Tarehe/siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa

Tarehe/siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa

Mimi mke wangu anajifunga kijiti kiunoni kama yuko kwenye hatari ya kupata mimba na mimba haiingii, tmefanya hivyo kwa muda wa mika 15 sasa

Fungwe hicho kijiti mmekipata wapi? Niliwahi kusikia Hospitali wana njia hiyo ya kuweka kijiti,,lakini wao wanaingiza ndani ya mwili (chini ya ngozi) sasa wewe chako kinafungwa kiunoni! MAKUBWA HAYO!

Au mlikichukua MVUMONI kwa KALUMANZILA??
 
kungurumweupe,
Nakushukuru sana kwa maelezo yako mazuri.

Hata hivyo naomba kutofautiana nawe kuhusu theory ya watoto zaidi ya mmoja yaani twins,triplets,nk.
1.Unasema mbegu zaidi ya moja zikirutubisha yai moja,basi yai hilo litagawanyika kulingana na idadi ya mbegu kutokeza " zygotes" kwa lugha rahisi "watoto" sawa na idadi ya mbegu za kiume.HII SI KWELI HATA KIDOGO MKUU.Hata siku moja ,haiwezekani mbegu zaidi ya moja kurutubisha yai lile lile moja.Daima,milele ,amina,mbegu moja ya kiume hurutubisha yao moja la kike.Ikumbukwe kua mara tu baada ya mbegu moja ya kiume kuingia ndani ya yai ,hutokea ukuta juu ya yai na chemical reactions nyingine kwenye yai ambazo huzuia mbegu nyingine ya kiume kuingia.

Nadharia,ya "Fratenal twins" yaani mapacha ambao si lazima wafanane,ambao huweza kuwa au wasiwe wa jinsia moja,ambao ni kama tu watoto wowote wa mama mmoja,hutokea pale ambapo mayai mawili ,kila yai kutoka ovary moja kulia na kushoto ,hutolewa wakati mmoja na hatimaye kurutubishwa na mbegu mbili za kiume,kila mbegu moja ikirutubisha yai la kwake.Watoto hawa huwa na placenta tofauti,kila mmoja ana placenta yake.Wanaweza kuwa wa jinsia moja au tofauti.Waweza kufanana au la.Kwa kifupi ni kama watoto wowote wa mama mmoja.Huwa huitwa FRATENAL TWINS au NON IDENTICAL TWINS.

2.nadharia yako kuwa kupatikana kwa watoto wawili au hufanana husababishwa na mbegu moja kurutubisha yai moja na kupatikana kwa muunganiko wa idadi ya chromosomes zaidi ya kiwango kinachohitajika,si kweli pia hata kidogo.Under normal circumstences muunganiko wa mbegu ya kiume na yai hutokeza zygote yenye chromosomes 46.Ikiwa itakua zaidi ya hapo ,basi mtoto atakua na malformations kama DOWNS SYNDROME n.k na si kua basi itagawanyika kusababisha twins,triplets etc.

Identical twins au Non fratenal twins hutokea pale ambapa mbegu moja hurutubisha yai moja,na kutokeza zygote yenye idadi inayohotajiwa ya chrosomes yaani 46 lakini wakati wa kuzalishwa na kuongezeka kwa chembe hai "cells" kitu ambacho hufanyika kwa speed kubwa sana,, katika hatua ya moja inayoitwa "morulla" ,kwa sababu nyingi including genetic factors and other unknown factors,hiyo morula huweze kugawanyika katika parts zinazolingana tuseme mbili,na kila part kukua independently na kuwa mtoto.Watoto hawa hukua katika placenta moja,wanapozaliwa wanafanana kila kitu kwani walitokana na mbegu moja ya kiume na yai moja la kike hivyo genetic yao {chembe zao za urithi } huwa sawa kwa asilimia mia moja.

Ndio maana huitwa IDENTICAL TWINS,TRPLETS,etc.Ila baada ya kuzaliwa kutokana na mazingira labda pia na nutritional differences kati yao,watoto hawa mara nyingi kufanana kwao hupungua taratibu.
Lakini nakubaliana nawe kwa maelezo yako mengine,isipokua haya.
I stand to be corrected.

Naomba kuwakilisha.
 
Kungurumweupe asante ; Heshima mkuu!!

Swali langu mie kama mwanaume nitazigunduaje hizo cycle yaani how do i tell kuwa hii ni 22, 28 na 35 etc ikiwa nataka kutegesha nimnasishe?

Pili breeding ya siku 9 mpka 10 ni normal? na kama mwenzi wako yuko hivi ndo anakuwa kwenye cycle ipi? ni haya tu.
 
