Tarime, Mara: Mmiliki wa mabasi ya Zacharia awapiga risasi maafisa wa Usalama wa Taifa, ashikiliwa na Polisi

Tarime, Mara: Mmiliki wa mabasi ya Zacharia awapiga risasi maafisa wa Usalama wa Taifa, ashikiliwa na Polisi

Zakaria mafia sana; nakumbuka miaka flani hivi zamani alimchukua mzee mmoja mtoza kodi akampeleka hadi chini kabisa kwenye nyumba yake ya kufanyia mafia shimoni chini kabisa akimwonya kuhusiana na tabia yake ya kuzuia Mali yake.
Tokea hapo wakawa marafiki sana hadi leo hii.
 
Amesema kabla ya tukio hilo, maofisa watano wa Usalama wa Taifa walifika katika kituo cha mafuta kinachomilikiwa na Zakaria kwa nia kujaza mafuta kwenye gari lao, “ wenzao wawili walishuka kwenye gari ghafla wakashambuliwa kwa risasi na Zakaria aliyekuwepo eneo hilo.”
Haka ka paragraph kamejaa usanii sana!
Yaani mtu awashambulie kwa risasi kisa walishuka? ipo namna hapa
 
Ajengewe sanamu gani Peter zakaria. zakaria ni huyu tajiri aliyewatesa watu wa Tarime Kwa kuwaua ,aliyewadhulumu wa Mali zao mchana kweupe, aliyewasingizia watu kesi na kuwaweka kolokoloni.zakaria huyu aliyewahi kuwachapa viboko abiria waliokataa kushuka kwenye Busi lake baada ya kukatisha safari ghafla instead ya kuwafikisha sirari akalazimisha waishie Tarime mjini , zakaria huyu mkepa kodi na mfanyabiashara ya magendo, Zakaria huyu aliyepora na kujipatia Mali na majumba na ya chama cha ushirika cha Nyanza Jijini mwanza , zakaria huyu mwana CCM kindakindaki anayetumia jina mwamvuli wa chama kujinufaisha kiuchumi etc. Sanamu inajengewa watu kama Peter zakaria
Aisee hii kali.
 
Hatujui lengo la waliojaribu kumteka mdogo wangu Zakaria, lakini tunaamini hawakuwa na nia njema ndiyo maana walifika usiku bila taarifa kama wanaokwenda kukamata jambazi,” alisema Chomete.

“Tunamshukuru Mungu aliweza kupambana na watu kujitokeza kumsaidia. Pengine naye angepotea kama wengine wanaoripotiwa kupotea katika siku za hivi karibuni,” alisema.
Aisee!
 
“Tunamshukuru Mungu aliweza kupambana na watu kujitokeza kumsaidia. Pengine naye angepotea kama wengine wanaoripotiwa kupotea katika siku za hivi karibuni,” alisema.
 
Back
Top Bottom