Tarehe/siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa

Katika kuhesabi siku, ile siku unayoona tone la damu(yaani unapoanza) ndiyo siku yako ya kwanza( yaani tarehe moja ya mzunguko wako. Kwa mahesabu rahisi ni kuwa chukua idadi ya siku za mzunguko wako wa mwezi, zigawe mara mbili, kisha hesabu siku mbili mbele na mbili nyuma. Hizo ndiyo siku za mimba. Mfano, kama una mzunguko wa siku 28, gawa kwa mbili ni siku 14. Jumlisha mbili ni siku ya 16 na toa mbili ni siku ya 12. Kwa kuondoa wasiwasi unaweza kuanzia siku ya 11 hadi ya 17. Hivyo tarehe za mimba ni kuanzia siku ya 12 hadi ya kumi na sita. Siku nyingine zote ni bwerereeee! Natumaini nimeeleweka!
 
ni kwamba mfano nimeanza kubrid date 26 then date 29 nimemaliza mi nataka kujua siku yangu ya kushika mimba ni ipi? na siku zangu ambazo sio za hatri ni zipi?

mzunguko wako ni siku ngapi? Kama siku 28 thenkuanzia tarehe 26 hesabu siku kumi hizo ni salama, then siku ya 11-17 ni hatari haswa siku ya 13&14. Baada ya siku 17 upo salama
 
Mkuu umeelekezwa vzr fanyia kazi halafu lete matokeo hapa.
 
inategemea na mzunguko wako, kama ni regular then if ur 28 days circle frm day 10 to 13 ni risk then 14 to 15 ni unsafe i.e fertility days then 16 to 17 risk and the rest safe..bt if ni 32 circle frm day 11 to 14 ni risk then 15 to 16 unseif then 17 to 21 risk and the rest ni seif NB LAZIMA UJUE MZUNGUKO WAKO USIKARIRI KISA MWENZAKO ANAENDA 28 KAMA WENG WAZANIAVYO.
 
dah hiyo nikweli nimepiga mahesabu nimeona imebalance. Asante sana
 
Huu mjadala unaendelea kwa ndugu yangu wa karibu, kuwa mke wake alishiriki nae siku sita baada ya kumaliza siku zake (siku ya sita ni toka siku ya kwanza ya kuona mwezi na inahuisha siku tatu za hedhi), lakini cha ajabu anadai wamepima wamekuta mimba je inakuwaje?
 
ndo imewezekana hivyo, si kashika sasa?

Anyway, kuna akina mama wanaendelea kupata hedhi hadi ujauzito wa miezi 3 nadahni.

note: mie si dokta na biology nilipata Father Xmas
 
Vp inawekana mwanamke kupata mimba wakati akiwa kwenye siku zake?
 
Nijuavyo mimi ukweli ni kuwa siku sita ukijumlisha na hedhi hawezi kupata maana 5-6 days kitaalamu zaweza kuwa ni siku za hedhi kulingana na mwanamke na mwanamke.

Kutoka hapo kuna siku 5 hadi kufikia siku ya 11 ambayo inakribisha siku za hatari.

Niwezacho kusema ni kuwa labda shemeji yako alikuwa na mimba lakini hakujijua lakini akawa anaendelea na mzunguko kama kawaida kama alivyosema Kongosho au kamuuzia mbuzi kwnye gunia bro wako.
 

Kuna uwezekano mkubwa wa hapo kwenye 'red'....kifiziolojia, ni impossible mwanamke kupata ujauzito siku ya 6 tangu AANZE hedhi. Hedhi ni mzunguko wa mwezi mzima (inategemea na urefu wa mzunguko wa mwezi lakini ni kuanzia siku 26 - 32), lakini uwe mzunguko mfupi au mrefu...haiwezekani kupata mimba siku ya 6 kwa hali ya kawaida! Siku za hatari ni kuanzia siku ya 11 tangu AANZE hedhi mpaka siku ya 18.

Kuna baadhi ya wanawake huwa wanapata hedhi wakiwa na mimba changa (mwezi wa kwanza au miwili ya mwanzo), japo huwa si nyingi kama ilivyokuwa kawaida, lakini ni rahisi kwa mwanamke kuiconfuse na hedhi ya kawaida kwani huja kipindi kile kile mwanamke huyo anataraji kupata hedhi.
 

