhusiana na madhaifu ya mpinzani wako . Na kikawaida ukishajua madhaifu ya mpinzani wako basi utatumia udhahifu huo huo kumpiga na kumshinda . Hivyo hivyo kwa nchi mahasimu hufanya hivi katika kukusanya taarifa hizo za Siri. Ndipo linapokuja neno UJASUSI. Hivyo nchi huamua kutuma au kupandikiza watu maalumu kwa nchi Fulani Ili iweze kukusanya taarifa hizo za kijasusi lakini maisha Yao Huwa hatarini .

Tukija kwenye level ya kitaifa . Nchi huamua kukusanya taarifa za kijasusi dhidi ya nchi nyingine ,Ili kuweza kujua mipango yake na mikakati yake kwa lengo binafsi la nchi husika Ili iweze kujilinda na pia kunufaika kimaslahi.
Wakati wa vita baridi baina ya USA na USSR , nchi hizi zilikuwa zinajikita Zaidi katika kupata taarifa za siri dhidi ya mwenzake kutokana na shinikizo lililotokana na tishio la kutokea vita ya nyuklia. Hii ilianza punde tu baada ya kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia .
Nchi hizi ziliamua kutumia mbinu mbalimbali walizoona Zinafaa katika kupata taarifa za kijasusi dhidi ya mwenzake . Mamlaka za serikali hususani bunge hutunga sheria Kwa ajili ya kuzipa ithibati organization za kijasusi Ili kukusanya taarifa hizo Kwa maslahi ya nchi au muda mwingine Kwa maslahi binafsi ya wanasiasa. Nchi ya uingereza kwa mfano ilianza hizi harakati za kukusanya taarifa za kijasusi au kiintelijensia kupitia shirika lake la kipindi hicho lililoitwa SIS Baadaye ikaitwa M16 tokea mwaka 1909. Lengo kuu lilikuwa kukusanya taarifa ambazo zingeisaidia kupunguza uwezekano wa nchi ya ujerumani kuvamia nchi za magharibi hususani washirika wa uingereza kijeshi. Vilevile USA iliamua kuanzisha harakati za ukusanyaji wa taarifa za kijasusi rasmi punde tu ilipoisha vita ya pili ya dunia . Kwa mfano bunge la congress wakati huo lilipitisha National security Act ya mwaka 1947 . Na sheria hii ilipopita likazaliwa shirika la kijasusi la CIA. Na pia Soviet waliunda shirika lao ukusanyaji taarifa za kijasusi lililoitwa Cheka punde tu baada ya mapinduzi ya mwaka 1917 ulioondoa utawala wa Czar. Mbali na hizi taasisi zilizoundwa kisheria katika kukusanya taarifa za kijasusi , ni kwamba muda mwingine hutumika kufanya mauaji kwa baadhi ya walengwa fulani fulani ambao huonekana ni tishio katika ulimwengu wa kijasusi au kwa nchi husika.
Walengwa Hawa Huwa ni waasi au double agent. Ni kwamba mtu huamua kuwa double agent kutokana na sababu fulani fulani ambazo muda mwingine huwa ni tamaa binafsi , shinikizo au mapenzi binafsi .....
Katika hili swala la uasi tunamwangalia bwana mmoja aliyeitwa Sergei skripal . Huyu alipewa sumu ambavo inasemekana ingepaswa kumuua taratibu yeye pamoja na bintiye anayeitwa Yulia kutokana na uasi .
Huyu Sergei skripal ni nani haswa?
Huyu bwana alizaliwa tarehe 23 June mwaka 1951 huko Soviet maeneo ya bahari ya Baltic . Alianza kuifanyia kazi shirika la kijasusi la jeshi la Russia lililoitwa GRU. Katika kutekeleza majukumu yake alitumwa kufanya kazi kwenye nchi ya Malta na baadaye uhispania. Lakini inasemekana kipindi cha utawala wa Boris Yeltsin , majasusi waliokuwa wanatumwa kufanya kazi za kijasusi nchi za nje hawakuwa wanapewa mkwanja kwa kipindi kirefu wakiwa Wanawajibika nje ya nchi . Huyu bwana akaamua kujiongeza na kutafuta fursa za kiuchumi ambazo zingemwezesha kuishi maisha aliyoyataka. Katika kutafuta fursa alijikuta anakutana na afisa mmoja wa M16 na akajitambulisha kama agent wa GRU. Sasa rasmi hapo akaamua kuwa double agent akiitumikia GRU shirika lililomwajiri na pia kuitumikia M16 ya uingereza kwa Siri kwa ajili ya kupata pesa . Kwa kifupi alikuwa anauza taarifa za nchi yake kwa nchi hasimu ya uingereza