Riwa
Platinum Member
- Oct 11, 2007
- 2,607
- 3,079
Mimi na mke wangu tumejaaliwa kupata mtoto mmoja katika ndoa yetu. tulikubaliana kwamba, mwenetu akifikisha miaka 3 tutafute mtoto wa pili. kipindi chote tangu mke wangu ajifungue alikuwa anatumia njia ya uzazi wa mpango ya kuchoma sindano, na mtoto wetu alipofikisha miaka 3 mwishoni mwa mwaka jana, alisimama kuchoma hizo sindano ili tuanza michakato ya kumtafuta mtoto wa pili. mwenzenu naona mwaka unakatika lakini sioni dalili mke wangu kushika mimba.......... kulikoni, au ndio sindano zishaharibu uzazi?
Nimekuwa worried na mustakabali wa kutengeneza familia, nawaomba wataalamu wa utabibu mtusaidie...................... Tunatanguliza shukrani zetu za dhati...............
Pole Tegelezeni....kwa kifupi, hakuna njia yeyote ya uzazi wa mpango ambayo inaharibu uzazi. Njia ya uzazi wa mpango zinazuia mimba kutunga tu aidha kwa kuzuia yai lisitoke (dawa za vidonge, sindano na vijiti), au kwa kuzuia yai lilirutubishwa lisijishike kwenye kizazi (IUCDs), au kuzuia yai lisirutubishwe (barriers eg condom, cervical cap). Hakuna kati ya hizo inayoharibu uzazi, kwani unapoacha kutumia njia ya uzazi wa mpango basi waweza pata ujauzito kama kawaida.
Mkeo alikuwa anatumia njia ya sindano (DepoProvera), hii sindano hudumu kwa miezi mi3...iana maana kama ukitaka apate ujauzito basi anaacha kutumia sindani na inabidi ipite zaidi ya miezi mi3 ili kuweza kupata ujauzito tena. Mkeo ameacha tangu mwaka jana, hivyo ni zaidi ya miezi mi3. Yes, ni muda muafaka kwa wewe kuanza kuwa worried kwa nini hapati ujauzito.
Kuna sababu nyingi zinazoweza sababisha mimba isitunge kama wote mko sawa (meaning hakuna mwenye tatizo). Tatizo kubwa na common sana ni timing. Kuna siku ambazo mwanamke anakuwa katika siku ambazo ukikutana naye basi anapata ujauzito, hakikisha kuwa mnakutana katika siku hizo. Anxiety ni sababu nyingine...wanawake wanapokuwa na shauku sana ya kupata ujauzito (mara nyingi kutokana na presha ya kuzaa toka kwa mume) inaweza ikawaathiri kisaikolojia na kwa kisai fulani kushindwa kutunga mimba.
Laknini pia kuna kitu kinaitwa 'secondary infertility' ambapo couple ambayo imeshawahi kuzaa, au mwanamke ambaye ameshawahi kuzaa akashindwa kutunga mimba tena...inaweza ikawa kwa sababu mirija (ovarian/fallopian tubes) imeziba, au uvimbe wa matezi yanayotoa mayai (ovaries), uvimbe wa kizazi hasa uterine fibroids, au kuna madabiliko ya hormones baada ya kujifungua.
Ushauri: Nendeni kwa daktari bingwa wa wanawake (gynaecologist) ataongea nanyi na pia kuwafanyia uchunguzi kama itabidi kisha kuwashauri nini cha kufanya ili mtimize lengo.