Kuelekea pambano la watani wa Jadi nchini Tanzania litakalo vurumishwa kunako dimba la
Uwanja wa Taifa, tukio la kukumbukwa na kutamaushwa ni hili;
Tarehe kama ya leo
28/9/1953 miaka 65 iliyopita (kabla kuzaliwa chama cha TANU), klabu ya
Yanga SC iligomea mchezo wa fainali ligi ya Ilala (wakati huo hakuna ligi kuu wala ya Taifa) dhidi ya Simba SC (wakati huo ikiitwa Sunderland) kwa madai kuwa
Simba SC ilivaa viatu vya mpira ilhali wao hawana.
Ikumbukwe klabu ya
Simba SC kutoka barabara ya Msimbazi ndio ya kwanza nchini Tanzania kuvaa viatu vya kusakatani kabumbu mnamo mwaka 1951 huku
Yanga SC kutoka mitaa ya Jangwani ikianza kucheza na Makatambuga mnamo1960 mwaka mmoja kabla ya Uhuru.
View attachment 880476View attachment 880477View attachment 880478