Tarehe/siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa


Pole Tegelezeni....kwa kifupi, hakuna njia yeyote ya uzazi wa mpango ambayo inaharibu uzazi. Njia ya uzazi wa mpango zinazuia mimba kutunga tu aidha kwa kuzuia yai lisitoke (dawa za vidonge, sindano na vijiti), au kwa kuzuia yai lilirutubishwa lisijishike kwenye kizazi (IUCDs), au kuzuia yai lisirutubishwe (barriers eg condom, cervical cap). Hakuna kati ya hizo inayoharibu uzazi, kwani unapoacha kutumia njia ya uzazi wa mpango basi waweza pata ujauzito kama kawaida.

Mkeo alikuwa anatumia njia ya sindano (DepoProvera), hii sindano hudumu kwa miezi mi3...iana maana kama ukitaka apate ujauzito basi anaacha kutumia sindani na inabidi ipite zaidi ya miezi mi3 ili kuweza kupata ujauzito tena. Mkeo ameacha tangu mwaka jana, hivyo ni zaidi ya miezi mi3. Yes, ni muda muafaka kwa wewe kuanza kuwa worried kwa nini hapati ujauzito.

Kuna sababu nyingi zinazoweza sababisha mimba isitunge kama wote mko sawa (meaning hakuna mwenye tatizo). Tatizo kubwa na common sana ni timing. Kuna siku ambazo mwanamke anakuwa katika siku ambazo ukikutana naye basi anapata ujauzito, hakikisha kuwa mnakutana katika siku hizo. Anxiety ni sababu nyingine...wanawake wanapokuwa na shauku sana ya kupata ujauzito (mara nyingi kutokana na presha ya kuzaa toka kwa mume) inaweza ikawaathiri kisaikolojia na kwa kisai fulani kushindwa kutunga mimba.

Laknini pia kuna kitu kinaitwa 'secondary infertility' ambapo couple ambayo imeshawahi kuzaa, au mwanamke ambaye ameshawahi kuzaa akashindwa kutunga mimba tena...inaweza ikawa kwa sababu mirija (ovarian/fallopian tubes) imeziba, au uvimbe wa matezi yanayotoa mayai (ovaries), uvimbe wa kizazi hasa uterine fibroids, au kuna madabiliko ya hormones baada ya kujifungua.

Ushauri: Nendeni kwa daktari bingwa wa wanawake (gynaecologist) ataongea nanyi na pia kuwafanyia uchunguzi kama itabidi kisha kuwashauri nini cha kufanya ili mtimize lengo.
 
ukimwacha mkeo utapata laana kubwa sana ..mtoto mmoja hakutoshi?
 
Dah jamani hebu tusiwe watu wa kufuata kila kitu kinacholetwa na hawa watu weupe jamani....Hizi sindano za kila kukicha zinabadilil mfumo mzima wa uzazi jamani. kuwa mvumilivu pia mshukuru sana mungu kwa kumpata mtoto mmoja na jitahidi umpende mtoto na mke wako pia.....wapo watu wengi sana waliozaliwa peke yao na wakua wala usiwe na shida....ila sasa hizo sindano mi sikushauri kabisa ndg yangu utaharibu maana hayo ni full madawa na inaenda kubadili endocrine system kabisa ndugu yangu
 

Kifulambute...uwe na uhakika na unachokiongea kabla hujapost hapa JF, watu wanasoma na kufuata, unaposema UONGO ili kufurahisha nafsi yako kwa sababu tu una negative attitude na kitu fulani SI SAWA! Weka proof hapa kuwa contraceptives zinabadili mfumo wa uazazi...how? weka proof kuwa zinabadili mfumo wa endocrine..how?

Unawezaje kutumia hormones (contraceptive za sindano na vidonge ni hormones) ambazo ni specific kwa reproductive system kubadili endocrine system ambayo ni very complex and specific (key-and-lock receptor system)? Si haki kwa kweli kuwanyima watu haki ya kufaidika na uzazi wa mpango sababu tu ya attitude yako kwa uzazi wa mpango na kushauri watu kwa msingi wa UONGO!
 
Njia nzuri na salama ya uzazi wa mpango ni kalenda na kondom, hizi ni njia ambazo hazina madhara yoyote, hapa nikiwa na maana kwamba ikiwa wanandoa watatumia kalenda itabidi siku za hatari watumie condom, na matumizi haya yanatakiwa mwanamke ndo awe mfuatiliaji mkuu,maana

mwanamume ni ngumu kufuatilia siku za hatari kwa mkewe. Hizi dawa za vidonge,sindano na vijiti ni nzuri pia lakini zina madhara makubwa japokuwa tunaambiwa ni madogo, kwasababu sasa hivi
wanawake wengi wananenepeana bila mpango na unene wa kupindukia unamadhara

Makubwa sana,Sasa hivi wanawake wengi wanaongoza kuwa na vitambi kuliko wanaume,hasa jiji la Dar pia kufunga hedhi unapotumia hizi dawa maranyingi damu inafunga, hebu jiulize hiyo damu inatakiwa kutoka lakini haitoki kwakweli wataalamu wanasema hakuna madhara lakini mimi binafsi nadhani yapo. Hivyo ni vema tukarudia mfumo wa wazazi wetu zamani,hapo tutakuwa salama salimini.
 
