Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Kwa mujibu wa maoni binafsi ya mwandishi wa hii ishu ya Oleg Bwana Ben macintyre, Ni kwamba kile kitendo Cha kuitwa Hadi kupata mwaliko ikulu ya white house kwa Ronald Reagan lilikuwa ni Kama tusi la nguoni kwa KGB na mbaya zaidi alipewa medani ya heshima ya juu na malkia Elizabeth...
 
SEHEMU YA SITA

Kama afisa yoyote wa KGB ,bwana Oleg alikata shauri na kuamua kuoa licha ya kazi iliyokuwa na majukumu mazito na hatarishi. Alimuoa Yelena Akopian mwanadada aliyekuwa na umri wa miaka 21 , mwalimu wa lugha ya kijerumani. Alikuwa ni nusu mwa Armenia na nusu mrusi na walikutana na oleg kwenye harakati za majukumu ya kazi za ujasusi. Kama tu Oleg, mwanadada huyu alikuwa anapenda maisha ya umagharibi na alikuwa ni wale akina dada wenye itikadi za ufeministi.
Kuoa kwa afisa wa KGB kwa wakati huo ilikuwa pia ni kigezo Cha kupanda ngazi ya cheo. Na ndivyo ilivyokuwa.
Baada ya kufunga ndoa ,mwishoni mwa mwaka 1965 ilikuwa ni siku iliyosubiriwa kwa hamu kubwa . Ilitoka post ya kufanya kazi ya ubalozini nchini Denmark. Ilitarajiwa kazi official ilikuwa ni ku deal na visa na pasi za kusafiria,usajili wa ndoa ,na kazi zingine official kama afisa wa ubalozini . lakini kazi yake Hiyo ilikuwa ni Kama cover kwa juu , majukumu yake kama JASUSI ilikuwa ni kupandikiza majasusi ndani ya nchi ya Denmark,kupokea infos,kutoa fund kwa majasusi na vilevile kuajiri na ku register majasusi. Kwa kifupi alikuwa na majukumu ya kusimamia shughuli zote za ujasusi nchini Denmark.
January 1966 majira ya kuanguka kwa barafu ndio siku bwana Oleg na mkewe Yelena walitua ndani ya Copenhagen. Kwao Jiji Hilo waliona kama wameingia kwenye ulimwengu wa kubuni wa fairy tales. Kwa kifupi Copenhagen lilikuwa ni Jiji safi, la kisasa na la kitajiri. Waliona kama wameingia mbingu nyingine ukilinganisha na Jiji lao la nyumbani la Moscow. Vilabu, maduka ya pombe,vyakula vya kila aina,bendi za miziki,maktaba na bustani za maua ya kila rangi yaliwavutia . Na ni Jiji ambalo everyone minds his/her own business . Na likiwa na polisi wachache mitaani na visa vichache vya uhalifu.
Walifika kituo chao Cha kazi . Ubalozi wa Soviet ndani ya Copenhagen kilichokuwa chini ya mwakilishi /ambassador Leonid yetsev ulikuwa kwenye kitongoji Cha kristianiagade kaskazini mwa Jiji .ilikuwa ni jengo la kisasa lenye bustani za kuvutia,kwao waliona ni kama villa park au aina ya resort ya kisasa . Sehemu ya uwanja wa michezo pamoja na social club. Aliishi yeye na mkewe kwenye apartment ya kisasa na kukabidhiwa Volkswagen beetle pamoja na euro 250 cash kila mwezi kama advance.
Ndani ya ubalozi huo kulikuwa na wafanyakazi 20 Maafisa sita tu kati ya hao walikuwa ni wanadiplomasia na wafanyakazi wa kawaida ila wote waliobaki walikuwa wanafanya kazi kwa niaba ya KGB,GRU. Yaani walikuwa ni majasusi.
Ndani ya ubalozi huo bwana Leonid yetsev ambaye ndie balozi mwakilishi alikuwa anajua kabisa asilimia kubwa ya wafanyakazi wake hapo walikuwa ni incompetent, hawakuwa serious na kazi na wavivu. Wengi wao walitumia pesa vibaya kulewa,kujirusha na totozi n.k kuliko kuzifanyia shughuli za kijasusi.Lakini kwa bwana Oleg alimuona mfanyakazi anayejituma,mchapakazi na pia alikuwa ni mwelewa wa lugha ya ki danish. Bwana Oleg majukumu yake yalikuwa ni kuprocess visa ,kuandaa nyaraka mbalimbali n.k .ila shughuli ujasusi yeye alianza kuzifanya muda wa lunch.Hii Ina maana kwamba wakati wa chakula siyo rahisi kushtukiwa kwa maana wakati mnakula huku mpo mnapiga stori na marafiki zako mnapeana na kubadilishana infos za kijasusi pasipo kushtukiwa kiurahisi.
Majukumu yake makubwa yalikuwa ni kusimamia mtandao mzima wa majasusi waliotapakaa pasipo pia kukutana nao USO kwa USO ,na pia asiwafahamu sura Wala Majina yao kabisa. Kwa mfano Oleg na majasusi wenzake walikuwa wanawasiliana kwa njia ambazo ni ideal zisizoweza kutambulika kiurahisi. Jasusi anaweza kuacha Ganda la chungwa kwenye Yale mabenchi sehemu za umma akimaanisha nipo hatarini, nafuatiliwa.Au unaweza kukuta mbegu za apple zimeachwa mahali ikiwa na maana jasusi huyo anaondoka nchi hiyo. Kwa mfano bwana Oleg siku Moja aliacha msumari uliokunjwa kwenye dirisha la choo Cha umma ,akiwa na maana jasusi Fulani akiuona akachukue kifurushi cha fedha kilichofichwa kwenye dustbin sehemu Fulani ya mji. Na labda jasusi huyo baada ya kupokea fedha hizo ,Ili kuonyesha amepata mzigo ,angeacha kizibo Cha bia kilichokunjwa kwa meno hapo kwenye dirisha la chooni. Hivyo ndivyo mambo ya kijasusi yalivyokuwa Yana operate.
