Elimu hiyo inakuwa 'reliable' kama unafahamu mzunguko wa mpenzio ni wa siku ngapi...maana mzunguko unatofautiana kutokana na urefu wa mzunguko kati ya wanawake. Wanawake wachache wana mzunguko wa siku 21 (mfupi), na wengi wana mzunguko wa kati ya siku 28 hadi 30, wanawake wachache tena huwa na mzunguko wa zaidi ya siku 30 (mrefu).
Hata hivyo...mizunguko yote (mifupi, kawaida, na mirefu) ina matukio mawili makubwa ambayo yanakuwa controlled na mabadiliko ya hormones kwenye mwili wa mwanamke (sitaingia kwenye details za hormones, huitaji sana kujua)..matukio hayo mawili makubwa ni 'Hedhi' - kutoa damu ya hedhi; na 'ovulation' au kutolewa kwa yai la kike, yai hutolewa kati kati ya mzunguko wa mwezi. Yai likitolewa, lina siku 3 au 4 kurutubishwa. Na pia, mbegu za kiume (manii) ikimwagwa ukeni, ina mpka siku 3 za kuwa hai na kuweza kurutubisha yai.
Mfano: Tuchukulie mwanamke mwenye mzunguko wa kawaida (yaani siku 28 hadi 30 tangu kuanza hedhi mpaka hedhi itakayofuatia)...kwa kawaida wanawake wanapata hedhi kwa siku 4 - 7, ukihesabu tangu mwanamke anapoanza kutoa damu ya hedhi, yai litatolewa siku ya 14 au 15. ukijumlisha siku 4 za uwezekano wa kurutubisha yai (inakuwa 18 au 19), na ukitoa siku 3 ambazo mbegu zinakuwa hai ukeni (inakuwa 11 au 12)...Kwa hiyo basi, kwa mwanamke mwenye mzunguko wa kawaida wa siku 28 hadi 30, siku zake za hatari za kushika mimba ni kuwanzia siku 11 tangu aanze hedhi hadi siku ya 19 tangu aanze hedhi!