Una bahati kwamba umejua tatizo ni hayo masindano, mi na mke wangu tumekubaliana kutotumia hayo masindano na madawa kabisa kwa sababu kuna mpangaji mwenzetu alitumia akawa anableed daily na ilikata baada ya mwaka mzima.

Hata hivyo ilichukuwa muda mrefu mpaka kupata mtoto wa pili, yakikukataa ni mabaya sana. Pateni ushauri wa dokta na pia uvumilivu unahitajika.
 
..........Kama alikuwa anatumia sindano kwa hiyo miaka 3, kushika mimba kirahisi itakuwa ngumu. Itachukua zaidi ya miaka 3 kuchukua mimba tena, hii lakini inategemea sumu ya sindano itachukua muda gani kutoka kwenye kizazi..........ila kuna dawa inaweza kwenda kusafisha hiyo sumu kwenye kizazi na kupata mimba kirahisi tu.
 
Peleka mawazo yako mbali zaidi,
What if wewe ndio una matatizo ya kizazi toka zamani,
Na hata huyo mmoja wa miaka mi3 inawezekana unamsaidia mtu kulea?
 
Acha kukurupuka, na humu kuna wajinga wengi wanaamini kila kitu anachafanya mzungu ni kutaka kutuangamiza, nenda kwa daktari mtapata solution ya maana.
 

Hapana Preta....sindano inadumu kwa miezi mi3, hivyo ukistop baada ya miezi mi3 hadi mi4 you are good to go!

Sindano zile wala hazifiki kwenye kizazi jamani...unajua mnaimagine kuwa ile dawa inafanya kazi kwenye kizazi ili kuzuia hizo mimba....LA HASHA! Haifiki na haifanyi kazi kwenye kizazi. Kizazi huwa kinatayarishwa na hormones ili kiweze kubeba mimba, na pia ni horomones hizo hizo zinazofanya yai likomae na kutolewa ili lirutubiashwe na kubeba mimba. Hizi hormones za kwenye contraceptives (sindano, vijiti na vidonge) zinadisrupt tu ile balance au concentration ya hormonoes kwenye damu na hivyo process nzima inakuwa imevurugika kiasi mimba haiwezi kutunga.
 
Thanks Dr.

Pipa nadhani stress and overdoing it may affect both...

si vibaya wakipata rest, relaxation, chakula bora na kuondoa kabisa stress, pia si vibaya wakikaa kwa muda bila kuchugana na wawe very relaxed
 
Please naomba msaada wenu,mimi nina mpenzi wangu ana mimba na inaonekana amepata hiyo mimba kati ya tarehe 1may hadi 5may ,hizo ndiyo siku tulizofanya mapenzi frequently:
SWALI: kwa mda huo je, anatakiwa kujifungua lini? maana ananiambia eti mwezi wa kwanza!!!!!.

Jamani naomba msaada wenu,nisije mwenzenu kuingizwa mjini..
 
Jumlisha miezi 9, (+ or -) 1 week.
Kama sio basi umepigwa changa
 
Kama ni mimba ya kwanza na kama ni mwisho wa january ni sawa. maana mara nyingi mimba ya kwanza anaweza kuzaa kuanzia 38 weeks... ila unahesabu 38 weeks kuanzia siku ya mwisho alipata heidh
Mfano:
Kama anapata heidh kila baada ya siku 28, na ya mwisho ilikua ni tarehe 22-may-2011 basi atakua alipata mimba 5th-05-2011 na atazaa 21 jan 2011. sasa hivi ana mimba ya wiki 33, kwenda 34...
 
Zidisha 28 mara 9 utapata jibu inakuwaje unasex na m2 ambaye humwamin?

2METHUBU2 2MEWEZA NA 2NASONGA MBELE
 

Kwa mahesabu ya kitabibu pia kulingana na tareh ulizotaja ni kwamba tarajia kupata mtoto kati ya tar 8 hadi 12 mwez feb, 2012. Karibu tena kwa swali lingine
 

... Wewe muulize tarehe yake ya mwisho ya hedhi. Kitabibu ili kujua tarehe ya kujifungua:
Unachukua tarehe ya mwisho ya hedhi[LMP=Last Mestrual period] unajumlisha na 7,unachukua mwezi wa mwisho wa hedhi unaongeza au unatoa 9 hapo unajua lini anatarajia kujifungua [EDD= Expedected Day Of Delivery]
... Kwa mfano kama LMP ilikuwa
26/4/2011 unachukua 26+7= 33, april ina siku 30, 33- 30= 3 may: 5+9= 14 mwaka una miezi 12 so 14-12= 2 [feb].
So EDD[Expected day of delivery ]
ni 03 february.
... Angalizo ni vigumu kujua mtoto ni wa kwako kwa kuangalia facts eti ulisex na that lady siku
gani. Kaa ukijua ni sperm moja tu inatosha kutengeneza mtoto[ the fastest,healthly,strong one]. So siku hizo sijui 5 unauhakika alisex nawe pekee! Kama kuna jamaa alikuwahi akatanguliza sperm yake mchana na ikatengeneza kimimba,utatuambia nini? Wakati mwingine ni bora kuaminiana tu kama tunavyoamini kuwa kesho kuna wokovu... Kama humuamini
kivile subiri siku katoto kakizaliwa kama hakafananii nawe [kwa imani yako],kang'oe tunywele tuwili ukacheki DNA kama zinarandana na za kwako !
...VP NIMEKUCHANGANYA MKUU ?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…