Kwa kuwa bwana Oleg kazi yake kubwa ilikuwa ni kupandikiza majasusi ndani ya Denmark alihitaji pia kupata access ya registration ya raia wa nchi hiyo.
Ni kwamba nchini Denmark ,rekodi za vizazi na vifo vinasajiliwa na kanisa la kiprotestant la nchini humo . Hivyo Oleg aliamua kufanya forgery ya majina kuingizwa kwa ajili ya kazi za kijasusi. Hivyo alianza urafiki na kuwashawishi makasisi wa kilutheri Ili aweze kuwa na access na daftari la rekodi za usajili la kanisa Hilo. Hivyo alifanikiwa kufoji na kuingizwa kwa majina ya raia wa ki danish ambao kiuhalisia hawakuwahi kuwepo . Hii ni kwa sababu majina hayo angeyatumia kwenye ku process visa na kutengeneza alias hapo ubalozini kwa ajili ya majasusi aliokuwa anawajibika kuwasimamia.
Kiukweli mbali na kuwa mfanyakazi hapo ubalozini ,Oleg alionja ladha halisi ya uhuru wa magharibi. Alipenda miziki,watu wake,na pia zaidi uhuru kwenye swala Zima la mapenzi. Ikumbukwe nchi ya Denmark ndio nchi ya kwanza duniani ku legalize homosexuality miaka ya 1960s. Nchi hii swala la ngono lilikuwa ni kipaumbele kwao kama Huku kwetu kipaumbele ni kutafuta Hela .kwao ngono ilikuwa kama ibada na chakula kwao.
Kwa mfano Siku Moja aliwahi nunua majarida mawili Moja likiwa la mapenzi ya jinsia moja kwenye duka kubwa la bidhaa za ngono, kwa ajili ya kwenda kumuonyesha mkewe. Kiukweli haya mambo yalipigwa marufuku nchini mwao . Ni kwamba Oleg alipata a real taste of liberty.
Lakini wanasema ukiwa ugenini ni ugenini tu.
Shirika la ujasusi la Denmark PET( Politiets Efterretningstjeneste) lilikuwa ni shirika dogo Japo lilikuwa effective na vigilant. Majukumu yake yalikuwa ni Yaleyale kama mashirika mengine ya kijasusi duniani . Walianza kumuweka huyu bwana mdogo kwenye radar zao kufuatilia nyendo zake kimya kimya .
Kutokana na itikadi za kikomunisti ni kwamba wa danish yaani hao PET walikuwa na utaratibu wa mara kwa mara wa kufuatilia nyendo za maafisa wa ubalozi wa urusi.Na pia baadhi ya simu za hapo ubalozini zilikuwa zinasikilizwa kwa Siri kwa kuwa zilikuwa tayari zimefanyiwa bugging. Lakini pia ma technician wa KGB nao walikuwa wamefanikiwa kupenyeza mitambo Yao ya kunasa mawasiliano ya pET. Kwa kifupi kila mmoja alikuwa anamwinda mwenzake bila kujua wanawindana.
Oleg na mkewe walikuwa wanasaidizana kusikiliza mawasiliano ya Siri kutoka kwenye ofisi za PET na kuzi decode na kuzitafsiri Hadi kwenye lugha ya kirusi na kuzituma home.
Kwa kuwa bwana Oleg naye alikuwa tayari alikuwa ameshakuwa suspect na idara ya PET, alipewa jina la uficho Ili asisanuke kama naye yupo kwenye radar za majasusi. Alipewa jina la uncle gormsson. Hili lilikuwa jina la mfalme Harald gormsson mfalme wa Denmark wa Karne ya kumi.
Ni kwamba PET walikuwa na mashaka kiasi kama kweli uncle gormsson au Oleg jasusi wa KGB anayefanya kazi chini ya formal diplomatic cover. Wakaamua kuweka mitego ......
Jioni Moja bwana Oleg na mkewe walipokea mwaliko kuhudhuria kupata chakula Cha jioni kwa rafiki yake mmoja aliyekuwa afisa polisi wa kawaida . Wakiwa wametoka kikosi Cha majasusi wa PET waliingia kwenye apartment Yao na kupandikiza vipaza sauti sehemu mbalimbali ndani ya nyumba hiyo. Lakini kwakuwa jasusi ni jasusi bwana Oleg kabla ya kutoka alitilia mashaka huo mwaliko na akaamua kuchukua tahadhari. Kwenye Mlango wa kutokea nje ya nyumba Yao sehemu ya chini kabisa ya mlango alibonyeza matone kadhaa ya super glue . Yaani tone likawa limeshikana na mlango sehemu ya chini na sakafu. Hii ni kwa majibu ya mafunzo aliyopata SCHOOL 101.Wakati aliporudi alikuta ile glue imeachana .Hivyo akajua ndani kwake Kuna watu waliingia na kufanya Yao. Tangia siku hiyo akawa makini na kila atakachokisema na kuongea na mkewe wakiwa nyumbani.
Wanasema taaluma ya ujasusi ni kama mchezo wa paka na panya ,mchezo wa kuviziana na kuwindana.
Ingawaje maafisa wa KGB walikuwa na uwezo wa kukwepa kufatiliwa(dry -cleaning) na majasusi wa PET ,nao pia PET hawakuwa wachache ku target na kuwafuatilia maafisa wa ubalozi wa urusi hapo Denmark hususan kwa target Yao bwana Oleg.
PET ilikuwa inamfuatilia Oleg Hadi mitaa aliyokuwa anatembelea hususan maduka ya kuuza bidhaa za ngono. Kilichowapa alama ya taa nyekundu ni kwamba inakuwaje kwa afisa wa kiurusi anapendelea kusoma majarida ya mapenzi ya jinsia Moja /gay magazine. Kila nyendo za bwana Oleg zilikuwa noted kwa umakini wa Hali ya juu kwenye file lake. Na kwa mara ya kwanza jina lake lilileta question mark.
Ohooooo
 
