Tarehe 9-12-1961 ilikukuta wapi?

Tarehe 9-12-1961 ilikukuta wapi?

Kuna hii picha aliileta M Said na kuelezea kuwa ni Kariakoo mwaka 1950 mtaa wa Congo
Mpaka nyumba akawa anazitaja za kina nani

Ila ukiangalia hiyo picha kwenye mitandao ya Historia utakuta kila mmoja ameweka mwaka anaoujua sijui kwanini wanapotosha View attachment 2837563
Nje ya mada kidg
Kizazi hiki kimeshindwa kabisa kujenga nyumba kwa mpangilio ukicheki hapo juu nyumba za matope zimekaa kwa mstari
 
Heri ya siku ya uhuru wadau.

Nikikumbuka siku ya tarehe 09/12/1961 naona ni kama juzi tu kumbe ni miaka kibao imepita.

Nakumbuka siku hiyo tulivyochinja mbuzi nyumbani kusherekea uhuru, nakumbuka mvua kubwa ilivyonyesha mpaka kusababisha maji kujaa ziwa Victoria kupita kingo zake.

Kweli wakati ni ukuta.

Mkuu unakumbuka nini siku hii?
Ilinikuta nina miezi 11 toka kuzaliwa kisangani Congo
 
Nje ya mada kidg
Kizazi hiki kimeshindwa kabisa kujenga nyumba kwa mpangilio ukicheki hapo juu nyumba za matope zimekaa kwa mstari
Ni kweli kabisa mkuu, Enzi hizo kulikuwa na nidhamu na watu wanafuata sheria kweli kweli
Ila leo unajenga unavyotaka
Unaweza kukuta mtu anajenga kukwepa jua lisimchome asubuhi, na mwingine anaamua kuweka ukuta kwenye dirisha la jirani na bwana ardhi hana ubavu maana kapewa hela

Sasa hali inazidi kuwa mbaya siku hadi siku na kuna watu wengi wanaona sawa tu
Sheria hazifuatwi ni virugu tu sio nchi tena limekuwa soko
 
Back
Top Bottom