Alipewa jina la uficho la FORTWITH akiuza taarifa za kijasusi zenye thamani kubwa kwa uingereza. Lakini mwaka 2000 alijikuta Na changmoto ya afya hivyo ikamlazimu kurudi Russia kwa ajili ya matibabu na akakutwa na kisukari . Ilimlazimu kujiuzulu kama afisa wa GRU na kuamua kufanya kwenye ofisi ya serikali hususan kwenye maswala ya kiutawala lakini Shughuli za kijasusi aliendelea nazo kama kawaida. Na vilevile alikuwa bado yupo kwenye payroll ya M16 akipokea mkwanja kama kawaida . Lakini mwaka 2004 shirika la kijasusi la Russia la FSB lilimtimua kutokana na tuhuma dhidi yake za kuwa double agent na mwaka 2006 alikutwa na hatia mahakama ya kijeshi na kupigwa mvua ya miaka 13. Tuhuma dhidi yake ni kwamba alikuwa anawapa taarifa M16. Lakini kupitia msaada wa serikali ya marekani huyu bwana alisamehewa kupitia makubaliano maalumu ya kubadilishana wafungwa baina ya U.S.A na Russia na huyu bwana aliamua kwenda kuishi nchini uingereza kwenye mji mdogo wa Salisbury.
Huyu bwana aliamua kununua nyumba huko Salisbury na kuamua kuhamia yeye na mkewe liudmila pamoja na wanao wawili mwaka 2011.
Lakini ajabu ni kwamba mwaka 2012 alimpoteza mkewe na mwaka 2017 mwanae wa kiume Alexander nae alifariki. Aliyebaki ni mwanae wa kike ambaye Alikuwa anakuja kumtembelea mshua wake Mara kwa mara akitokea Russia. Kutokana na vifo vya wanafamilia Hawa WA kwake , aliamua kuishi maisha ya kawaida tu akiwa na paka wake mmoja kwa ajili ya kuondokana na upweke .
Mwaka 2018, mwaka mmoja tu tokea kifo Cha kijana wake huyu bwana skripal akiwa na bintiye walikutwa hawajitambui wamepoteza fahamu eneo la hifadhi la Salisbury Park. Ripoti za kiuchunguzi za awali kutoka vyombo vya usalama na habari zilitabanaisha na kusema shambulio Hilo lilikuwa ni jaribio ya mauaji dhidi ya huyu bwana na huenda pia hata mkewe na mwanae ilikuwa ni mauaji ya kupanga. Baada ya kupelekwa hospitali , bwana skripal na mwanae walikuwa hawajitambui kwa wiki kadhaa pasipo kujulikana sababu ni Nini zilizopelekea Hali hiyo kwa mujibu wa ripoti za kitabibu. Lakini baada ya kupata nafuu waliruhusiwa kutoka hospitali tarehe 9 April 2018. Kutokana na huyu bwana kuwa na hadhi yake , mamlaka za serikali ya uingereza ziliamua kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hili . Taarifa zilitoka na kudhibitisha bwana huyu na bintiye walipewa sumu iliyoitwa nerve agent ambayo pia baadaye Theresa May waziri mkuu wa uingereza wakati huo aliithibitisha bungeni kuwa ni sumu aina ya Novichok (A-234) .
The organization for the Prohibition of chemical weapons (OCPW) ni Taasisi iliyokuwa inahusika na udhibiti wa matumizi ya silaha za kemikali ziliamua kufanyia kazi hili swala na kutaka kujua chanzo Cha hii sumu ilifikaje hapo uingereza. Kupitia maabara ya
Defence science and technology laboratory(DSTL) sample zilichukukuliwa na ripoti ikathibitisha ni sumu ya Novichok with high purity na ilikuwa kwa wingi eneo la mlangoni kwenye nyumba ya skripal.
Kwa mujibu wa mshauri wa maswala ya ya kiusalama ya kitaifa bwana mark sedwil alisema kwamba kupitia uchunguzi uliofanywa na DSTL ,sumu hii ilikuwa kwa wingi kwenye eneo la kitasa Cha mlango wa mbele wa nyumba ya skripal. Na sumu hii ilikuwa katika Hali ya umajimaji . Hivyo huyu bwana akasema sumu hii hutumiwa na Russia na hivyo wao wanahusika Moja kwa Moja na tukio la majaribio la kumuua bwana skripal. Lakini kama kawaida Russia wakakanusha madai haya na kusema ni propaganda dhidi yao ya kutaka kuzorotesha mahusiano ya kidiplomasia.