SEHEMU YA NANE
Aliporudi nyumbani nyumbani mapema January 19670,alikuta mambo yapo tight kuliko alivyoondoka ,ukandamizaji kwa raia ulizidi. Ukikutwa na bidhaa au Jambo lolote ,iwe ni mavazi,au vitabu vyenye maswala ya west unasekwa ndani. Utawala wa bwana Brezhnev uligubikwa na kila aina ya ubabe,rushwa ,ujuaji n.k. Ni kwamba mpaka raia wakawa wanapelelezana wao kwa wao . Kila uliyekutana naye hakuwa na tabasamu, na ole wako ukutwe una urafiki na raia wa kigeni,lazima ungekuwa suspect na kitengo.Propaganda ndio ilikuwa inapigiwa chapuo ,kuisifu serikali,kuhubiri uzalendo n.k. Bwana Oleg hakuwahi kuona furaha baada ya kurudi kutoka Denmark,kwa kuwa Mambo yalikuwa yako tight kuliko ilivyotarajiwa. Kila mahali uendapo serikali ilikuwa inajua. What a stressful life to be watched for every step you make.
Oleg alirudishwa kwenye idara ile ile ya FCD pale makao makuu ya KGB kufanya paperwork,na kipindi hicho ndoa yake ilikuwa katika Hali mbaya Japo hawakuwahi kukaa chini ku settle all matters Na bibiye Yelena. The feminist woman. [emoji28].
Miaka miwili iliyofuata Japo alipandishwa cheo na malipo yalikuwa mazuri ,ni kwamba hakuhisi utofauti wowote ,achilia mbali kazi aliyoifanya miaka mitatu iliyopita. Hii ni kutokana na mfumo aliokuwa anautumikia pamoja mifarakano ndani ya ndoa yake.
Bwana Oleg kipindi hiki aliamua kujifunza lugha ya kingereza akiamini huenda post itakayokuja huenda akatumwa u.s au Britain au nchi yoyote ya commonwealth. Lakini kwenye ulimwengu wa kijasusi ikiwa umetumwa kufanya ujasusi kwenye nchi nyingine halafu ukahisiwa na kurudishwa nyumbani uwezekano wa kutumwa Tena nje ya nchi yako unakuwa ni mdogo sana. Hii ni kwa sababu ,alikuwa ameshaanza kuhisiwa nyendo zake na idara ya ujasusi ya PET akiwa Denmark kwamba bwana huyu uwezekano wa kuwa jasusi wa KGB ni mkubwa.
Aliamua pia kujifunza kifaransa akiamini huenda post inayofuata ikawa ni Morocco.
Upweke uliendelea kumwandama na kazi kwake hakuiona Ina umuhimu , mahusiano yakizidi kumpa msongo wa mawazo. It was not over . Ngoma ilikuwa bado mbichi.



