Tarehe/siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa

Mimi mke wangu anajifunga kijiti kiunoni kama yuko kwenye hatari ya kupata mimba na mimba haiingii, tmefanya hivyo kwa muda wa mika 15 sasa

Fungwe hicho kijiti mmekipata wapi? Niliwahi kusikia Hospitali wana njia hiyo ya kuweka kijiti,,lakini wao wanaingiza ndani ya mwili (chini ya ngozi) sasa wewe chako kinafungwa kiunoni! MAKUBWA HAYO!

Au mlikichukua MVUMONI kwa KALUMANZILA??
 
kungurumweupe,
Nakushukuru sana kwa maelezo yako mazuri.

Hata hivyo naomba kutofautiana nawe kuhusu theory ya watoto zaidi ya mmoja yaani twins,triplets,nk.
1.Unasema mbegu zaidi ya moja zikirutubisha yai moja,basi yai hilo litagawanyika kulingana na idadi ya mbegu kutokeza " zygotes" kwa lugha rahisi "watoto" sawa na idadi ya mbegu za kiume.HII SI KWELI HATA KIDOGO MKUU.Hata siku moja ,haiwezekani mbegu zaidi ya moja kurutubisha yai lile lile moja.Daima,milele ,amina,mbegu moja ya kiume hurutubisha yao moja la kike.Ikumbukwe kua mara tu baada ya mbegu moja ya kiume kuingia ndani ya yai ,hutokea ukuta juu ya yai na chemical reactions nyingine kwenye yai ambazo huzuia mbegu nyingine ya kiume kuingia.

Nadharia,ya "Fratenal twins" yaani mapacha ambao si lazima wafanane,ambao huweza kuwa au wasiwe wa jinsia moja,ambao ni kama tu watoto wowote wa mama mmoja,hutokea pale ambapo mayai mawili ,kila yai kutoka ovary moja kulia na kushoto ,hutolewa wakati mmoja na hatimaye kurutubishwa na mbegu mbili za kiume,kila mbegu moja ikirutubisha yai la kwake.Watoto hawa huwa na placenta tofauti,kila mmoja ana placenta yake.Wanaweza kuwa wa jinsia moja au tofauti.Waweza kufanana au la.Kwa kifupi ni kama watoto wowote wa mama mmoja.Huwa huitwa FRATENAL TWINS au NON IDENTICAL TWINS.

2.nadharia yako kuwa kupatikana kwa watoto wawili au hufanana husababishwa na mbegu moja kurutubisha yai moja na kupatikana kwa muunganiko wa idadi ya chromosomes zaidi ya kiwango kinachohitajika,si kweli pia hata kidogo.Under normal circumstences muunganiko wa mbegu ya kiume na yai hutokeza zygote yenye chromosomes 46.Ikiwa itakua zaidi ya hapo ,basi mtoto atakua na malformations kama DOWNS SYNDROME n.k na si kua basi itagawanyika kusababisha twins,triplets etc.

Identical twins au Non fratenal twins hutokea pale ambapa mbegu moja hurutubisha yai moja,na kutokeza zygote yenye idadi inayohotajiwa ya chrosomes yaani 46 lakini wakati wa kuzalishwa na kuongezeka kwa chembe hai "cells" kitu ambacho hufanyika kwa speed kubwa sana,, katika hatua ya moja inayoitwa "morulla" ,kwa sababu nyingi including genetic factors and other unknown factors,hiyo morula huweze kugawanyika katika parts zinazolingana tuseme mbili,na kila part kukua independently na kuwa mtoto.Watoto hawa hukua katika placenta moja,wanapozaliwa wanafanana kila kitu kwani walitokana na mbegu moja ya kiume na yai moja la kike hivyo genetic yao {chembe zao za urithi } huwa sawa kwa asilimia mia moja.

Ndio maana huitwa IDENTICAL TWINS,TRPLETS,etc.Ila baada ya kuzaliwa kutokana na mazingira labda pia na nutritional differences kati yao,watoto hawa mara nyingi kufanana kwao hupungua taratibu.
Lakini nakubaliana nawe kwa maelezo yako mengine,isipokua haya.
I stand to be corrected.

Naomba kuwakilisha.
 
