TARIME: Kada wa CCM auawa kwa kisu katika ubishi wa kisiasa kati ya CCM na CHADEMA

TARIME: Kada wa CCM auawa kwa kisu katika ubishi wa kisiasa kati ya CCM na CHADEMA

Kuua mtu kisa hizo siasa uchwara ni uboya, ukizingatia usikute ni makada tu wala sio viongozi.

Mnauana kwa ajili ya watu wasio na maslahi na nyie.
 
Mbona hakuna Chadema ilipotajwa hapo?
Inawezekana Sukuma gang wameua mwana CCM unasema Chadema
 
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Sokoni Kata ya Sirari Wilayaní Tarime Mkoaní Mara, Moshi Sayi Maduhu, ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani karibu na shingoni baada ya kutokea ubishi wa kisiasa kati yake na mfuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Senga Shuri.

Kufuatia hali hiyo, Shauri ambaye ni fundi baiskeli anashikiliwa na Jeshi la Polisi kituo cha Sirari.

Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, ACP William Mkonda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema ilitokea Jumamosi Aprili 16, 2022 jioni katika Kitongoji cha Sokoni wakati wa ugomvi kati ya Maduhu na Shuri aliyekuwa na kisu kisha kumchoma kifuani na kumsababishia kifo.

Alisema mtuhumiwa amekamatwa na wanamhoji, baadaye atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Kamanda Mkonda alisema Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi katika Wilaya za Tarime na Rorya kuacha kutembea na silaha, na kwamba halitasita kuwachukulia hatua kali watu wote wanaokamatwa wakitembea na silaha na kujichukulia sheria mkononi badala yake kama kuna malalamiko watu waende kwenye vyombo husika ili haki iweze kupatikana.

Wakizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki Diwani wa Sirari kupitia CCM, Amos Sagara, Diwani wa Regicheri, John Bosko, Diwani wa Gwtiryo, Nashon Mchuma, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Sokoní kupitia CCM, Bob Benjamin, mjumbe wa mkutano mkuu CCM Wilaya ya Tarime, Laurent Nyablangeti.

Katibu Kata CCM, Kata ya Gwitiryo Hidaya Peter, Mwenyekiti wa Kijii cha Gwitiryo, Joseph Timuti na wanachama wa CCM kata hizo, walisema kuwa CCM Sirari na kata jirani za Gwitiryo na Regicheri wamepata pigo kubwa kutokana na kifo cha Maduhu.

Walisema kuwa Maduhu alikuwa kiongozi asiyependa kushindwa kwa jambo alilokuwa analitetea, kwamba amepigania chama chake hadi umauti unamkuta alinadi sera na ilani katika kata zote tatu bila kuchoka, na ameacha alama ya kujitolea.


Habari: Nipashe
Ukifuatilia nae ameua wengi wa upinzani. Siku hizi malipo ni hapa hapa
 
Ndio maana tunawaita nyumbu kichwa mzigo akili kisoda, apumzike amini kada
 
MaCCm na Machadema ni mapumbavu sana maccm yanajiona nchi ya kwao na machadema huko Twitter ukipishana nayo kimtazamo tu unakua adui yao wanakufukuza hadi Twitter Kama vile Wana hisa zao kule.
Wote hawastahili kuongoza nchi udikteta na uchu wa madaraka ni mwingi sana Kati yao, na wote wanatumika Kama misukule kunufaisha walio juu
 
Back
Top Bottom