***************@************

Tukienda Hadi nchini uingereza, kulikuwa Kuna afisa mmoja wa shirika la ujasusi la uingereza kipindi hicho lilijulikana kama secret intelligence service/SIS. Huyu bwana mdogo alikuwa ametokea huko Canada muda mfupi na kurejea home kwenye majukumu ya kitengo. Alikuwa anapitia "personal file" Moja alilokuta ofisni mwake . Na ni kawaida kwa hizi idara za ujasusi kukutana na file mezani la KAZI maalumu unayopaswa kuikamilisha.
Aliitwa Geoffrey guscott. Ni bwana mdogo aliyekulia huko south -east London baba yake akiwa ni wale printers daraja la working -class. Huyu chalii alipata ufadhili na kusoma Dulwich college na Cambridge kujiendeleza zaidi hususan kwenye lugha za kirusi na Czech. Kwenye graduation yake 1961alipata barua ya mwaliko isijulikane ilikotoka,kwamba anatakiwa kufika London. Huko London alikutana na veteran wa kitengo wa SIS(Baadaye ilikuja kutambulika Kama M16). Kwa hiyo rasmi bwana mdogo tokea akawa ameajiriwa na kitengo akiwa na miaka 24 tu.
Mwaka 1965 alitumwa Czechoslovakia kipindi nchi hiyo inafukuta na joto la reformation.
Miaka mitatu akiwa Czechoslovakia alikuwa anamtumia jasusi wa nchi hiyo ya Czech kukusanya infos(Kipindi kile Soviet anaivamia czech )mbalimbali na kuzituma kwa idara yake ya SIS.
Hapa Ili tuelewane ni kwamba jasusi wa CIA kutoka u.s anaweza kuja hapa TZ na kumwajiri jasusi wa TISS kupata infos zote za hapa nchini. ... concept imeeleweka[emoji108][emoji108].money talks[emoji39][emoji39].
Okay huyu bwana guscott alikuwa anamtumia jasusi aliyejulikana kwa jina la uficho la FREED kipindi hicho kupata infos zote kipindi Cha uvamizi wa urusi huko Czech au Prague spring. Hivyo huyu bwana mdogo baada ya maandamano kuzimwa huko Czechoslovakia alirudishwa nyumbani ikawa kazi yake ni kupandikiza majasusi (illegals) nchini humo na nchi zilizopakana na Czechoslovakia kupata infos mbalimbali kuhusu Soviet bloc.
Sasa bwana huyu akiwa hapo ofisni kwake ,file alilokuwa anapitia lilikuwa ni file la taarifa nyeti na nzito za afisa mmoja aliyefukuzwa kwenye idara ya ujasusi ya Czechoslovakia . lilikuwa ni file juu limeandikwa kwa wino mzito DANICEK. Lilikuwa ni jina/codename la taarifa sensitive na classified information za stanislav Kaplan (swahiba wa Oleg). Ambaye ndio huyuhuyu alikuwa anamtumia kukusanya taarifa kipindi akiwa Czech.

