Tarehe ya kuzaliwa na utabiri wa kesho yako

Tarehe ya kuzaliwa na utabiri wa kesho yako

Sehemu ya Kwanza

Tarehe ya kuzaliwa uwa inabeba taarifa zote muhimu kuhusu maisha ya muhusika na hii ni kwa mujibu wa elimu ya namba (Numerology). Katika hatua ya mwanzo nitaanza kwa kuzungumzia kitu muhimu ambacho kinapatikana kwa kukokotoa tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa, kitakachopatikana katika ukokotozi huo kitaitwa Mzunguko wa maisha (Tafsiri Binafsi). Kuna mambo muhimu ya kuzingayia katika ukokotozi wa mzunguko wa maisha ambayo ni namba mama na namba kiongozi.

Namba Mama
Namba mama ambazo zitakuwa zikitumika katika uchambuzi ni 1,2,3,4,5,6,7,8,9, namba yoyote baada ya 9 inaweza kurudiswa katika namba mama. Zingatia mfano unaofuata
10=1+0= 1
27= 2+7= 9=
389= 3+8+9=20=2+0=2

Kila namba mama kuanzia namba 1 hadi 9 inakuwa imebebe nguvu maalum, na hiyo nguvu inakuwa imegawanyika katika pande mbili, nguvu chanya na nguvu hasi.

Namba Kiongozi
Namba kiongozi ni namba ambazo zina sifa maalumu, nazo ni 11 na 22, namaba hizi zinapojitokeza wakati wa kukokotoa uwa zinabaki kama zilivyo, zingatia mifano ifuatayo;
155= 1+5+5=11
949=9+4+9=22

Namba hizi zinakuwa zimebeba sifa za Namba Mama na Namba Kiongozi, zingatia mfano ufuatao;

155= 1+5+5=11=1+1=2
949=9+4+9=22=2+2=4

Wakati mwingine hizo Namba Kiongozi uwa zinaandikwa 11/2 na 22/4.

Sehemu ya Pili

Mzunguko Wa Maisha​
Mzunguko wa maisha ni funguo ya kufungua kile ambacho mwenyezi Mungu amekiweka ndani yako wakati wa kukuumba. Hii ni namba ya kudumu katika kipindi chako chote cha uhai, daima haitabadilika kwa kuwa inatokana na tarehe yako ya kuzaliwa.
Mzunguko wa maisha utakuwezesha kutambua mambo unayotakiwa kuyatimiza katika kipindi chako cha uhai kwa kuzingatia fursa na vipaji ambavyo Mungu amekuumba navyo. Mzunguko wa maisha utakuwezesha kwa urahisi kufanya maauzi kuhusu;
Uelekeo wa maisha
Kupanga na kutimiza Malengo
Mahusiano
Mipango ya mbeleni
Kazi ambayo itakufikisha katika kilele cha mafanikio

Hivyo basi Mzunguko wa maisha utatuwezesha kutambua mazingira ambayo yataambatana na fursa ambazo Mungu ameziumba kwa ajili yako.

Mzunguko wa maisha ni namba inayopatikana kwa kuzipunguza tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa hadi kufikia katika Namba Mama au Namba Kiongozi, mfano wa kwanza unahusu Namba Mama na wa pili unahusu Namba Kiongozi

Mfano wa kwanza 21/04/1990
Tarehe 21= 2+1 = 3
Mwezi 04= 0+4= 4
Mwaka 1990=1+9+9+0=19=1+9=10=1+0= 1

Baada ya kupata hizo Namba Mama kutoka katika tarehe ya kuzaliwa, mwezi na mwaka unazijumlisha zote;
3+4+1=8
Mfano wa pili 14/01/1985
Tarehe 14= 1+4 = 5
Mwezi 01= 0+1= 1
Mwaka 1985=1+9+8+5=23=2+3=5

Baada ya kupata hizo Namba Mama kutoka katika tarehe ya kuzaliwa, mwezi na mwaka unazijumlisha zote;
5+1+5=11

Itaendelea.............................
Alfu lela ulela
 
hahaha mchangieni hela ya bando atakuwa ameishiwa!!!
 
Nimeenda sawa na mfumo ulio drop nimepata Total 11, So what next Fanta?
 
Nimeenda sawa na mfumo ulio drop nimepata Total 11, So what next Fanta?
hiyo ni namba kiongozi endelea kufuatilia uzi nitatoa maelezo yake kwa kina, lakini kwa ufupi

Mtu mwenye mzunguko wa namba 11 ni lazima uwe na uelewa mpana wa masuala ya kiroho na mahusiano yake katika maisha yetu ya kila siku hapa duniani. Mtu mwenye mzunnguko huu ana faida ya ziada katika kuelewa na kufahamu mambo ukilinganisha na watu wa mizunguko mingine.

Jambo la kuzingatia ni kuwa huu uelewa na ufahamu vinachukua muda ili kujijenga na vikishajijenga mtu mwenye mzunguko huu anakuwa na uwezo wa kukamilisha mambo ambayo watu wa mizunguko mingine hawawezi kuyakamilisha kwa urahisi. Mtu mwenye mzunguko huu pia ni lazima kujifunza kuamini na kuboresha uwezo wake wa kupata maono uwe unaongozwa kiroho.
Lazima ujitambue kuwa wewe ni njia katika kuhakikisha kuwa unainua maisha ya watu wengine kwa kuwapatia mwanga kupitia uwezo mkubwa wa ufahamu na uelewa wa mambo.
 
Kaka unasema kweli maana kuna muda huwa najiogopa kwa uwezo nilio nao, mtaani wanasema mimi ni usalama wa Taifa, Wenye shida wanaamini mimi ndio mtetezi wao, Mfano mkuu wa Nchi kazaliwa 29 October na mimi nimezaliwa 30 november tofauti ni namba 1 kwenye tarehe na mwezi tofauti ni moja bahati mbaya nimeishia darasa la saba lakini maisha yangu kama nimemaliza vyuo vyote. Please nipe neno zaidi kaka.

Sawa, endelea kufatilia maana namba haijawai kudanganya, utayajua mengi kuhusu hiyo 11.
 
Sawa, endelea kufatilia maana namba haijawai kudanganya, utayajua mengi kuhusu hiyo 11.
Asante sana kaka na nashukuru maana nahisi hii mada kama umeleta kwa ajiri yangu, ukizingatia kesho ni 30 November ni siku yangu ya kuzaliwa.
 
Back
Top Bottom