hakuna mtume yeyote au nabii yeyote aliyekuwa mkristo..
Mafundisho yote ya kwenye biblia ya kale ndo Mafundisho ambayo walikuja nayo mitume wote mpaka Muhammad alipofika.ya Mungu mmoja.
Mungu anasema, 'watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa'. Ndiyo maana leo hii mpaka tuna watu wanajilipua na kuua watu wengine, wakiamini wakifanya hivyo, watafika ahera na kupewa tuzo. Watu hawa ni dhahiri wanafanya kazi ya shetani, wamepofushwa na kuondolewa maarifa, na kuhadaiwa na Ibilisi kuwa wanafanya mapenzi ya Mungu.
Katika Ulimwengu wa kale, kila jamii ilikuwa na mungu wao. Wayahudi, Mungu wao alikuwa ni Mungu wa Ibrahim, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo. Mungu huyu alijifunua kwa Wayahudi pekee, ndiyo maana hata Musa anapowaletea waisrael zile amri 10 za Mungu, zinatanguliwa na maneno, "Mimi ndiye Mungu wenu niliyewatoa toka utumwani Misri".
Wamisri baada ya kupata mapigo toka kwa Mungu wa Ibrahim, Mungu wa Israel, wakati wanawafuata Waisrael, walitamka, "tukazane kwani Mungu WAO anawapigania" , wanasema Mungu 'wao', hawasemi Mungu wetu, kwa sababu wao walikuwa na miungu yao.
Maandiko yote ya vitabu vya kale viliwalenga wayahudi. Maagizo yote ya vitabu vya kale yalilenga kuandaa mazingira ya kumpokea masiha, na manabii wakapewa ishara za huyo masiha, lakini wanadamu hata walipoletewa huyo masiha, akafanya ishara zote waluzoambiwa na manabii wa kale, bado hawakumtambua, wala hawakumpokea, waliompokea aliwafanya wana wa Mungu, akawafunulia siri za ufalme wa mbinguni, na ni yeye alilitengeneza Agono Jipya, ambalo sasa likawa siyo kati ya Mungu na wayahudi pekee, bali na watu wa Ulimwengu mzima. Na akawaamuru mitume wake kwenda Ulimwengu mzima kuwafikishia wanadamu wote ujumbe wa Mungu. Anayekubali, anabatizwa na kuwa kiumbe kipya cha Mungu.
Ni kweli kuwa kabla ya Kristo, hakukuwa na ukristo kwa sababu ukristo ni kwa wanadamu wote, lakini agano la kale lilikuwa kati Mungu na wayahudi likitengeneza mazingira ya kumpokea masiha/Kristo atakayewaunganisha wanadamu wote kwa njia ya damu yake takatifu, na baada ya hapo kuifuta sadaka ya damu.
Baada ya Masiha/Kristo kuja Ulimwenguni kwa umbile la mwanadamu, kuendelea kung'ang'ania mafundisho ya kale yaliyokuwa na kusudi maalum, ni kuukataa wokovu.