Mimi ni binti, nina umri wa kutosha kabisa, sina mtoto ila sasa nimejiwekea malengo mwaka huu nipate mimba na nizae mtoto. Basi nikajaribu January 6 ilikuwa siku ya 14 tangu ni-bleed ikawa bila, nikijaribu tena february siku ya 11,12 na 13 tangu nibleed nayo naona bila leo nimejaribu kwenda hospitali.
Kuonana na Dr. mmoja hivi wa wanawake na kanieleza yaleyale na kusema huwa hawafanyi chochote kwa mtu ambae hajakaa kwenye ndoa mwaka mmoja na mume akakosa mtoto. Yeye kasema nijaribu at least wiki moja kuanzia siku ya kumi.
Sasa mume mwenyewe yuko mbali na mimi niko mkoani kikazi, nilimfuata mara mbili imeshindikana. Nataka nijaribu hii ya tatu na nimemaliza bleed jana, nilianza tarehe 19.
Ushauri tafadhali Dr, kama unao tofauti na alionipa Dokta au kwa kuongezea. Natanguliza shukrani zangu.