Rozanna Agro Africa
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 809
- 793
Malizia tuone uongo wako
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mm sielewi na sijawahi kuelewa,mm katika maisha yangu karibu kila kitu kikubwa iwe mafanikio,ndoa, lazima iwe either tarehe 11 au tarehe 29.kwenye swala la ajira iwe kuajiriwa ama kuachishwa kazi lazima iwe tar 11 mwezi wa pili au 11 mwezi wa may,na ikifika mwezi wa 10 kila mwaka lazima nisafiri mbali na nyumbani(hili la safari nimelifuatilia zaidi ya miaka 20).na kila mwaka mwezi wa pili lazima nisingiziwe kitu.ni vitu vingi sana lkn sielewi au labda sina elimu ya namba.Usikariri ndugu, inaonekana haya ni maarifa mapya sana kwako.
Utanishtua mkuu nipate somoSehemu ya Kwanza
Tarehe ya kuzaliwa uwa inabeba taarifa zote muhimu kuhusu maisha ya muhusika na hii ni kwa mujibu wa elimu ya namba (Numerology). Katika hatua ya mwanzo nitaanza kwa kuzungumzia kitu muhimu ambacho kinapatikana kwa kukokotoa tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa, kitakachopatikana katika ukokotozi huo kitaitwa Mzunguko wa maisha (Tafsiri Binafsi). Kuna mambo muhimu ya kuzingayia katika ukokotozi wa mzunguko wa maisha ambayo ni namba mama na namba kiongozi.
Namba Mama
Namba mama ambazo zitakuwa zikitumika katika uchambuzi ni 1,2,3,4,5,6,7,8,9, namba yoyote baada ya 9 inaweza kurudiswa katika namba mama. Zingatia mfano unaofuata
10=1+0= 1
27= 2+7= 9=
389= 3+8+9=20=2+0=2
Kila namba mama kuanzia namba 1 hadi 9 inakuwa imebebe nguvu maalum, na hiyo nguvu inakuwa imegawanyika katika pande mbili, nguvu chanya na nguvu hasi.
Namba Kiongozi
Namba kiongozi ni namba ambazo zina sifa maalumu, nazo ni 11 na 22, namaba hizi zinapojitokeza wakati wa kukokotoa uwa zinabaki kama zilivyo, zingatia mifano ifuatayo;
155= 1+5+5=11
949=9+4+9=22
Namba hizi zinakuwa zimebeba sifa za Namba Mama na Namba Kiongozi, zingatia mfano ufuatao;
155= 1+5+5=11=1+1=2
949=9+4+9=22=2+2=4
Wakati mwingine hizo Namba Kiongozi uwa zinaandikwa 11/2 na 22/4.
Sehemu ya Pili
Mzunguko Wa MaishaMzunguko wa maisha ni funguo ya kufungua kile ambacho mwenyezi Mungu amekiweka ndani yako wakati wa kukuumba. Hii ni namba ya kudumu katika kipindi chako chote cha uhai, daima haitabadilika kwa kuwa inatokana na tarehe yako ya kuzaliwa.
Mzunguko wa maisha utakuwezesha kutambua mambo unayotakiwa kuyatimiza katika kipindi chako cha uhai kwa kuzingatia fursa na vipaji ambavyo Mungu amekuumba navyo. Mzunguko wa maisha utakuwezesha kwa urahisi kufanya maauzi kuhusu;
Uelekeo wa maisha
Kupanga na kutimiza Malengo
Mahusiano
Mipango ya mbeleni
Kazi ambayo itakufikisha katika kilele cha mafanikio
Hivyo basi Mzunguko wa maisha utatuwezesha kutambua mazingira ambayo yataambatana na fursa ambazo Mungu ameziumba kwa ajili yako.