Kungurumweupe asante ; Heshima mkuu!!

Swali langu mie kama mwanaume nitazigunduaje hizo cycle yaani how do i tell kuwa hii ni 22, 28 na 35 etc ikiwa nataka kutegesha nimnasishe?

Pili breeding ya siku 9 mpka 10 ni normal? na kama mwenzi wako yuko hivi ndo anakuwa kwenye cycle ipi? ni haya tu.
 
Nimeikumbuka tipic ya REPRODUCTION form two 'B'
 
....
Pili breeding ya siku 9 mpka 10 ni normal? na kama mwenzi wako yuko hivi ndo anakuwa kwenye cycle ipi? ......




I hope unamaanisha, bleeding. Hiyo sio normal. Ni dalili ya matatizo kwenye nyumba ya uzazi, tatizo lina root course. Consequences zake zinaweza kuchukua muda kujitokeza kama hatua za makusudi kung'amua root course hazitachukuliwa kwa wakati muafaka.
 
Pili breeding ya siku 9 mpka 10 ni normal? na kama mwenzi wako yuko hivi ndo anakuwa kwenye cycle ipi? ni haya tu.

I hope unamaanisha, bleeding. Hiyo sio normal. Ni dalili ya matatizo kwenye nyumba ya uzazi, tatizo lina root course. Consequences zake zinaweza kuchukua muda kujitokeza kama hatua za makusudi kung'amua root course hazitachukuliwa kwa wakati muafaka.[/QUOTE]

Kuna watu wengine huwa wanaanza kuona dalili wiki1 au na nusu kabla na huwa vinatoka kama vitone.Na siku ya kubreed rasmi breeding inakuwa ndogo sana hata kama itaenda siku nne.Is it normal ? au ni tatizo?
 
sio leo wala kesho!.....πŸ˜€πŸ˜€(this is MY WISH,mwenzangu sijui anawaza nini)

Hahahahahhaa.Naheshimu 'wish"yako.Ila ushauri wangu ni huu:

Kwa vile unayomazingira tayari,its better ukapata watoto ungali bado kijana,na badae ibakie kazi ya kulea tu.Usisubiri kuzaa watoto uzeeni wakawa kama wajukuu.
Ni mtizamo tu lakini.
 
Hahahahahhaa.Naheshimu 'wish"yako.Ila ushauri wangu ni huu:
Kwa vile unayomazingira tayari,its better ukapata watoto ungali bado kijana,na badae ibakie kazi ya kulea tu.Usisubiri kuzaa watoto uzeeni wakawa kama wajukuu.
Ni mtizamo tu lakini.
Noted! nitaupeleka muswada huu serikali kuu FOR MORE DISCUSSIONS
 
Hahahahahhaa.Naheshimu 'wish"yako.Ila ushauri wangu ni huu:
Kwa vile unayomazingira tayari,its better ukapata watoto ungali bado kijana,na badae ibakie kazi ya kulea tu.Usisubiri kuzaa watoto uzeeni wakawa kama wajukuu.
Ni mtizamo tu lakini.
samahani kidogo,
HIVI WATOTO WANAPATIKANAJE?????πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
samahani kidogo,
HIVI WATOTO WANAPATIKANAJE?????πŸ˜€πŸ˜€
Soma maelezo hayo chini nimekopi na kupesti.Kwa kuongezea ingia magotini pia kwa kuwa mambo haya huwa hayatabiriki.


 
Soma maelezo hayo chini nimekopi na kupesti.Kwa kuongezea ingia magotini pia kwa kuwa mambo haya huwa hayatabiriki.
Nimesoma bwana. Nimeprinti nyingine 'copi ya serikali kuu'
 
Yep ni kweli pia tarehe 17th na 18th kwa mtiririko wa huyu bwana, una uwezekano mkubwa kupata mtoto wa kiume ---
 
Yep ni kweli pia tarehe 17th na 18th kwa mtiririko wa huyu bwana, una uwezekano mkubwa kupata mtoto wa kiume ---

Duuhhhhhh, wanaJF kuweni makini na ushauri mnaoupata hapa. In the pool of living organisms, every organism is unique.


Always remember that you are unique, that worked for someone is not necessary that its works for you.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…