Huyu bwana ni kwamba baada tu ya Prague spring alichukua likizo na kwenda Bulgaria.Na huko alitoweka asijulikane alipo. Baadaye akaja kuonekana ufaransa. Akajiunga na idara ya usalama ya ufaransa kwa kuifanyia kazi idara hiyo. Lakini kitengo Cha usalama Cha ufaransa wanauhusiano na MI6. Nao M16 wakapata debrief ya huyu afisa wa Czech ambaye kaamua kushirikiana na idara za ujasusi za magharibi. Na vilevile taarifa za huyu bwana stanislav zikawafikia Hadi CIA mezani kwao . Huyu bwana alitoa ABCD zote kuhusu jinsi idara ya ujasusi ya Czechoslovakia inavyofanya kazi ,kipindi anasoma Moscow alitoa Hadi taarifa za mabest zake aliokuwa nao huko . Wengi aliowataja ambao wako interested kufanyia kazi nchi za magharibi walikuwa ni WA Czech lakini jina Moja tu lilikuwa la ki Russia. Jina la Oleg Gordievsky.
Akaulizwa kutoa details za kutosha kuhusu huyu mwamba . Akazitema kama zilivyo.
Hizi taarifa zote bwana guscott alikuwa anazisoma kwenye file Hilo la DUNICEK.
Ni kwamba Guscott alilifanyia Jina la Oleg Gordievsky cross-reference za kutosha na kugundua kwamba huyu bwana alishawahi fanya kazi huko Copenhagen kama afisa wa ubalozini mwaka 1966. Na kwakuwa MI6 na PET wanauhusiano wa kikazi ,alipitia pia ma file ya idara ya usalama ya PET akaja kugundua alikuwa anahisiwa na kutiliwa mashaka huenda ni kachero wa KGB na idara hiyo. Pia akapata kufahamu akiwa huko alikuwa na urafiki na baadhi ya maaskari na Wachungaji wa ki lutheran na pia ndoa yake Ina Mgogoro. Mpaka taarifa zake za kurudi kwake nyumbani huko Moscow.
Baada ya hapo bwana guscott akaamua ku note hili jina pembeni na kulifungulia file lake special na kupewa jina la SUNBEAM. /Person of interest .
Person of interest
 
12.