Mzunguko wa maisha ni namba inayopatikana kwa kuzipunguza tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa hadi kufikia katika Namba Mama au Namba Kiongozi, mfano wa kwanza unahusu Namba Mama na wa pili unahusu Namba Kiongozi
Mfano wa kwanza 21/04/1990
Tarehe 21= 2+1 = 3
Mwezi 04= 0+4= 4
Mwaka 1990=1+9+9+0=19=1+9=10=1+0= 1
Baada ya kupata hizo Namba Mama kutoka katika tarehe ya kuzaliwa, mwezi na mwaka unazijumlisha zote;
3+4+1=8
Mfano wa pili 14/01/1985
Tarehe 14= 1+4 = 5
Mwezi 01= 0+1= 1
Mwaka 1985=1+9+8+5=23=2+3=5
Baada ya kupata hizo Namba Mama kutoka katika tarehe ya kuzaliwa, mwezi na mwaka unazijumlisha zote;
5+1+5=11
Itaendelea.............................
Siwezi kukupa jibu la moja kwa moja kwa kuwa sijafahamu mzunguko wako wa maisha ni namba ngapi ivyo nashindwa kukupa uchambuzi unaoendana na maarifa ya namba.mm sielewi na sijawahi kuelewa,mm katika maisha yangu karibu kila kitu kikubwa iwe mafanikio,ndoa, lazima iwe either tarehe 11 au tarehe 29.kwenye swala la ajira iwe kuajiriwa ama kuachishwa kazi lazima iwe tar 11 mwezi wa pili au 11 mwezi wa may,na ikifika mwezi wa 10 kila mwaka lazima nisafiri mbali na nyumbani(hili la safari nimelifuatilia zaidi ya miaka 20).na kila mwaka mwezi wa pili lazima nisingiziwe kitu.ni vitu vingi sana lkn sielewi au labda sina elimu ya namba.
Haya ndio yale yale ya Story za The BoldSa si ungejiandaa full kabisa, badala yake unakuja nusu nusu.
AiseeeeUlikuwa huna haja ya kuleta habari ambayo haijakamilika, ungesubiri wewe hiyo kesho kisha ukaleta full
Hapo Lumumba hamfundishwi hesabu?Sikuwahi kumpenda mwalimu wa hesabu.
Usiniharibie siku.
mimi tarehe yangu ni 21/9/1983 naomba niujue mwendendo wa mambo yangu kipitia namba..tafadhali kiongozi nisaidie hapoSiwezi kukupa jibu la moja kwa moja kwa kuwa sijafahamu mzunguko wako wa maisha ni namba ngapi ivyo nashindwa kukupa uchambuzi unaoendana na maarifa ya namba.
Mzunguko wako wa maisha ni namba 6, endelea kufatilia nitatoa maelezo ya kina lakini kwa ufupimimi tarehe yangu ni 21/9/1983 naomba niujue mwendendo wa mambo yangu kipitia namba..tafadhali kiongozi nisaidie hapo
Endelea kufatilia hili nisiharibu mtiririko wa somo ila kwa ufupiMzunguko Wangu wa maisha ni namba 9 .....Hebu nambie ndo inakuwaje hapo
Vipi kuhusu mafanikio inakuwaje kupitia namba hizo?Mzunguko wako wa maisha ni namba 6, endelea kufatilia nitatoa maelezo ya kina lakini kwa ufupi
Unatakiwa ujifunze kuyakubali majukumu kwa kuwa Mungu amekujalia uwezo mkubwa wa kusaidia na kufariji wengine pale inapohitajika. Tegemea watu wengi kuja kwako ili kupata msaada na faraja zaidi ya vile unavyofikiri ivyo ni muhimu kuyakubali majukumu na kujifunza namna kusaidia familia, ndugu na marafiki. Ni muhimu kujifunza kujitoa katika urafiki na matendo ya upendo kwa kuwa kile unachopanda ndicho utakachovuna, ni muhimu kutofautisha kati ya kusaidia na kuingilia mambo ya wengine.