Tarehe kama ya leo Yanga SC iligomea mchezo, kwa madai Simba SC kuvaa viatu vya mpira

Tarehe kama ya leo Yanga SC iligomea mchezo, kwa madai Simba SC kuvaa viatu vya mpira

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Kuelekea pambano la watani wa Jadi nchini Tanzania litakalo vurumishwa kunako dimba la Uwanja wa Taifa, tukio la kukumbukwa na kutamaushwa ni hili;

Tarehe kama ya leo 28/9/1953 miaka 65 iliyopita (kabla kuzaliwa chama cha TANU), klabu ya Yanga SC iligomea mchezo wa fainali ligi ya Ilala (wakati huo hakuna ligi kuu wala ya Taifa) dhidi ya Simba SC (wakati huo ikiitwa Sunderland) kwa madai kuwa Simba SC ilivaa viatu vya mpira ilhali wao hawana.

Ikumbukwe klabu ya Simba SC kutoka barabara ya Msimbazi ndio ya kwanza nchini Tanzania kuvaa viatu vya kusakatani kabumbu mnamo mwaka 1951 huku Yanga SC kutoka mitaa ya Jangwani ikianza kucheza na Makatambuga mnamo1960 mwaka mmoja kabla ya Uhuru.
IMG_20180928_165216_146.jpg
IMG_20180928_165251_186.jpg
IMG_20180928_165146_755.jpg
 
Naam...Wakati wakisubiri kichapo Septemba 30, tuwarejeshe yaliyofichika.
Tuwe wakweli Mtani mlivaa viatu ka hizo au ndio picha tu kushibisha uzi wako.

Maana sidhani kama vilifanania au kufikia robo ya hivyo sio kimuonekano tu bali hata kwa ubora. 😂😂😂😂
 
Sasa ukata unahusiana nini Mtani wakati tunachokiangalia sasa ni kucheza na kukufunga mdomo na tambo zako.
Ni....FlashBackFriday kuelekea mtanange wa watani wa jadi. Unajua kama hujui unakotoka huwezi kujua unakokwenda.
 
Mkuu, pia ungesindikiza uzi wako na picha za makatambuga...
 
Hahahaaa. Sitaki mieee.

Uwepo hewani tu sio yote haya halafu mwisho wa siku unatokomea. [emoji23][emoji23]
Nitakuwepo Insha' Allah na huenda tukafanya kolabo la wakali kutoka Msimbazi sembo, Ghazwat kukuleteeni mtanange hapa JF kwa mara ya kwanza.

Usibonye kidude. Uangalie namna mnyama mkali mwituni akirarua vilivyo.
 
Back
Top Bottom