Nyadunga...hii njia inakuwezesha kuongeza kwa kiasi kikubwa 'uwezekano' wa kupata mtoto wa kiume, lakini sio lazima kupata mtoto wa kiume ukifuata njia hii. Njia ya uhakika zaidi (kama una hela) ni kurutubisha yai nje ya tendo la ndoa (In-Vitro Fertilization).

Njia hii kama alivyokuambia mpita Njia...inafuata 'timing' ya mzunguko wa mwezi wa mwanamke, hivyo shati uelewe mzunguko wa mkeo ( ni mrefu zaidi ya siku 28, au siku 28, au mfupi chini ya siku 28) kwani hii hubadlisha timing ya tarehe/siku za kufanya tendo.

Kwa kawaida, genetically binadamu ana chromosomes X na Y (usijali sana hiki ni nini), akiwa na XX basi huyo ni mwanamke..na akiwa na XY basi huyo ni mwanamume. Wakati wa kutunga mimba, mtoto anapata nusu ya chromosome toka kwa yai la mama (X) na nusu toka kwa mbegu ya baba (X au Y). Kwa hiyo yai la kike mara zote ni X na mbegu ya kiume ni aidha X au Y.

Manii (kumradhi..shahawa) inapomwagwa ina mbegu za kiume zaidi ya milioni kwa goli moja, mbegu hizi ni mchanganyiko wa X na Y. Ila sasa, mbegu X na Y zina tabia tofauti..

- X zinaishi muda mrefu (hadi siku 3), lakini ziko slow...hivyo zikimwagwa huchukua muda mrefu kulifikia yai na kulirutubisha

- Y zinaishi muda mfupi (siku 1 na nusu), lakini ziko fast...hivyo zikimwagwa huwai kulifikia yai na kulirutubisha kama limeiva vya kutosha.

Sasa hapo ni kucheza na timing tu mkeo anatoa yai lini kutokana na urefu wa mzunguko wake wa mwezi. Yai likitolewa linakuwa halijakomaa na ukuta wake mgumu kwa mbegu kupenya, inachukua siku 1 na nusu hadi 2 kwa yai kumature na ukuta kuwa laini kupenywa na mbegu. Hivyo ukishanote siku ambayo mkeo anatoa yai (yai hutolewa kati kati ya mzunguko...usually siku ya 14 au 15 ya mzunguko) ongeza siku 2 then mfanye tendo, hapo assumption ni kuwa yai litakuwa limeiva na ukuta laini, na ukimwaga mbegu basi zile Y ambazo ni za kiume zitawahi na kurutubisha yai kabla ya X ambazo ni za kike. Hapo unazaa mtoto wa kiume.

Kwa hiyo basi, kuna uwezekano mkubwa sana wa kuzaa mtoto wa kiume kama utafanya tendo na mkeo siku ya 16 na/au 17 ya mzunguko tangu mkeo aanze bleeding!