30
Tulipoishia part one ndio tunaanzia hapa..............,,............[emoji3578][emoji3578][emoji3578]
Ndani ya Moscow baada ya Oleg kufika mbele ya mlango wa nyumba yake na kubaini kitasa Cha Tatu kipo locked hakutaka kuamini kabisa labda alisahau kufunga vitasa vyote. Ni dhahiri alikuwa na uhakika hakufunga kitasa hiki Cha Tatu na hakuwahi kuwa na ufunguo wake. Kwa kuwa naye ni jasusi mbobevu anayejua medani za kijasusi rasmi Sasa akajua KGB wanamfuatilia. Kijasho chembamba kilimtoka, aliamini muda wowote atakuwa mfu. Na adhabu ya msaliti aliijua . Ni kwamba atatiwa ndani ,Kisha atahojiwa kwa mbinu zote na ateme data za kila aina alizonazo ,na mwisho ni BULLET IN THE HEAD na mwisho kuzikwa kama mbwa na kaburi lake lisikae lijulikane kamwe. Mawazo haya yote yalimfanya agande kifikra kwa sekunde kadhaa.
Akiwa kwenye Lindi la mawazo akazidi kutafakari endapo KGB walikuwa wanajua mambo yake yote ya Siri ni kwamba wasingemruhusu muda huo aweze kufika Hadi mlango wa nyumba yake. Angekamatwa kulekule airport na Moja kwa Moja angepelekwa kwenye torture chamber zilizoko kwenye basement ya jengo la lubyanka makao makuu ya KGB. Mpaka hapo alijua ashashtukiwa ila walikuwa hawana ushahidi wa kutosha kumtia hatiani. Kwa cheo Cha ukanali alichokuwa nacho Oleg wakati huo , sio rahisi kumtuhumu juu juu tu na tuhuma za usaliti ilihitajika jitihada zaidi za kumtia hatiani na pia hata kama akitiwa hatiani kulikuwa na utaratibu KGB wa kuwapa mateso makali maafisa (torturing) wenye vyeo vya ukanali. Kumnasa msaliti au spy kulikuwa na hatua kadhaa zilipaswa kuzingatiwa. Kumwangalia kwa ukaribu suspect, kumsikiliza kila jambo huyu suspect na mwisho kumsubiri ajae kwenye 18 na afanye mistake Moja tu Ili kumnasa red handed . Hili bwana Budanov aliyekuwa anamtilia mashaka Oleg alilizingatia. Advantage kubwa aliyokuwa nayo Oleg ni kwamba alikuwa anajua anafuatiliwa na majasusi wenzake....
Muda huu wote akiwa anatafakari , alikuwa bado mbele ya mlango na alihitaji kuingia ndani kipengele kikawa kitasa Cha Tatu funguo zake Hana. Hapo hapo akaenda jirani kwenye nyumba ya afisa mwenzake ambaye alikuwa ni mtaalamu wa vyuma vyuma ,na kweli akamsaidia kufungua mlango ule na mwamba akazama ndani. Hii nyumba ya Oleg tayari ilishafanyiwa upekuzi na kupandikizwa vinasa sauti na kamera za Siri kila Kona ya chumba. Baada ya kujua Hilo akawa mpole hakutaka kuonyesha ku panick maana aliona akipaniki na nyumba hiyo alihisi tayari Kuna camera za Siri basi watakuwa wanamwona jinsi anavyofanya hapo ndani muda huo. Kwa haraka haraka nyumba hiyo unaweza sema hakukuwahi kuingia mtu kutokana na vitu kuwa in placed kama vilivyoachwa . Lakini kwa Oleg alijua tu hapa kulikuwa na kikosi Cha majasusi walifika ,wakafanya Yao Kisha wakasepa.
Usiku huo bwana Oleg hakulala sana kutokana na mawazo mengi yakimwandama na swali likiwa NI NANI ALIYENISALITI , na KGB WANAJUA NINI KUMHUSU?.[emoji28][emoji28][emoji28]
Kesho yake aliamka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda makao makuu ya KGB. Na kweli alipofika alikutana na bwana Nikolai Gribin . Na gribin afisa mwenzake akamwambia kuna mahojiano na wakuu wa KGB hivyo ajipange .alimwambia hayo maneno kiutani utani.. lakini katikati ya utani Kuna ukweli mchungu nyuma yake......
Na kweli baada ya kama lisaa hivi bwana Oleg aliitwa kwenye ofisi ya deputy wa idara ya FCD bwana Victor Grushko.....