Ripoti Zaidi kuhusiana na hili tukio la jaribio la mauaji dhidi ya skripal ilisema kwamba hata eneo walilokuwa skripal na bintiye mara ya mwisho kabla ya kukutwa na hii dhahama kulikuwa na kiwango kikubwa Cha sumu hii. Hivyo Ili kuzuia watu kuwa exposed na hii sumu serikali iliamua kuizingira nyumba hiyo na viwanja vya karibu na eneo Hilo kwa utepe wa crime scene Ili kufanya uchunguzi zaidi. Shirika la bbc lilisema serikali ilituma maafisa 250 wa kitengo Cha kupambana na ugaidi na maafisa wa kijeshi 180 katika kulizingira eneo Hilo kwa ajili ya uchunguzi wa kina.
Maafisa uchunguzi walianza kuchunguza kuanzia nyumba ya skripal,gari yake maeneo walikopita, mgahawa walioenda kula, Hadi kwenye benchi walikokuwa wamekaa na kukutwa wamepoteza fahamu akiwa bintiye.
Kulikuwa na mkanganyiko kuhusiana na chanzo Cha hii sumu ilikotoka mpaka kufika uingereza. Kwa mfano vyombo vya habari vilisema huenda sumu hii ilichanganywa kwenye baadhi ya vitu vya Yulia skripal alivyoondoka navyo Moscow kuja uingereza. Taarifa za vyombo vya habari vya U.S vikadai huenda sumu hii iliwekwa kwa Siri kwenye gari ya skripal.
Lakini kwa mujibu ya mwanahistoria katika maswala ya kiintelijensia anayeitwa Boris volodarsky alisema kupitia chapisho lake la mtandaoni la "the poison war"
Kwamba huenda sumu hii ilifika eneo Hilo alilokuwa akiishi skripal kupitia technical timu ya majasusi na kufanya Yao huku mlengwa akiwa ni skripal.
Hivyo serikali ya uingereza ikafanya jitihada zote za kujua walengwa waliofanya hili tukio ni kina nani .
Na kweli mamlaka za shirika la kijasusi la uingereza likiwasuspect Raia wawili wa Russia ambao ni Alexander Petrov na Ruslan boshirov ambao pia walihusishwa kuwa ni maagent wa GRU. Walituhumiwa katika kufanya jaribio la mauaji dhidi ya skripal. Kwa mujibu wa ripoti za kiutafiti kuhusiana na hili swala huyu Alexander Petrov jina lake halisi alitambulika kama Alexander mishkin ambaye alikuwa ni daktari na Ruslan boshirov alitambulika rasmi kama kanali Anatoliy chepiga na wote walikuwa wanafanyia Kazi shirika la kijasusi la Russia tokea 2010. Kwa mujibu wa ushahidi uliopatikana nchini uingereza inasemekana huyu Chepiga alikuwa akijihusisha na operesheni za Siri muda mrefu na inawezekana yeye ndio aliyefanya tukio hili la kujaribu kutaka kumuua huyu skripal kwa sumu ya Novichok. Na inasemwa operesheni hii ilitolewa order kutoka kwenye mamlaka ya juu kabisa ya Russia.kremlin office.
Mamlaka za uingereza zilituma ombi la kuwakamata watu hawa na kuletwa uingereza kwa ajili ya kuja kujibu tuhuma dhidi yao. Na ilisema tukio hili ni kinyume na UN charter kutokana na matumizi ya nguvu kudhuru na ilitaka majibu ya kisheria kutokana na tukio hili kutoka kwa Russia.
Russia kama kawaida Yao wakakaza.
Sumu hii ya Novichok kwa mujibu wa ripoti za OCPW inasemwa ni miongoni mwa sumu zilizokuwa zinatengenezwa huko Russia miaka ya 1980s kipindi hicho Cha vita baridi. Na inasemekana ni sumu inayoathiri mfumo wa ufahamu mwilini na huweza kupenya kupitia ngozi . Na ikianza kufanya reaction mwilini inapelekea mfumo wa upumuaji kushindwa kufanya kazi na kupelekea kupoteza fahamu.
Sumu hii mara ya kwanza ilianza kutengenezwa huko ujerumani kipindi cha vita ya pili ya dunia, baadaye Russia ikachukua formula yake na kuanza kuitengeneza miaka hiyo ya 1980.
Bwana skripal na bintiye baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ,Sasa wanahifadhiwa kwa Siri kwenye eneo mojawapo ndani ya uingereza chini ya ulinzi mkali japo bado maisha Yao yapo hatarini.
Kutokana na Russia kukataa kuwakabidhi washukiwa kwenye mamlaka za uingereza kwa ajili ya kujibu tuhuma, serikali ya nchi hiyo pamoja na U.S iliamua kuwatimua maafisa wa Russia kwenye nchi hizo kutokana na hili sakata. Huku Russia iliendelea kukanusha.