Kwenye dunia ya manjagu ,pale majasusi wanapotaka kukutana ,Huwa Kuna mind games zinafanyika . Bwana bromhead jasusi wa M16 alitafakari na kuwazua ,kwanini Oleg alichagua wakutane kwenye hotel ya østerport iliyo karibu na uelekeo wa ubalozi wa Soviet. What if ilikuwa ni set up? Na Je vipi mpango wa ku mu approach ateme Siri za USSR bwana Oleg ukienda kombo. What if yeye akawa ndio chambo na akawa recruited na KGB? Maana kwenye ulimwengu wa ujasusi linawezekana muda wowote swala la usaliti na Utiifu unatengwa na mstari mwembamba sana. Siku tatu baadaye bwana bromhead alikatiza cemetery nyuma za ofisi ya ubalozi wake Hadi mitaa iliyokuwa hotel ya østerport kwenda kukutana na Bwana Oleg.
Alifika na kukaa kwenye nafasi ambayo angeweza kumuona kila anayeingia ndani. Na muda huohuo Oleg alifika na kuchukua nafasi. Mazungumzo Yao yalikuwa ni maswala ya miziki, falsafa, siasa na dini. Huku wakipata kahawa na snacks , Bwana. Bromhead alimwambia kama mazungumzo haya yote anaweza kuyaweka kwenye file.[emoji102][emoji102] Oleg aliafiki hili swala. Na hapo wakaagana. Kila kikao Bwana bromhead alikuwa anawatonya manjagu wenzake wa M16 huko London. Hiki. Kikao pia bwana Oleg alireport pia Moscow kwa boss wake .
Swala la ajabu likatokea ni kwamba kwa zaidi ya miezi nane hakukuwa na mawasiliano ya aina yoyote baina ya bromhead Wala Oleg . Haikuwai fahamika ni kwanini. Hili swala hata bwana guscott huko London lilimshangaza sana kwa kuwa hakukuwa na update za aina yoyote kuhusiana na mazungumzo au kukutana kati Oleg na bromhead . Ikawa imeonekana mpango huu kabambe umekuwa terminated. Kwa Bwana Oleg aliona hakukuwa na Mpango wa bwana bromhead kutaka wakutane tena. Ukimya huu huenda ungeleta faida , Gordievsky aliwaza .

Iliwahi semwa kwenye ulimwengu wa manjagu nanukuu: in spying, as in love, a little distance,a little uncertainty,an apparent cooling, on one side or the other, can stimulate desire". Na kweli ukimya huu ulimpa Oleg kiwewe kwa kiasi fulani cha kutaka wakutane tena na bromhead.

Lakini bwana bromhead alionekana Tena 1 oktoba 1974. Ikasemekana alikuwa kikazi huko Ireland kaskazini . Akakutana na bwana Oleg kwenye hotel Moja ya kifahari sana iliyokuwa inamilikiwa na shirika la ndege la Scandinavia SAS. Kikao hiki kilikuwa Cha Siri maana Oleg hakumtaarifu boss wake kwa namna yoyote ile. Wakiwa katika Convo za hapa na pale bwana bromhead alivunja ukimya ,akamwambia Oleg kwamba tayari yeye anajua ni KGB agent anayefanya kazi idara ya FCD kitengo kidogo cha political intelligence. Bromhead akamuuliza ni nani anayesimamia hicho kitengo na ndipo bwana Oleg Kwa kifupi alifunguka na na alijibu tu IAM. Kikao hakikuwa na mambo mengi sana baada ya kupata kilaji guscott alinyanyuka na kuafikiana wangekutana Tena wiki tatu zijazo. Guscott aliondoka na bwana Oleg akafuata akaondoka .

Rasmi Sasa bwana Oleg tokea hapo akawa ni jasusi mtiifu wa KGB anayefanya kazi na idara ya ujasusi ya uingereza ya M16 .[emoji88][emoji88][emoji91].
Oleg akiwaza kuhusu familia yake ,kifo Cha bro wake Vasili. Utawala wa kikomunisti wa Soviet, manyanyaso yote waliopitia Czechoslovakia na Hungary , Mgogoro wa ndoa yake , na culture barrier Baina ya West na east Soviet ,hayo yote Sasa ilibidi Aishi maisha ambayo ni DOUBLE LIFE . Kama double Agent. Alihisi ni usaliti mtakatifu anaoufanya . Na ni nini kitampata endapo maafisa wa KGB hususan wakubwa zake wakagundua usaliti wake. Hayo yote yalikuwa kichwani mwake

