Tarehe kama ya leo Yanga SC iligomea mchezo, kwa madai Simba SC kuvaa viatu vya mpira

Tarehe kama ya leo 28/9/1953 miaka 65 iliyopita (kabla kuzaliwa chama cha TANU), klabu ya Yanga SC iligomea mchezo wa fainali ligi ya Ilala (wakati huo hakuna ligi kuu wala ya Taifa) dhidi ya Simba SC (wakati huo ikiitwa Sunderland) kwa madai kuwa Simba SC ilivaa viatu vya mpira ilhali wao hawana.

Ikumbukwe klabu ya Simba SC kutoka barabara ya Msimbazi ndio ya kwanza nchini Tanzania kuvaa viatu vya kusakata kabumbu mnamo mwaka 1951 huku Yanga SC kutoka mitaa ya Jangwani ikianza kucheza na Makatambuga mnamo1960 mwaka mmoja kabla ya Uhuru.View attachment 880476View attachment 880477View attachment 880478
Timu iliokua inacheza na yanga ni simba au sunderland???
 
Mkuu ikifika ile Tarehe ambayo Mikia walitia mpira kwapani Timu zilipoenda mapumziko match ya Yanga,nishtue.
 
Naam...Wakati wakisubiri kichapo Septemba 30, tuwarejeshe yaliyofichika.
Usisahau na ile Tarehe mliyotia mpira kwapani mapumziko Shamba la Bibi. Na pia ukumbuke Mikia haijawahi kuifunga wala kutoa draw na Yanga match yoyote iliyochezwa September.
 
Ha ha ha. Endelea kucheza kwa ramli mkuu

Kikosi gani safari hii cha kufanya hivyo?

Hata hivyo umeandika hali una wasiwasi kuona kuwa zile 5 zitarejea!
 
Mkuu nasikia kambi mmeweka Kinyerezi,Mo amegona kutoa hela amekasirika kawapeleka Turkey lakini hakuna lolote la maana mlilorudi nalo.
 
Hivi mkuu.. Uliona wapi Real Madrid anakwenda Dubai kuweka kambi kujiandaa na Barcelona?

Tumeacha hayo mambo, tunajiamini kukufunga hata tuweke kambi mtaa wa Twiga Kariakoo.
 
Jibu swali wacha kurukaruka, hiyo ilikuwa Simba au Sunderland?
Nimejibu kuwa Simba. Wakati huo ikiitwa Sunderland..

Au hujui kuwa kabla ya kuitwa Simba ilikuwa ikiitwa Sunderland?
 
Kuelekea pambano la watani wa Jadi nchini Tanzania litakalo vurumishwa kunako dimba la Uwanja wa Taifa, tukio la kukumbukwa na kutamaushwa ni hili;

Tarehe kama ya leo 28/9/1953 miaka 65 iliyopita (kabla kuzaliwa chama cha TANU), klabu ya Yanga SC iligomea mchezo wa fainali ligi ya Ilala (wakati huo hakuna ligi kuu wala ya Taifa) dhidi ya Simba SC (wakati huo ikiitwa Sunderland) kwa madai kuwa Simba SC ilivaa viatu vya mpira ilhali wao hawana.

Ikumbukwe klabu ya Simba SC kutoka barabara ya Msimbazi ndio ya kwanza nchini Tanzania kuvaa viatu vya kusakatani kabumbu mnamo mwaka 1951 huku Yanga SC kutoka mitaa ya Jangwani ikianza kucheza na Makatambuga mnamo1960 mwaka mmoja kabla ya Uhuru.View attachment 880476View attachment 880477View attachment 880478
Yaani timu ianzishwe mwaka 1935 alafu mwaka 1953 hawana viatu hakika wewe shabiki wa mbumbu FC.
 
Timu ya Taifa ilicheza vifua wazi bila jezi mbele ya Rais wa Sudan na Mwalimu Nyerere uwanja wa Uhuru Julai 4, 1972.

Inakuwaje unashangaa klabu kukosa viatu kwa wakati huo. Ndo maana niaona nyie Vyura wengine hamjui chochote kwenye soka la Tanzania

Chukua hiyo utoe utandu au tongotongo kutoka bwawani, na kama unajiona Kinda, basi acha kubisha usilolijua

Makwasukwasu FC wewe!
IMG_20180928_221618_732.jpg
 
Bila picha au ushahidi wa video clip,kakojoe ukalale..
 
Timu ya Taifa ilicheza vifua wazi bila jezi mbele ya Rais wa Sudan na Mwalimu Nyerere uwanja wa Uhuru Julai 4, 1972.

Inakuwaje unashangaa klabu kukosa viatu kwa wakati huo. Ndo maana niaona nyie Vyura wengine hamjui chochote kwenye soka la Tanzania

Chukua hiyo utoe utandu au tongotongo kutoka bwawani, na kama unajiona Kinda, basi acha kubisha usilolijua

Makwasukwasu FC wewe!View attachment 880780
Mwaka 72 Shida ilikua jezi zimefanana na mwenyeji ikaonekana busara avue jez, wacheze tumbo wazi alafu ulikua mchezo wa kirafiki. Baada ya mapumziko zikaletwa jezi nyingine waka zivaa. Kwaiyo ndugu usidanganye watu ukifikiri wote ni mbumbu fc.
 
Tunazungumzia uhaba wa vifaa. Kuwa miaka ya nyuma hakuna, sasa kama jezi zilifanana kwa fikra zako, si kuna jezi ya away na nyumbani.

Si angebadili rangi tu. Tatizo lipo pale pale uhaba wa vifaa vya michezo.

Ikiwa hujui hilo, utajua kweli kwanini mnaitwa Gongowazi? Au Ndala?
 
Back
Top Bottom