Nimeikumbuka tipic ya REPRODUCTION form two 'B'
 
....
Pili breeding ya siku 9 mpka 10 ni normal? na kama mwenzi wako yuko hivi ndo anakuwa kwenye cycle ipi? ......




I hope unamaanisha, bleeding. Hiyo sio normal. Ni dalili ya matatizo kwenye nyumba ya uzazi, tatizo lina root course. Consequences zake zinaweza kuchukua muda kujitokeza kama hatua za makusudi kung'amua root course hazitachukuliwa kwa wakati muafaka.
 
Pili breeding ya siku 9 mpka 10 ni normal? na kama mwenzi wako yuko hivi ndo anakuwa kwenye cycle ipi? ni haya tu.

I hope unamaanisha, bleeding. Hiyo sio normal. Ni dalili ya matatizo kwenye nyumba ya uzazi, tatizo lina root course. Consequences zake zinaweza kuchukua muda kujitokeza kama hatua za makusudi kung'amua root course hazitachukuliwa kwa wakati muafaka.[/QUOTE]

Kuna watu wengine huwa wanaanza kuona dalili wiki1 au na nusu kabla na huwa vinatoka kama vitone.Na siku ya kubreed rasmi breeding inakuwa ndogo sana hata kama itaenda siku nne.Is it normal ? au ni tatizo?
 
sio leo wala kesho!.....😀😀(this is MY WISH,mwenzangu sijui anawaza nini)

Hahahahahhaa.Naheshimu 'wish"yako.Ila ushauri wangu ni huu:

Kwa vile unayomazingira tayari,its better ukapata watoto ungali bado kijana,na badae ibakie kazi ya kulea tu.Usisubiri kuzaa watoto uzeeni wakawa kama wajukuu.
Ni mtizamo tu lakini.
 
Hahahahahhaa.Naheshimu 'wish"yako.Ila ushauri wangu ni huu:
Kwa vile unayomazingira tayari,its better ukapata watoto ungali bado kijana,na badae ibakie kazi ya kulea tu.Usisubiri kuzaa watoto uzeeni wakawa kama wajukuu.
Ni mtizamo tu lakini.
Noted! nitaupeleka muswada huu serikali kuu FOR MORE DISCUSSIONS
 
Hahahahahhaa.Naheshimu 'wish"yako.Ila ushauri wangu ni huu:
Kwa vile unayomazingira tayari,its better ukapata watoto ungali bado kijana,na badae ibakie kazi ya kulea tu.Usisubiri kuzaa watoto uzeeni wakawa kama wajukuu.
Ni mtizamo tu lakini.
samahani kidogo,
HIVI WATOTO WANAPATIKANAJE?????😀😀😀
 
samahani kidogo,
HIVI WATOTO WANAPATIKANAJE?????😀😀
Soma maelezo hayo chini nimekopi na kupesti.Kwa kuongezea ingia magotini pia kwa kuwa mambo haya huwa hayatabiriki.

Wakuu,

Nakubaliana kwa kiasi fulani na wachangiaji wengine waliotangulia. Lakini natofautiana nao juu ya jambo moja tu, nalo ni namna wanavyoweza kui-pin point siku ile ya kilele (i.e fruitful/productive/fertile day), hapa nina maana ya siku ile ambayo wao wanaiita siku ya 14.

Ikumbukwe kuwa wanawake wanatofautiana katika suala zima la urefu wa MENSTRAL CYCLE, yaani idadi ya siku kati ya period ya kwanza hadi ile ya pili inayofuatia. Kundi kubwa la wanawake wana fall kwenye range ya siku 22-35. Japo walio-normal wana siku 28. Vile vile kuna wengine huwa na menstral cycle mbili, yaani fupi na ndefu. Hivyo walio na menstral cycle fupi, mathalani wale wenye siku 22, huwa vilevile wana kipindi kifupi sana cha kutokwa na damu (period), yaani damu inaweza kukatika ndani ya siku 2 tu! Na wale wenye siku 35 au zaidi huwa wana kipindi kirefu sana cha kutokwa na damu (period) ambapo wengine huwachukua hata siku kati ya 5 hadi 8.

Hivo basi, kama wewe ni mwanaume inakubidi umwelewe vizuri mwenzi wako juu ya hayo niliyoyasema hapo juu ili ikusaidie kui-pin point ile fertile day (yaani siku ya mimba).

Swali: Je siku ya mimba ni ipi?