Kuna baadhi ya wanawake huwa wanapata hedhi wakiwa na mimba changa (mwezi wa kwanza au NIJUAVYO MIMI, KUNA MIZUNGUKO YA CKU 14, 21, 28, NA 35. HUYU MWENYE CKU 14 ANAPATA HEDHI MARA 2 KWA MWEZI NA NI WACHACHE SANA BINAFSI CJAWAHI KUMUONA. THEN KAMA ATAKUWA M1WAPO, INAWEZEKANA. KAMA KUNA MASHAKA PIMA DNA, AU HESABU WK 36 TANGU CKU YA MIMBA KMA ASIPOJIFUNGUA KUNA MASHAKA. CALL 0683 084658
 
Kwa experience yangu kwenye clinical medicine na pia public health (jumla ya miaka 13 now) sijapata kusikia mwanamke mwenye circle ya siku 14, hapa Tanzania! Wapo wachache sana wenye circle ya siku 21, wengi ni wa siku 27/28 hadi 30, na mara nyingi ushauri wangu huwa naugeneralize hapo..unless mhusika awe certain kuwa ana circle fupi zaidi ya hapo..then atapata ushauri specific kwa urefu wa cirlce yake!
 
Siku za hatari ni kuanzia siku ya 11 tangu AANZE hedhi mpaka siku ya 18.

Heshima yako mkuu Riwa, naomba elimu hapo kuhusiana na siku za hatari maana mimi sielewi kitu chochote.
 
Last edited by a moderator:
Heshima yako mkuu Riwa, naomba elimu hapo kuhusiana na siku za hatari maana mimi sielewi kitu chochote.

Elimu hiyo inakuwa 'reliable' kama unafahamu mzunguko wa mpenzio ni wa siku ngapi...maana mzunguko unatofautiana kutokana na urefu wa mzunguko kati ya wanawake. Wanawake wachache wana mzunguko wa siku 21 (mfupi), na wengi wana mzunguko wa kati ya siku 28 hadi 30, wanawake wachache tena huwa na mzunguko wa zaidi ya siku 30 (mrefu).

Hata hivyo...mizunguko yote (mifupi, kawaida, na mirefu) ina matukio mawili makubwa ambayo yanakuwa controlled na mabadiliko ya hormones kwenye mwili wa mwanamke (sitaingia kwenye details za hormones, huitaji sana kujua)..matukio hayo mawili makubwa ni 'Hedhi' - kutoa damu ya hedhi; na 'ovulation' au kutolewa kwa yai la kike, yai hutolewa kati kati ya mzunguko wa mwezi. Yai likitolewa, lina siku 3 au 4 kurutubishwa. Na pia, mbegu za kiume (manii) ikimwagwa ukeni, ina mpka siku 3 za kuwa hai na kuweza kurutubisha yai.

Mfano: Tuchukulie mwanamke mwenye mzunguko wa kawaida (yaani siku 28 hadi 30 tangu kuanza hedhi mpaka hedhi itakayofuatia)...kwa kawaida wanawake wanapata hedhi kwa siku 4 - 7, ukihesabu tangu mwanamke anapoanza kutoa damu ya hedhi, yai litatolewa siku ya 14 au 15. ukijumlisha siku 4 za uwezekano wa kurutubisha yai (inakuwa 18 au 19), na ukitoa siku 3 ambazo mbegu zinakuwa hai ukeni (inakuwa 11 au 12)...Kwa hiyo basi, kwa mwanamke mwenye mzunguko wa kawaida wa siku 28 hadi 30, siku zake za hatari za kushika mimba ni kuwanzia siku 11 tangu aanze hedhi hadi siku ya 19 tangu aanze hedhi!
 
Asante Dr, sasa nimeelewa vizuri zaidi...
 

U r right mate.
 

profesa unaweza kuwauliza pia haya maswali madaktari wataalam wa mambo ya watoto na kina mama kupitia mtandao wao wa Wanetu.com :: Elimu kuhusu Ujauzito na Uzazi, Malezi na makuzi ya watoto, Afya ya watoto, Saikoljia, Tabia na Haki za Watoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…