Tarehe kama ya leo Oktoba 25, 2015 tulipiga kura na kuchagua haya maisha, mnakumbuka?

Asanta mkapa, Nape, January, Kikwete, Libuva, IGP Mangu...
nia yenu ndio imelifikisha taifa hili hapa..
Hapa ambapo yametimia maana hapa ndipo ambapo ukipita mtaani wanasaga meno kwani yule alishasema nikiishika watatembea kwa meno..
Hivi ni kwanini aliomba hii nafasi? Ina maana alikuwa anakumis kuumiza watu akawa anakosa fursa ya kufanya hivyo? Shida ya kuwapa madaraka wakimbizi toka nchi jirani ndio hii.
 
Hahahahahahahah nhahahhahahah nimecheka mbaka mbavu zimeniuma hahaha hakika haya ndio maisha tuliyoyachagua.
 
Aaaaamin
 
Wakuu nawasalimia kwa upendo mkubwa sana , na baada ya salamu naingia moja kwa moja kwenye hoja yangu .

Tarehe kama ya leo miaka mitatu iliyopita nchi yetu iliingia kwenye vitabu vya historia ya dunia kwa kukubali kupokea laana kwa mikono miwili baada ya Tume ya uchaguzi kuacha weledi na kuamua kusikiliza matakwa ya watu binafsi kwa kutoa matokeo ya uchaguzi kutokana na maelekezo ya watu hao .

Kisiwani Zanzibar hali ilikuwa mbaya zaidi ambapo Mtukufu Salum Jecha , Mwanachama wa ccm aliyewahi kugombea ubunge siku zilizopita , kabla ya kuangukia pua kwenye kura za maoni , akiwa kama Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi alifuta matokeo yote ya uchaguzi baada ya kubaini kwamba chama chake kimeshindwa , akaitisha uchaguzi mpya ambapo miongoni mwa waangalizi wa kimataifa alikuwa ALI KARUME !

Wachunguzi wa mambo wanasema kwamba huu ugumu wa maisha unaoikabili nchi yetu , matetemeko , ajali za vivuko na magari ya serikali na kila Mkwamo mnaouona ni sehemu ndogo tu ya laana hii .

Nimeamua kufanya maadhimisho haya ili kumuenzi Mwenyezi Mungu ambaye amekataza dhuluma katika vitabu vyake vyote .

Naomba kuwasilisha .
 
Hizi ni porojo tu za wanamitandao ambao wengi wao sio wapiga kura. Wapiga kura wako kimya wakisubiri kipindi kingine tena cha kutahiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…