Mzunguko wako wa maisha ni namba 6, endelea kufatilia nitatoa maelezo ya kina lakini kwa ufupi
Unatakiwa ujifunze kuyakubali majukumu kwa kuwa Mungu amekujalia uwezo mkubwa wa kusaidia na kufariji wengine pale inapohitajika. Tegemea watu wengi kuja kwako ili kupata msaada na faraja zaidi ya vile unavyofikiri ivyo ni muhimu kuyakubali majukumu na kujifunza namna kusaidia familia, ndugu na marafiki. Ni muhimu kujifunza kujitoa katika urafiki na matendo ya upendo kwa kuwa kile unachopanda ndicho utakachovuna, ni muhimu kutofautisha kati ya kusaidia na kuingilia mambo ya wengine.