Hili swala baada ya bromhead kureport bwana Oleg Yuko tayari kushirikiana nao ,huko London kuliitishwa kikao Cha dharura Cha maafisa wa ngazi za juu za usalama wa taifa la uingereza . Walikutana kwenye kambi ya mafunzo ya M16 Monckton Kwenye mji wa Portsmouth kusini mwa uingereza. Agenda ya kikao hicho ni namna ya kumtumia SUNBEAM (Oleg). Report yake ilijadiliwa kwa kina wakichambua hasara na faida za kumtumia Oleg jasusi wa KGB kupata Siri za Soviet union. Baada ya kuafikiana na mpango ukapewa baraka zote kama walivyopanga walitawanyika.
Hatari
 
Kuna yanayoendelea sasa ktk nchi za Urusi,Ukraine na west ambapo majasus wa kila upande wanahaha kutafuta taarifa


Mfano unakuta west wanasafirisha silaha kuzipeleka Ukraine kwa ajili ya mapambano lkn hizo silaha inabid ziende kwa kificho


Wakat huo Urusi kupitia majasus wake nae anataka kujua silaha zinapitia wap na kuhifadhiwa wap ili azilipue


Kwa hiyo majasus wanashirik pakubwa kwenye hili zoez
 
Surely huku sio kwa kila mtu ,watu wanakuumbua na facts na sio rahisi watu kuwachota akili kizembe zembe .Na pia huku nasikia hata top official figures wa serikalini hupita huku kwa fake i.d kuchukua nondo kimya kimya [emoji28][emoji3578][emoji3578]
[emoji28][emoji28][emoji28]...! Lazima I see huku kuna nondo hatari. Mtu mwenye uelewa lazima uje uchote maarifa huku.

Ukitaka kujua huku kuna nondo za maana pitia huu Uzi, members wamejadiri kama wako bunge la congress.

Huku sio kwa majaribio. Ukileta kitu huku uwe na uhakika, utafikiri watu wanaingia mpaka moyoni mwako
 
Kuna yanayoendelea sasa ktk nchi za Urusi,Ukraine na west ambapo majasus wa kila upande wanahaha kutafuta taarifa


Mfano unakuta west wanasafirisha silaha kuzipeleka Ukraine kwa ajili ya mapambano lkn hizo silaha inabid ziende kwa kificho


Wakat huo Urusi kupitia majasus wake nae anataka kujua silaha zinapitia wap na kuhifadhiwa wap ili azilipue


Kwa hiyo majasus wanashirik pakubwa kwenye hili zoez
Haya mambo Huwa yanakuja kugundulika Baada ya vita kuisha ,pale wataalamu wa hayo maswala wanapokuja na tafiti za kijasusi kuhusiana na hii vita.
 
Nimejaribu kuanzisha Uzi na kupandisha humu jf ila naona kama umezuiliwa na mods Sasa sijui shida ni nini haswa na huo Uzi [emoji848][emoji848]. Nawaomba wanipe maelezo
Wakileta maznguzi unganisha na huu tuu
 
Nimejaribu kuanzisha Uzi na kupandisha humu jf ila naona kama umezuiliwa na mods Sasa sijui shida ni nini haswa na huo Uzi [emoji848][emoji848]. Nawaomba wanipe maelezo
Uzi Gani huo itakuwa mods hawajau release don't forget to tag me please
 
Na marafiki zangu ni wa Irish aisee wakija bongo wakienda supermarket wananunua bidhaa made in Irish Kwa kuzitafta na wanafurahia kabisa huku Tanzania sijui kwanini hatupendi kununua vitu made in Tanzania tunapenda vya nje
Quality
 
Kuna yanayoendelea sasa ktk nchi za Urusi,Ukraine na west ambapo majasus wa kila upande wanahaha kutafuta taarifa


Mfano unakuta west wanasafirisha silaha kuzipeleka Ukraine kwa ajili ya mapambano lkn hizo silaha inabid ziende kwa kificho


Wakat huo Urusi kupitia majasus wake nae anataka kujua silaha zinapitia wap na kuhifadhiwa wap ili azilipue


Kwa hiyo majasus wanashirik pakubwa kwenye hili zoez
Kati Kwa kati
 
Back
Top Bottom