Jibu lisilosahihi: Watu wengi na hata baadhi ya wanasayansi wanafikiri siku ya mimba ni ile ya 14 baada ya dalili za kwanza za damu ya hedhi! Wao huhesabu kuanzia siku ile damu ilipoanza kutoka hadi siku ya 14! Utaratibu huu ume-prove failure! Hii ni kwa sababu wanawake wana menstral cycle zinazotofautiana kwa urefu. Hivo basi jibu sahihi ni hili hapa chini:

Jibu sahihi:
1. Kwanza inabidi ujue kama mwenzi wako ana menstral cycle ipi? Fupi au ndefu, ama zote mbili?

2. Baada ya kujua urefu wa menstral cycle ya mwenzi wako then pin point siku ile ya mwisho halafu uhesabu backwards siku 15 kuanzia siku ile ya mwisho. Siku hii ya 15 kuanzia mwisho ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote!

Once you know the '15th day' from the last one, then you can manoeuvre whatever you want to get her pregnant or to avoid pregnancy!

With this new approach of pin pointing the fertile day you will find that all women (menstral cycles) are covered, whereas the old way of counting fits only to women whose menstral cycles are 28 days!

Mkuu Mr. Kiroboto,

Naomba nitoe mifano hai kwa faida ya dada zetu na wengine:

1. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 22 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa chini:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd.

Kisha ahesabu kuanzia ile 22nd day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 8th day ya kalenda yake. Hivo 8th day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 22. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!


2. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 28 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa chini:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th.

Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 14th day. Inamaana kwamba 14th day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 28. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!


3. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 35 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa chini:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th, 29th, 30th, 31st, 32nd, 33rd, 34th, 35th.

Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 21st day. Inamaana kwamba 21st day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 35. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!


4. Kama mwanamke ana abnormal menstration cycle ya siku 15 , BASI KUNAUWEZEKANO WA KUTOPATA MIMBA KABISA KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI:

Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama kawaida:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th.

Kisha ahesabu kuanzia ile 15th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 1st day. Inamaana kwamba, the 1st day of her bleedind ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 15. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed, na ndiyo hiyo hiyo siku ambayo mwanamke wa kundi hili anaweza kupata mimba!

Hii inamaana kwamba, siku ambayo linaharibika lile yai la upande mmoja ndiyo siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili linapevuka tayari kwa kurutubishwa. Mwanamke wa aina hii anaweza kupata mimba tu kama atakutana na mwanaume siku ile anayoanza kubleed, kwani siku ambayo yai moja linaanza kuharibika ndio siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili linakuwa tayari kurutubishwa!

Na wanawake wa kundi hili la nne ukiwauliza vizuri watakiri kwamba hawajawahi kuona au ku-feel ule ute mweupe ambao wenzao huwa wanaupata siku ile yai linapokuwa tayari kwa kurutubishwa, kwani ute wa wanawake wa kundi hili la nne huwa unachanganyikana na damu kwa vile unatoka siku ile ile wanapoanza ku-bleed. Pia wanawake wa kundi hili huwa wanatokwa na kiasi kidogo sana cha damu; na bleed hukatika ndani ya siku moja au mbili tu!

Jambo la kushangaza ni kwamba, wanawake wengi hawana knowledge ya kutosha juu ya hili suala la siku ya mimba; hasa wale ambao wana menstration cycle inayobadilikabadilika! Wao husitukia tu wameanza ku-bleed. Ndo maana hawawezi hata ku-plan kutopata mimba! Hawana ujanja kabisa ndio sababu wengi wanatumia sindano na njia zingine nyingi za artificial ambazo mwisho wa siku huwaletea matatizo ya uzazi, kwani nyingi hu-block njia ya uzazi! Nimeona wengi wenye matatizo ya uzazi unaosababishwa na hizi artificial family planning. Wengine hulazimika kwenda hospital kuzibuliwa ili wapate mimba jambo ambalo ni hatari kwa afya zao!
 
Soma maelezo hayo chini nimekopi na kupesti.Kwa kuongezea ingia magotini pia kwa kuwa mambo haya huwa hayatabiriki.
Nimesoma bwana. Nimeprinti nyingine 'copi ya serikali kuu'
 
Yep ni kweli pia tarehe 17th na 18th kwa mtiririko wa huyu bwana, una uwezekano mkubwa kupata mtoto wa kiume ---
 
Yep ni kweli pia tarehe 17th na 18th kwa mtiririko wa huyu bwana, una uwezekano mkubwa kupata mtoto wa kiume ---

Duuhhhhhh, wanaJF kuweni makini na ushauri mnaoupata hapa. In the pool of living organisms, every organism is unique.


Always remember that you are unique, that worked for someone is not necessary that its works for you.
 
Back
Top Bottom