Nilikuwa duniani, ila sikumbuki hilo tukio maana unajua tena waswahili kila leo ni sherehe wala hujui nini kinaendelea
Sherehe tangu uhuru mpaka leo ndio maana hata maendeleo ni zero
Niliona ni ujinga kuishi huko nikasepa baada ya kuona maduka ya ushirika ya Nyerere wameanza kuuza ngano unalazimishwa na sabuni
Ila miaka 10 ya kwanza ya Uhuru tulikuwa bado tuna mentality za kizungu maana watu walikuwa wanajielewa sana na akili kibao
Baba alikuwa mfanyabiashara na supplier mkubwa kwa wazungu, Gari lake lilikuwa Land Rover nakumbuka mwaka 1967 alinunua ila kulikuwa na wakulima wawili pia walikuwa na Peugeot kabla ya mzee hao walikuwa nazo kabla ya Uhuru
Maisha zamani yalikuwa matamu asikuambie mtu yaani mswahili tajiri tena anatamba na Gari?
Hapo ndio wenye roho ya korosho wakaingia madarakani na kuona wao waanze nao badala ya kuwahamasisha waendeleze biashara zao
Mahasidi wametufanya hivi ila poleni sana