Tukirudi nyuma kutokana na hili swala la ukusanyaji taarifa za kijasusi kwa nchi Moja dhidi ya nyingine , ni kwamba Hawa maagent wanaoenda field hukutana na dhahama nyingi sana ikiwemo kuuliwa .
Kwa mfano skripal , changamoto yake ya kukosa pesa akiwa field katika kukusanya taarifa za kijasusi kwa ajili ya nchi yake , ikabidi kuuza taarifa kwa nchi hasimu . Ilimgharimu uhai wa Memba wa familia yake na yeye almanusura kuuliwa .
Hivyo naweza kusema maagent huhatarisha maisha Yao pamoja na wale wapendwa wao kwa maslahi ya usalama wa nchi, na vilevile maslahi ya WANASIASA waliopo madarakani.



View attachment 2616819
Sergei na bintiye Yulia skripal




View attachment 2616825
Watuhumiwa wanaoshutumiwa kwenye mpango wa kumuua bwana Sergei na bintiye Yulia kwa sumu ya Novichok


UJASUSI SIO KAZI YA KILA MTU KUWEZA KUIFANYA , LINAPOKUJA SWALA LA MASLAHI YA TAIFA


Credit : google
Mzee membe marehem nae eti ni kachero...
 
Sijaona sababu za msingi za Oleg kuwa msaliti ... Ukizingatia amezaliwa katika familia ya kishushushu ambao ni mambo super mda wote ...
Msaliti tuu mwamba
 
Kusema kweli mimi huo ushujaa wa Oleg siuoni hapo,ila kwa kuwa ni west wamefanya inataka kuonekana kwamba imefanyika kwa maslahi mapana ya dunia ili kumuondolea sifa ya usaliti kisa wamenufaika naye. Katika story inaonyesha Russia walikuwa wanahisi USA/UK wanataka kufanya mashambulizi ya makombora na wao wakawa wametuma mashushu wao kuhakiki taarifa hizo na sio kwamba walikuwa na lengo la kushambulia bila kuwa na taarifa za uhakika za wapinzani.
Ukianza kuangalia hata taarifa alizokuwa anazitoa zilikuwa hazielekea kusaidia dunia bali kusaidia USA/UK kuufahamu udhaifu wa Rusia. Na kitendo cha kuendelea kukomalia kuwa naye ni kwa maslahi yao na wala sio usalama wa Oleg,ilimradi walijua jamaa anajua mengi kuhusu Russia na si vinginevyo.
Umefikiria mbali wamempamba Oleg kuliko uwezo pia waonekane wao intelligence ya ni hatari mara oo Oleg kasave Dunia na vita ya nyuklia mara kile tu kumpa sifa kuliko uhalisia.
Jasusi hatari ni yule aliyeokoa nchi ya Israel huyo ndio alikuwa hatari mno
 
[emoji28][emoji28] halo kumbe usaliti ni ushujaa, at least Oleg was smart kiasi maua yake apewe
Umeona-eeh?. Hatimae umemuelewa eeh?. Ukimfuatilia vizuri kwa umakini utagundua kuna muda dunia nzima ilimtegemea yeye kusave mambo fulani makubwa yasitokee bila kujua
 
Umeona-eeh?. Hatimae umemuelewa eeh?. Ukimfuatilia vizuri kwa umakini utagundua kuna muda dunia nzima ilimtegemea yeye kusave mambo fulani makubwa yasitokee bila kujua
Ila western Huwa Wana propaganda kuliko uhalisia ili waonekane Bora. Wako vizuri kwenye promo pia
 
Back
Top Bottom