Njoo kwangu nina uwezo wa kutoa mapacha
Kwani muuliza swali amekwambia yeye hana watoto mzee, soma vizuri, umerukia tu kuzungumza kilichokujaa moyoni bila hata kuwa na ufahamu...aje kwako una uwezo wa kutoa mapacha? kwanza yeye anayeleta mada anaonekana mwanaume...na wewe unatamba kuwa unao uwezo wa kutoa mapacha, kama Mungu asingekusaidia kuwa na watoto mapacha unaoringa nao kiburi ungekitoa wapi, si ungekuja hapa unalialia kuomba msaada...nenda katubu hii dhambi uliyoifanya hapa haraka sana.....kuna watu hapa wana tatizo la kupata watoto, na wewe umekuja kuwapiga msumari kwamba waje kwako utatoa mapacha, hivi umeongea toka moyoni mwako kweli?, haumwogopi Mungu, haujui kama Mungu anaweza akakufanya lolote sasahivi kisisimame tena tuone hao mapacha unaowaumiza wenzio moyo utawatoaje, haujui kama Mungu huwainua wale wanyenyekevu na kuwashusha wenye kiburi, Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema....kwa kukusaidia, nenda katubu kwa Mungu, utapona, la sivyo, Mungu atakushusha ili uwe sawa na wamama na wababa wengi wenye shida ya kupata watoto humu jf.
Kama kuna mtu humu amepata watoto, hebu piga magoti mshukuru Mungu. however, kwa wale ambao hawapati mimba, naomba wamsubiri Mungu, mwombeni Mungu atawapa watoto hakika, Mungu humweka nyumbani mwake mwanamke aliyetasa ili awe mama wa watoto wenye furaha, furahi ewe uliye tasa, kwasababu watoto wake yeye aliyeachwa ni wengi kuliko wa yule asiyeachwa...Mungu wako atakupigania endapo utamkumbuka na kumheshimu.....nimepokea watu wenye tatizo kama hili wengi sana, wengine wamekaa miaka hadi kumi hawapati, lakini Mungu anawasaidia, wananyonyesha, Mungu wetu anao uwezo wa kukupatia watoto, watoto ni zawadi toka kwa Mungu wala msiumize kichwa...mwaminini Mungu, mwombeni, msubirini, msiumize moyo bure, mnapozidi kuumiza moyo ndipo inavyozidi kuwa vigumu kibiologia kutunga mimba kwasababu ya stress etc.
Na kiimani, mtu yeyote amwendeaye Mungu pasipo imani hapati kitu, na jambo lolote likitendwa bila imani ni dhambi....hivyo umwendeapo Mungu kama unaona haumwamini, bora usiende kabisaaa, ukienda kwa kumwamini kuwa ANAWEZA YOTE, lazima ataonekana kwako ktk jambo unaloliomba... tulia kimya ili Mungu atakapojitokeza ujue kuwa yeye ni Mungu, tulia mngoje Mungu, Be still and know that he is God, yeye atatukuzwa milele, neno hili Mungu mwenyewe husema (be still and know, I am God), akimaanisha kuwa, usiwe na wasiwasi, usihofu, usiwe na mashaka, alimradi unamwamini, mngojee, usifikiri kama yeye hawezi, HE IS GOD, that is what he means.....Mungu awabariki.